Hata Galileo Galilei aliposema dunia inazunguka jua, na si kweli kwamba jua linazunguka dunia kama kanisa na Biblia inavyosema, aliambiwa kakufuru. Akafungiwa nyumbani kwake baada ya kuomba msamaha bila sababu ili tu asiuawe.
Biblia inasema Mungu ameisimamisha dunia, haizunguki. Hilo tu linatakiwa kukuonesha Biblia imeandikwa na watu, si Mungu. Tena watu ambao hawakuwa na elimu ya kujua dunia inazunguka.
Miaka 350 baadaye, kanisa katoliki limeomba msamaha na kusema Galileo alikuwa sawa.
Galileo alikuwa mbele zaidi ya kanisa katika kujua ukweli, kwa kutumia majaribio ya kisayansi.
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na habari za kuwapo huyo Mungu si hadithi za watu tu?
Habari ya kanisa kuomba radhi kwa kumhukumu Galileo kimakosa iliandikwa na The New York Times hapa chini.
Wengine mpaka leo tunahukumiwa kimakosa na wanadini kama alivyohukumiwa Galileo. Labda miaka 350 ijayo watu wataelewa ukweli.
www.nytimes.com
Mistari ya Biblia inayosema dunia haizunguki.
1 Chronicles 16:30: "He has fixed the earth firm, immovable."
Psalm 93:1: "Thou hast fixed the earth immovable and firm ..."
Psalm 96:10: "He has fixed the earth firm, immovable ..."
Psalm 104:5: "Thou didst fix the earth on its foundation so that it never can be shaken."
Isaiah 45:18: "...who made the earth and fashioned it, and himself fixed it fast