Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

"contradiction" Ndiyo nini?.
Ukianacho wewe kuwa ni contradiction, kwangu mimi siyo contradiction.
Unawezaje sasa kunifanyia maamuzi ya kwamba hiki kipo hivi ili hali kwangu mimi hakipo hivyo?.

A billion dollars question.

Na ndio tatizo la atheists wote hili, contradiction anayoiona yeye, kwako sio contradiction na anajaribu kulazimisha iwe contradiction kwako pia. Na wanachofeli zaidi ni kwamba wanadhani wanajua kila kitu. Kimsing all atheists are materialists hawajui lolote kuhusu spiritual realm. Hawataki kujiongeza na kujifunza kuhusu spiritual things ambapo ndipo utaona na kumjua Mungu.
 
Lakini Mungu akaamua kuumba ulimwengu ambao mtu anaweza kwenda motoni.

Hakuuishia hapo,pia akaumba pepo ili watakao enda peponi waende,lakini akaumba na hiari ya kuamua kipi cha kufanya na kipi usifanye.

Lakini hakuacha hivyo hivyo,akatujalia akili,milango ya fahamu na mitume miongoni mwa wanadu watukumbushe juu ya kufanya mema.
Kwa nini kaamua kuumba ulimwengu ambao watu wengi sana wataenda motoni na hakuamua kuumba ulimwengu ambao hakuna mtu atakayeenda motoni?

Umejuaje kama watu wengi wataenda motoni ? Kwanini unafikiri kama upande mmoja tu ? Vipi angeumba wanawake tu au angefanya kuwe na mchana tu au angefanya kuwe na njaa tu ? Huoni ungekuja kuhoji kinyume chake ?

Sababbu binadamu ameumbwa na uhuru,hawezi kuacha choko choko,na watu mfano wako walianza tangu wewe hujulilani yaani haupo.

Kwa maana hiyo Mola wetu anaumba na kuweka sheria zilizo bora.
 
Ukishajua square root ya mbili ni ndogo kuliko mbili, jibu lolote lililo zaidi ya mbili utajua si la kweli, hata kama hujui square root ya mbili ni nini.

Hii kwanza si kweli. Sababu kabla ya yote lazima tujue ni upi msingi wa hiyo "Square root" je ni uhalisia au makubaliano ya wana mahesabu ?

Kama ni makubaliano ya wana mahesabu hap utakuwa una amini na wala huna yakini na uhalisia unaondoka. Kwa maana hiyo hata kama nikijua ya kuwa "Square root" ya mbili ni ndogo kuliko mbili huu si uhalisia sababu asili ya jibu hilo ni makubaliano ya wana mahesabu yaliyo jengeka katika misingi ya majaribio na kubahatisha.
Sasa dini inatuambia square root ya 2 ni 9 (contradiction). Tukiuliza imepatikanaje? Mbona hesabu zimeharibiwa hapa? Tunaambiwa akili ya Mungu huwezi kuijua wewe.

Nakuuliza swali,ili mfano wa "Square root" ya mbili kuwa ndogo kuliko mbili yenyewe ni uhalisia au makubaliano ya wana mahesabu ? Kama ni makubaliano vipi iwe hoja katika mambo ya uhalisia ?

Kwa maana hiyo mfano wa "Square root" ya 2 ni 9 ukaunasibisha na dini,huo mfano wako unakuwa batili,sababu umelinganisha vitu viwili vyenye dhati tofauti. La kwanza ni makubaliano ya wana mahesabu na la pili uhalisia.

Yaani ni sawa sawa na kuleta mfano wa mtoto wa kuasili kuwa ni wako wakati kiuhalisia si wako na nasaba inarudi kwa baba.

Kwahiyo ninacho kukumbusha ni kuwa hata kutoa mifano pia ni elimu,elimu ambayo nyinyi hamkupewa.
Ukiuliza, mnajuaje huyo Mungu yupo na si hadithi tu? Hakuna anayeweza kuthibitisha Mungu yupo.

Uwepo wa Mungu unajulikana kupitia akili,milango ya fahamu na ufunuo. Tatizo mlipewa mifumo ya kufikiri kitoto na walimu na mkakosa ala za kuuujua ukweli.

Kama wewe unakubali "Simu" yako unayoitumia haiwezi kujitengeneza bila shaka dunia yupo aliye itengeneza na kuiwekea taratibu ambazo zipo na tunaziona.

Ajabu wewe una amini Mungu hayupo kisa kuna "The Problems of evil", mpaka kesho hujawahi kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Naendelea .....
 
Dini ina contradictions zinazoonesha ina diverge kutoka ukweli. Sayansi, hata kama haina picha kamili ya ukweli leo, inaelekea kwenye direction ya ukweli na ina narrow down on that.

Ukiona dini ina "Contradictions" kwanza ituhumu akili yako au elimu yako kwa kuwa haijaweza kuidiriki maana ya aya au hadothi husika.

Lakini swali la msingi,unatumia nini kuujua ukweli ?

Mathalani wewe una amini vipi kama ni kweli Newton aliwahi kuishi duniani ?

Je hizo sehemu zenye tofauti ya gravity (Heavy Gravity na kinyume chake) ni zipi na je mmeshafika na kujua ukweli wa hilo ?

Sayansi ina tatizo moja kubwa sana,nalo ni tatizo la kutoa hitimisho,kama ni mfatiliaji wa mambo ya sayansi na kuyaelewa utaliona hili,na Sayansi haipo kwa ajili hakika ya mambo yalivyo.

Msingi wa dini(Hapa nakusudia Uislamu) ni Ukweli,ndio maana hukuti sheria za Mola wetu ni zenye kubadilika,msingi wa Sayansi ni nadharia,majaribio jambo ambalo linawafanya Wana Sayansi wawe waongo na kuwa mbali na ukweli,na ndio maana anae fanya marejeo kwenye Sayabsi huwa ana matatizo ya akiki na anakuwa hana msimamo wa kielimu,hapa kuna mifano mingi sana.

Naendelea ...
 
Tatizo la waumini wengi, hususan hawa wanaochangia humu, ni wanaonekana kama hawajui 'imani' ni nini katika muktadha wa dini.

Naomba utusaidie kwa heshima na taadhima ni nini Imani kwa muktadha wa Dini ?
Kwa sababu, kama wangekuwa wanajua 'imani' ni nini katika muktadha wa dini zao, sidhani kama hii mijadala ingekuwa inajirudia rudia hivi.

Hivi unafikiri Wakana Mungu wangekuwa wanatumia akili ipasavyo na si kwa upande mmoja,unafikiri hii mijadala ingekuwepo ?

Jibu ingekuwa haipo na hili huwa nalisema kila siku.
 
Kwangu mimi, uzuri wa sayansi si kwamba ina majibu yote, au inahodhi ukweli wote, au haiwezi kushindwa.

Niambie ukweli kuhusu KIFO kwa misingi ya Sayansi ?

Na ukweli kuhusu ROHO kwa mujibu wa Sayansi ?

Na uniambie UKWELI ni nini kwa mujibu wa Sayansi ?
 
Utakapokuja kuujua ukweli utaona ni kiasi gani hoja zako hizi za square root zilikua za kijinga.
Thibitisha hoja ni za kijinga.

Hoja hujaweza kuzijibu unaita za kijinga?

Thibitisha Mungu yupo.
 
Kwanza hujaelewa maana ya freewill....

Pili swala la kusema jua ni kubwa kuliko dunia hayo ni maelezo ya wanasayansi ambayo huwez mwelesha mtoto mdogo akakuelewa. ..but intuitively binadamu yeyote anaelewa ivo ..

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa kila mwanadamu ... Ndio maana kuna myriad of things almost everything science can't create from the scratch...

.hata jinsi unavopumua wewe huoni kama ni muujiza huo??.

Hewa haionekan ila iko kila sehemu ww unaona ni kawaida???.. Unaweza tengeza oxygen from the scratch??..

ni kiburi tu watu hujipa..

Yaan kama ungeweza kwanza kutolea maelezo vitu vinavyoonekana kama ivo ...ingekua vizur sana kabla ya kuanza kujadili yeye aliyeviumba...

Pia kumbuka wewe una brain .mind ..logic etc.... Unawaza na kufikiri kupitia ivo... Je utaweza kuwaza aliyeiumba iyo akili yenyewe??

Last question tell me who in this world can create something from nothing????????

Mbona uwepo wa Mungu uko wAzi sana jamani...

Jina lake lihimidiwe...ONE GOD..

Wewe ulipewa free will ya kuchagua uzaliwe wapi,mwenye jinsia gani,na wazazi gani,wenye uwezo gani kimaisha,wenye magonjwa ya kurithi au laa,wakati gani na uwe na kipaji kipi?

Watu wanaozaliwa vilema nao walipewa free will na Mungu ya kuzaliwa na ulemavu huo ama walilazimishwa wawe hivyo kabla hata ya kuzaliwa?.

Unafikiri wanaozaliwa vipofu,viwete,viziwi wenye mitindio ya ubongo na waliopungukiwa viungo vya mwili huku wengi wao wakija kuishi maisha ya tabu, wangekuwa na free will wangechagua kuzaliwa hivyo?

Kama kweli free will ipo kwa nini tunatishiana mamoto na kuzamishana kwenye magharika ya Nuhu?

Kwa nini hiyo free will iwe ktk mema na mabaya tu na si kwenye kuchagua nizaliwe wapi na bila magonjwa ya kurithi kama ualbino,sickle cell,night blindness na ma kansa ambacho ndicho kitu cha muhimu zaidi?

Unaelewa hata maana halisi ya free will wewe?

Kwa nini hakuumba dunia ambayo mlevi atamtii automatic na hasa kwa kuwa uwezo huo anao badala ya kusubiri huruma za mlevi?

Kwani angepungukiwa nini kwa kufanya hivyo?

The same question apply to you,

Kwa nini watoto wadogo wengi kabla ya kuelimishwa wanafikiri jua ni dogo kiukubwa kulinganisha na dunia na si dunia kuwa ndogo kulinganisha na jua?

Ni nadharia gani hii yenye nguvu hivi kiasi cha kuwaaminishà watoto kwamba dunia ni kubwa kuliko jua?

Kupitia fikira hizo za kitoto ndivyo ukweli ulivyo kuhusu ukubwa wa jua na dunia?

Can you prove that The God exist real, and not just the products of your imagination only!?
 
Hii kwanza si kweli. Sababu kabla ya yote lazima tujue ni upi msingi wa hiyo "Square root" je ni uhalisia au makubaliano ya wana mahesabu ?

Kama ni makubaliano ya wana mahesabu hap utakuwa una amini na wala huna yakini na uhalisia unaondoka. Kwa maana hiyo hata kama nikijua ya kuwa "Square root" ya mbili ni ndogo kuliko mbili huu si uhalisia sababu asili ya jibu hilo ni makubaliano ya wana mahesabu yaliyo jengeka katika misingi ya majaribio na kubahatisha.

Nakuuliza swali,ili mfano wa "Square root" ya mbili kuwa ndogo kuliko mbili yenyewe ni uhalisia au makubaliano ya wana mahesabu ? Kama ni makubaliano vipi iwe hoja katika mambo ya uhalisia ?

Kwa maana hiyo mfano wa "Square root" ya 2 ni 9 ukaunasibisha na dini,huo mfano wako unakuwa batili,sababu umelinganisha vitu viwili vyenye dhati tofauti. La kwanza ni makubaliano ya wana mahesabu na la pili uhalisia.

Yaani ni sawa sawa na kuleta mfano wa mtoto wa kuasili kuwa ni wako wakati kiuhalisia si wako na nasaba inarudi kwa baba.

Kwahiyo ninacho kukumbusha ni kuwa hata kutoa mifano pia ni elimu,elimu ambayo nyinyi hamkupewa.

Uwepo wa Mungu unajulikana kupitia akili,milango ya fahamu na ufunuo. Tatizo mlipewa mifumo ya kufikiri kitoto na walimu na mkakosa ala za kuuujua ukweli.

Kama wewe unakubali "Simu" yako unayoitumia haiwezi kujitengeneza bila shaka dunia yupo aliye itengeneza na kuiwekea taratibu ambazo zipo na tunaziona.

Ajabu wewe una amini Mungu hayupo kisa kuna "The Problems of evil", mpaka kesho hujawahi kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Naendelea .....

Bro Zurri ndio maana nimesema hapo juu kwamba Kiranga akija kuujua ukweli ataona mambo na hoja zake za square root ni za kijinga mno. Eti square root haiwezi kuwa ndogo, sasa mbona square root ya nusu ni robo? Hoja zingine bana za ajabu kweli
 
Kwanza hujaelewa maana ya freewill....

Pili swala la kusema jua ni kubwa kuliko dunia hayo ni maelezo ya wanasayansi ambayo huwez mwelesha mtoto mdogo akakuelewa. ..but intuitively binadamu yeyote anaelewa ivo ..

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa kila mwanadamu ... Ndio maana kuna myriad of things almost everything science can't create from the scratch...

.hata jinsi unavopumua wewe huoni kama ni muujiza huo??.

Hewa haionekan ila iko kila sehemu ww unaona ni kawaida???.. Unaweza tengeza oxygen from the scratch??..

ni kiburi tu watu hujipa..

Yaan kama ungeweza kwanza kutolea maelezo vitu vinavyoonekana kama ivo ...ingekua vizur sana kabla ya kuanza kujadili yeye aliyeviumba...

Pia kumbuka wewe una brain .mind ..logic etc.... Unawaza na kufikiri kupitia ivo... Je utaweza kuwaza aliyeiumba iyo akili yenyewe??

Last question tell me who in this world can create something from nothing????????

Mbona uwepo wa Mungu uko wAzi sana jamani...

Jina lake lihimidiwe...ONE GOD..

MPUMBAVU asema moyoni mwake HAKUNA MUNGU..... Zaburi 14:1
 
Kwanza hujaelewa maana ya freewill....
Mimi kutoelewa maana ya freewill ni ushahidi mwingine wa kutokuwepo Mungu muweza yote na mwenye upendo mkuu.

Angekuwepo asingekuwa na upendeleo wa kiwango hiki kiasi cha wewe kukufanya ujue maana ya freewill huku mimi nikishindwa.

Lakini pia ningekuona wa maana sana iwapo ungeeleza freewill ni nini baada ya kubaini kwamba mimi siielewi.

Pili swala la kusema jua ni kubwa kuliko dunia hayo ni maelezo ya wanasayansi ambayo huwez mwelesha mtoto mdogo akakuelewa. ..
Ulishajaribu kumuelewesha mtoto yeyote kwa maelezo yenye logic akashindwa kukuelewa?

Kwa nini una generalize kuwa maelezo ya sayansi ni magumu kuwaelewesha watoto wakati hata kuhesabu 1,2,3.. ni sayansi ya namba na kindergarten wengi wanaimbishwa na kujua vyema kuhesabu?

After all mimi sikusema suala la jua kuwa kubwa zaidi ya dunia ni gumu kuelezeka,

Niliuliza kwa nini mtoto kabla ya kuelimishwa huwa anadhani jua ni dogo kuliko dunia?

but intuitively binadamu yeyote anaelewa ivo ..
Kuhusu nini?

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa kila mwanadamu...
Una uhakika ama unaropoka tu?.

Mbona mimi ni mwanadamu na uwepo wa huyo Mungu wenu haujajidhihirisha?

Ndio maana kuna myriad of things almost everything science can't create from the scratch...
Logical non sequitur!.

Unaelewa hicho ni kitu gani?

Hata kama sayansi haiumbi kitu kutoka kwenye nothing, huo si ushahidi wa kwamba muumbaji huyo ni Mungu.

Ni sawa na kusema Mzee Lomolomo wa kwenye riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie ndiye mzazi wako kisa tu sayansi haiwezi kuzaa mtu.

Ndicho unachokifanya hapa.

Unatumia udhàifu wà sayansi kutokuwa na uwezo wà kuzaa kulazimisha mzee Lomolomo kuwa ndiye mzazi wako.

Wakati mimi najua mzee huyo hayupo kwenye uhalisia nje ya masimulizi ya kinadharia, na hivyo hawezi kuwa ndiye baba yako.

Thibitisha kwanza Mzee Lomolomo yupo kiuhalisia, nje ya masimulizi ya kufikirika ya mwandishi Emmanuel Mbogo ndipo uje tuanze kutazama kama kweli ni yeye ndiye baba yako mzazi.

hata jinsi unavopumua wewe huoni kama ni muujiza huo??.
Kwa hiyo?

Hewa haionekan ila iko kila sehemu ww unaona ni kawaida???..
Kwangu mimi ni jambo la kawaida sana.

Unaweza tengeza oxygen from the scratch??..
Another logical non sequitur!.

Hata kama nisipoweza,hiyo haithibitishi kuwa anayetengeneza hiyo hewa ni Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na upendo wote,ambae alishathibitishwa na the problem of evil na proof by contradictions kuwa hayupo.

Inawezekana sana mtengenezaji huyo (iwapo kweli inatengenezwa) akawa ni mwingine tu ambae haujamjua bado.

Ndiyo maana nataka uthibitishe hapa kuwa muumbaji huyo ni Mungu na si mwingine yeyote.

ni kiburi tu watu hujipa..
Kwa nini Mungu aliumba Ulimwengu ambao mtu anaweza akajipa kiburi wakati angeamua kiburi kisiwepo na kikawa hakipo?

Yaan kama ungeweza kwanza kutolea maelezo vitu vinavyoonekana kama ivo ...ingekua vizur sana kabla ya kuanza kujadili yeye aliyeviumba...
Thibitisha iwapo kweli vitu hivyo viliumbwa!.

Mbona unalazimisha uumbaji pasina kutuambia kwanza yeye muumbaji kaumbwa na nani?

Pia kumbuka wewe una brain .mind ..logic etc.... Unawaza na kufikiri kupitia ivo... Je utaweza kuwaza aliyeiumba iyo akili yenyewe??
Hata nikikwambia sijui, muumbaji huyo si lazima awe ni Mungu mnayemtaja taja sana huko makanisani na misikitini.

Unaweza niuliza jina la mchina aliyejenga uwanja wa taifa mwaka 2005 nikakujibu sijui.

Ila ukiniambia mchina huyo ni Bruce Lee,(ninayejua alifariki mwaka 1963), nitakukatalia jibu lako.

Kwa hiyo mimi kutokujua jibu sahihi si tiketi ya wewe kulazimisha nikubali jibu lako,ambalo kwanza naona ni la uongo.

Last question tell me who in this world can create something from nothing????????
I do no,can you tell me who is he or she?

Mbona uwepo wa Mungu uko wAzi sana jamani...
Sasa kipi kinachokushinda kuthibitisha huo uwepo wake?

Jina lake lihimidiwe...ONE GOD..
Kabla ya jina lake kuhimidiwa, thibitisha kwanza uwepo wàke!.
 
when you are broke there are topics you should only listen to. So guys keep debating, am here listening, won't say a word.

This thread was doing good until I saw your contributions 🤣🤣🤣🤣, Nigger Go get some greens..cause you have them greens you become happy, confident, and all that..Money Starts first...PERIOOOOOD!!!!
 
I went through alot of comments on this thread and i noticed few things:

1. White people are the Evil one, they did alot of brainwashing when they came to colonize us.

2. Alot of people think dying is a punish while its not and dying is a must, this must be confused with the grief that somebody leaves after he/she is gone...NOW The one punished is the One who is still alive once your dead you dont feel a damn thing..

3. We were all born with Goos sense of humor, NATIVELY knowing BAD and GOOD, example No one has ever told you its bad to foulmouth you moma, you natively know that if you do that its NOT OKAY, unless otherwise your on serious NARCOTIC..

4 AND LAST, If you want to be good at stuffs, you must read alot, it is very akward that people come here and deliver stuffs they were told by their uncles and aunties, Like someone said UTAKUFA VIBAYA kisa jamaa kasema hana uhakika kama MUNGU YUPO? nigger how do you know ? If God is there and he is all that people SAY, then God doesnt do revenge...We all know that God knows everything, so HE problably knew some day you are going to put Mockery on HIM so He got prepared and He probably has forgiven you, because if he wanted he would have stopped you from doing every evil that you have been doing....

NB: Get a chill pill playa, Do something constructive, Becuse thats what God want us to do and so on....#micdrops
 
Ebu nikurahisishie kazi..sema unataka ushahidi wa aina...wa picha ,video ,document au live na macho au aina gan??..sema nikujibu
Mimi kutoelewa maana ya freewill ni ushahidi mwingine wa kutokuwepo Mungu muweza yote na mwenye upendo mkuu.

Angekuwepo asingekuwa na upendeleo wa kiwango hiki kiasi cha wewe kukufanya ujue maana ya freewill huku mimi nikishindwa.

Lakini pia ningekuona wa maana sana iwapo ungeeleza freewill ni nini baada ya kubaini kwamba mimi siielewi.

Ulishajaribu kumuelewesha mtoto yeyote kwa maelezo yenye logic akashindwa kukuelewa?

Kwa nini una generalize kuwa maelezo ya sayansi ni magumu kuwaelewesha watoto wakati hata kuhesabu 1,2,3.. ni sayansi ya namba na kindergarten wengi wanaimbishwa na kujua vyema kuhesabu?

After all mimi sikusema suala la jua kuwa kubwa zaidi ya dunia ni gumu kuelezeka,

Niliuliza kwa nini mtoto kabla ya kuelimishwa huwa anadhani jua ni dogo kuliko dunia?

Kuhusu nini?

Una uhakika ama unaropoka tu?.

Mbona mimi ni mwanadamu na uwepo wa huyo Mungu wenu haujajidhihirisha?

Logical non sequitur!.

Unaelewa hicho ni kitu gani?

Hata kama sayansi haiumbi kitu kutoka kwenye nothing, huo si ushahidi wa kwamba muumbaji huyo ni Mungu.

Ni sawa na kusema Mzee Lomolomo wa kwenye riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie ndiye mzazi wako kisa tu sayansi haiwezi kuzaa mtu.

Ndicho unachokifanya hapa.

Unatumia udhàifu wà sayansi kutokuwa na uwezo wà kuzaa kulazimisha mzee Lomolomo kuwa ndiye mzazi wako.

Wakati mimi najua mzee huyo hayupo kwenye uhalisia nje ya masimulizi ya kinadharia, na hivyo hawezi kuwa ndiye baba yako.

Thibitisha kwanza Mzee Lomolomo yupo kiuhalisia, nje ya masimulizi ya kufikirika ya mwandishi Emmanuel Mbogo ndipo uje tuanze kutazama kama kweli ni yeye ndiye baba yako mzazi.

Kwa hiyo?

Kwangu mimi ni jambo la kawaida sana.

Another logical non sequitur!.

Hata kama nisipoweza,hiyo haithibitishi kuwa anayetengeneza hiyo hewa ni Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na upendo wote,ambae alishathibitishwa na the problem of evil na proof by contradictions kuwa hayupo.

Inawezekana sana mtengenezaji huyo (iwapo kweli inatengenezwa) akawa ni mwingine tu ambae haujamjua bado.

Ndiyo maana nataka uthibitishe hapa kuwa muumbaji huyo ni Mungu na si mwingine yeyote.

Kwa nini Mungu aliumba Ulimwengu ambao mtu anaweza akajipa kiburi wakati angeamua kiburi kisiwepo na kikawa hakipo?

Thibitisha iwapo kweli vitu hivyo viliumbwa!.

Mbona unalazimisha uumbaji pasina kutuambia kwanza yeye muumbaji kaumbwa na nani?

Hata nikikwambia sijui, muumbaji huyo si lazima awe ni Mungu mnayemtaja taja sana huko makanisani na misikitini.

Unaweza niuliza jina la mchina aliyejenga uwanja wa taifa mwaka 2005 nikakujibu sijui.

Ila ukiniambia mchina huyo ni Bruce Lee,(ninayejua alifariki mwaka 1963), nitakukatalia jibu lako.

Kwa hiyo mimi kutokujua jibu sahihi si tiketi ya wewe kulazimisha nikubali jibu lako,ambalo kwanza naona ni la uongo.

I do no,can you tell me who is he or she?

Sasa kipi kinachokushinda kuthibitisha huo uwepo wake?

Kabla ya jina lake kuhimidiwa, thibitisha kwanza uwepo wàke!.
 
Bro Zurri ndio maana nimesema hapo juu kwamba Kiranga akija kuujua ukweli ataona mambo na hoja zake za square root ni za kijinga mno. Eti square root haiwezi kuwa ndogo, sasa mbona square root ya nusu ni robo? Hoja zingine bana za ajabu kweli
Unajuaje huu ni ukweli? Unajuaje huu ni uongo?

Nimeongelea square root ya specific namba, umekwepa kuitaja hiyo namba specifically, umechagua yako nyingine ambayo sijaitaja.

Square root ya mbili inaweza kuwa kubwa kuliko mbili?
 
Hahahhhahhs. Hapa ndio huwa tunaibuka kidedea kua Mungu ni mmoja...namuuliza unataka ushahid gan ili uamini... ET WEKA WOWOTE HII INAONYESHA UKUU WA MUNGU YAAN AKILI ZAKO HAZIWEZI KUCHUNGUZA UWEZO WA MUUMBAJI..HII NDIO MAANA HALIS YA MUUMBA....SIKU NJEMA
Weka ushahidi wowote ule unaojua wewe.
 
Back
Top Bottom