Kwanza hujaelewa maana ya freewill....
Mimi kutoelewa maana ya freewill ni ushahidi mwingine wa kutokuwepo Mungu muweza yote na mwenye upendo mkuu.
Angekuwepo asingekuwa na upendeleo wa kiwango hiki kiasi cha wewe kukufanya ujue maana ya freewill huku mimi nikishindwa.
Lakini pia ningekuona wa maana sana iwapo ungeeleza freewill ni nini baada ya kubaini kwamba mimi siielewi.
Pili swala la kusema jua ni kubwa kuliko dunia hayo ni maelezo ya wanasayansi ambayo huwez mwelesha mtoto mdogo akakuelewa. ..
Ulishajaribu kumuelewesha mtoto yeyote kwa maelezo yenye logic akashindwa kukuelewa?
Kwa nini una generalize kuwa maelezo ya sayansi ni magumu kuwaelewesha watoto wakati hata kuhesabu 1,2,3.. ni sayansi ya namba na kindergarten wengi wanaimbishwa na kujua vyema kuhesabu?
After all mimi sikusema suala la jua kuwa kubwa zaidi ya dunia ni gumu kuelezeka,
Niliuliza kwa nini mtoto kabla ya kuelimishwa huwa anadhani jua ni dogo kuliko dunia?
but intuitively binadamu yeyote anaelewa ivo ..
Kuhusu nini?
Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa kila mwanadamu...
Una uhakika ama unaropoka tu?.
Mbona mimi ni mwanadamu na uwepo wa huyo Mungu wenu haujajidhihirisha?
Ndio maana kuna myriad of things almost everything science can't create from the scratch...
Logical non sequitur!.
Unaelewa hicho ni kitu gani?
Hata kama sayansi haiumbi kitu kutoka kwenye nothing, huo si ushahidi wa kwamba muumbaji huyo ni Mungu.
Ni sawa na kusema Mzee Lomolomo wa kwenye riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie ndiye mzazi wako kisa tu sayansi haiwezi kuzaa mtu.
Ndicho unachokifanya hapa.
Unatumia udhàifu wà sayansi kutokuwa na uwezo wà kuzaa kulazimisha mzee Lomolomo kuwa ndiye mzazi wako.
Wakati mimi najua mzee huyo hayupo kwenye uhalisia nje ya masimulizi ya kinadharia, na hivyo hawezi kuwa ndiye baba yako.
Thibitisha kwanza Mzee Lomolomo yupo kiuhalisia, nje ya masimulizi ya kufikirika ya mwandishi Emmanuel Mbogo ndipo uje tuanze kutazama kama kweli ni yeye ndiye baba yako mzazi.
hata jinsi unavopumua wewe huoni kama ni muujiza huo??.
Kwa hiyo?
Hewa haionekan ila iko kila sehemu ww unaona ni kawaida???..
Kwangu mimi ni jambo la kawaida sana.
Unaweza tengeza oxygen from the scratch??..
Another logical non sequitur!.
Hata kama nisipoweza,hiyo haithibitishi kuwa anayetengeneza hiyo hewa ni Mungu muweza yote,mjuzi wa yote na upendo wote,ambae alishathibitishwa na the problem of evil na proof by contradictions kuwa hayupo.
Inawezekana sana mtengenezaji huyo (iwapo kweli inatengenezwa) akawa ni mwingine tu ambae haujamjua bado.
Ndiyo maana nataka uthibitishe hapa kuwa muumbaji huyo ni Mungu na si mwingine yeyote.
ni kiburi tu watu hujipa..
Kwa nini Mungu aliumba Ulimwengu ambao mtu anaweza akajipa kiburi wakati angeamua kiburi kisiwepo na kikawa hakipo?
Yaan kama ungeweza kwanza kutolea maelezo vitu vinavyoonekana kama ivo ...ingekua vizur sana kabla ya kuanza kujadili yeye aliyeviumba...
Thibitisha iwapo kweli vitu hivyo viliumbwa!.
Mbona unalazimisha uumbaji pasina kutuambia kwanza yeye muumbaji kaumbwa na nani?
Pia kumbuka wewe una brain .mind ..logic etc.... Unawaza na kufikiri kupitia ivo... Je utaweza kuwaza aliyeiumba iyo akili yenyewe??
Hata nikikwambia sijui, muumbaji huyo si lazima awe ni Mungu mnayemtaja taja sana huko makanisani na misikitini.
Unaweza niuliza jina la mchina aliyejenga uwanja wa taifa mwaka 2005 nikakujibu sijui.
Ila ukiniambia mchina huyo ni Bruce Lee,(ninayejua alifariki mwaka 1963), nitakukatalia jibu lako.
Kwa hiyo mimi kutokujua jibu sahihi si tiketi ya wewe kulazimisha nikubali jibu lako,ambalo kwanza naona ni la uongo.
Last question tell me who in this world can create something from nothing????????
I do no,can you tell me who is he or she?
Mbona uwepo wa Mungu uko wAzi sana jamani...
Sasa kipi kinachokushinda kuthibitisha huo uwepo wake?
Jina lake lihimidiwe...ONE GOD..
Kabla ya jina lake kuhimidiwa, thibitisha kwanza uwepo wàke!.