Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Mimi naposhindwa kuelewa ni hapo kwamba mnapinga uwepo wa Mungu au mnapinga kwamba huyo Mungu hakuumba huu ulimwengu?Hivi unaelewa Mantiki ya maneno haya
Mungu muweza wa yote
Mjuzi wa yote
Mwenye upendo kwa wote '... Hizo ndio figure ambazo Zina mfanya huyo mungu wenu aonekane kuwa ni wakufikirika. ..
Mungu angekuwa ni muweza wa yote. .asingeumba dunia ambayo ina mapungufu kibao ..ikiwemo matetemeko. Maradhi. Njaa. Kifo. Na majanga ya kila Aina. ..uwepo wa hivyo vyote inadhihirisha kuwa maandiko yanayo tu taka tutambue kuwa mungu ni muweza wa yote Yana jipinga yenyewe -kwa sababu kama angelikuwa nimuweza wa yote kweli asingeiumba dunia yenye mapungufu kiasi hicho. ..
Mungu angekuwa ni mjuzi wa yote -- asinge muumba shetani wakati anajua kuwa atakuja kumsaliti " asinge wa agiza Adamu na Eva kuto kula tunda wakati anajua fika kuwa hawatoweza kuitekeleza amri yake --..Angekuwa ni mjuzi wa yote Asinge shindwa kuiumba dunia yenye mapungufu kiasi hiki ---
Mungu angekuwa ni mwenye upendo kwa wote ---asinge kuwa ana ya acha Mataifa yenye nguvu yazipige vita Mataifa dhaifu. .asinge acha matetemeko ya waue watu. ...wakiwemo watoto ambao hawana makosa yeyote. .......ilhali wakati huo huo Kuna watu wa Mataifa mengine wapo kwenye furaha -- hapo mantiki ya upendo wake kwa wote iko wapi --hauoni hapo hayo maandiko yanaonyesha kumpachika mungu sifa ambazo hana "" wakati binaadamu wengine Wana kufa kwa Njaa wengine Wana kula na kusaza '' ina maana huyu mungu ana double standard ---!!? Kama jibu ni ndio? Je huo upendo wake kwa wote uko wapi? ?
Je tukisema kuwa mungu hayupo kutokana na hizo sifa mnazo mpachika kutokuwa nazo itakuwa tunakosea? ?
So---Hivi hapo Mnacho shindwa haswa kumuelewa kiranga ni nini? ? Hamuoni kuwa vitabu vyenu vina muhubiri mungu ambaye ambaye hayupo na vitabu vyenu vinajipinga vyenyewe kudhihirisha hilo