Mkuu, hapa tunazungumza kuhusu DINI-IMANI vs SAYANSI.
na hoja ya msingi hapa ni kwamba sayansi ina makosa hivyo si njia sahihi ya kutafuta majibu. Kwa kulijua hilo ume prefer vitabu vya dini na imani kiujumla kwamba ndio njia sahihi ya kuufikia ukweli, so kabla ya kuikubali njia hii tunatakiwa tuipime kama ina makosa ili tusipoteze muda kuitumia katika kutafuta majibu sahihi kwasababu tushajua kua mafundisho ambayo yamekosewa au yanamokosa ndani yake hayawezi kutoa jibu la uhakika.
Ili kufikia hitimisho kwa jambo lolote la Kidini mfano katika Biblia Imani inatumika kuliko hoja.
Imani ni kuamini kitu kipo bila evidence
Sasa tutajuaje majibu ya mambo yanayotutatiza kwa uhakika wakati msingi mzima wa imani ni betting???
Ili kufikia hitimisho kwa jambo lolote la Kisayansi, majaribio na hoja zinatumika kuliko imani ndipo tunafikia hitimisho.
Hitimisho gani zuri katika kutafuta ukweli kati ha hayo mawili?
Kuamini bila kujua kwa uhakika wa jambo hilo wala uthibitisho?? Au kua na majaribio ambayo yanaweza kua proved na kila mtu akajua ukweli??
So nikutake uelewe hilo kuanzia sasa.
Nami nataka nielewe vizuri ipi njia bora ya kujua ukweli wa jambo kwa uhakika? kati ya imani ambayo haina majaribio yanayoweza kuchunguzwa ili kufikia hitimisho lenye majibu ya maswali au sayansi yenye kufata kanuni hiyo ya majaribio ambayo yameambatana na uthibitisho???
Maelezo niliyokupa kwa mtu mwelewa, yanajitosheleza kabisa.
Kuelewa kwamba hueleweki, nimeelewa
Kwa mfano, Tofaa (Apple) kudondoka toka kwenye mti hadi chini inaleta Mantiki kwamba kuna kani inaitwa Gravity? Hayo maelezo yanajitosha?
Kama isivyowezekana nyoka kuzungumza na adam na eva
Kwangu Mimi hayajitoshi, na ndio maana naandika kitabu kuonesha namna Sayansi imetufanya wajinga kwa muda mrefu.
Hayajitoshi kwa vipimo gani? Hapa kipimo ni uhalisia katika kufananisha mambo
Sasa tunaona habari za punda na nyoka kuongea na binadamu zinapwaya kiuhalisia. je hii kwako ina make sense??
Tukio lililotokea pale Eden, haliwezi kuwa na shaka, kwa mfano nikikuuliza kwanini Mashariki ya kati ndiko mafuta mengi yanapatikana, Jibu unalo? Kwanini?
Nami pia naweza kukuuliza swali kupitia hiyo hoja uliyoijenga.
Hayo mafuta kwanini hayakugunduliwa kipindi chote cha kina yuda na petro (wakati kipindi icho biblia ndio ilikua inasomwa sana na kuaminiwa) mpaka sayansi ilivyokuja kusambaa ulimwenguni??
Hayo mafuta yanachimbwa hadi kufikia process yanakua pure kwa vifaa vilivyotengenezwa na watu gani??