Asante sana,sijawahi kushindwa kufanya hivyo,ila aliyeko dhidi yetu ndio ameshindwa kuonyesha kutokuwepo kwake.
Maarifa yanapatikana kwa njia hizi :
1. Milango ya fahamu.
2. Akili
3. Ufunuo.
Unaweza kutambua uwepo wa aliyeumbwa asie kuwa na chanzo kwa kutumia nyenzo hizo tatu hapo juu.
Mathalani kama "Simu" unayoitumia leo hii imekuwepo kabla ya kutokuwepo kwake kwa kusanifiwa na mjuzi wa jambo hilo,basi kwa binadamu na vilivyomo ni bora zaidi kuwa na chanzo.
Katika maumbile najua tulitoka kitambo sana. Lakini wakana Mungu wa leo wamejikita katika jambo moja ambalo ni dogo sana jambo lao wanaliita "The Problems of evil" huku sasa ndipo walipojificha lakini kwa hakika ni wao hawautaki tu ukweli,limekuja hili baada ya wao kushindwa kuthibitisha kutokuwepo kwa Mola muumba katika chanzo cha maisha na mfano wake.
Lakini ukanaji wao huu umejengeka katika ujinga na wasi wasi tele,nakupa wewe mfano tu mdogo kisha nitakupa ufafanuzi.
"Najua ishawahi kukutokea ya kuwa,unafanya jambo fulani ambalo unajua kabisa jambo hili ukilifanya lina madhara lakini unalifanya,na ukilifanya kweli unapata madhara". Hivi hapa nani wa kulaumiwa ?
Huo ni mfano tu wa kuanzia,nimeamua kukuanzia mbali labda hnaweza kuelewa.
Tofauti na kina
Kiranga kwao kumkana Mola muumba ni imani na ajabu imani yao haijangeka katika misingi ya kielimu bali ni ujinga. Na kufikiri kwao ni kufikiri kwa kitoto sana na nusu nusu.
Mathalani hivi hii dunia ingekuwaje tu kwamba waouvu wasije kuhukumiwa au mafisadi wasije kuhukumiwa au waonevu wasije kuhukumiwa ?
Naendelea ....