Kama ulisoma walau kuanzia elimu ya sekondari kuna vitabu tulivitumia kujibia kiingereza na Kiswahili.
Kuanzia kizazi changu kielimu cha miaka ya 1996 tulikuwa na wakina Okonkwo (Things fall apart), kina Sikamona ndani ya zawadi ya ushindi, Ngoswe, Mzee Toboa Mambo (Kiu ya Haki) na wengineo.
Walikuwepo pia kina Hawa the bus driver na Mabala the farmer kwa F1 na F2.
Tuliwajadili ma characters hawa na mpaka leo hii mtu ukimwambia afanye i margination ya Hawa the bus driver bila shaka atakwambia ni lijimama fulani lililojaa mwili na minguvu mingi.
Kwa kuwa characters hawa wana majina, tuliwajadili, tuliwahisi kifikira, tukawatamka na kujibia mitihani uhusika wao je,
Kwa maelezo yako wakina Okonkwo,Sikamona, Ngoswe, Mzee Toboa Mambo na Hawa the bus driver wapo kiuhalisia, nje ya dhana ya kufikirika?
Kivipi?
Kwani tukianza kujadili habari za kina Harakati za Pimbi,Kipepe,Lodilofa, Sokomoko na Ndumila kuwili wa gazeti la Sani enzi hizo, hapo tayari hao watu wanakuwa wapo kweli kiuhalisia, nje ya masimulizi ya kufikirika pekee!?
Unaelewa ya kwamba Mungu nae amebuniwa na kuingizwa ndani ya vitabu mnavyovisema vya Mungu, kama ambavyo kina Harakati za Pimbi walivyoingizwa ndani ya gazeti la Sani!?