[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] HON: CASTR I'm with you because I might add something to be a reason for me to be poor poor and poor.
These topics are for successful people.
I keep my words with my broke black *ss
Kuna rais mmoja wa Marekani wa mwanzo kabisa, nafikiri alikuwa John Aadams yule, alisema wao wanayafanyia kazi masuala ya msingi kabisa yasiyokwepeka katika maisha ya kila siku (kula, pahala pa kuishi, afya, mambo ya kimsingi ya kiuchumi kama ajira etc) ili watoto wao wawe na luxury ya kuweza kuchambua masuala mengine (kama haya ya uwepo wa Mungu).
Tatizo kwetu huko wengi hawajatatua matatizo ya msingi, sasa kujadiliana na mtu ambaye hajapata muda wa kumsoma Anselm, Augustine, Russell, Dawkins, Hitchens, kwa sababu hata bajeti ya vitabu hana, au Kiingereza hajui kwa sababu hakufanikiwa kupata nafasi ya kujifunza, ni tabu sana.
Ndiyo maana nafikia nafasi hata kuonesha areguments za kutokuwepo kwa Mungu zinazotolewa na watu wanaosema Mungu yupo.
Hawana uwezo wa kufikiri kwa kina, muda wao mwingi unatumiwa kufukuza riziki ya siku.
Mtu anakwambia complexity ya dunia na viumbe ni lazima iwe imeumbwa, haiwezi kuwa imetokea yenyewe tu.
Hajui kwamba, kwa kusema hilo, anachosema kiukweli kabisa, ni kwamba Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.
Kwa sababu, kama complexity ni lazima iumbwe, haiwezi kutokea tu, hata Mungu naye ni complex, naye atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad nauseam.
Kwa hiyo, hapo hakuna Mungu muumba yote, kuna an infinity of viumbe.
Kwa hiyo Mungu hayupo.
Yani mtu anafikiri ananipinga mimi, kumbe anajipinga mwenyewe.
Kwa nini? Kwa sababu hajapata nafasi ya kuchunguza hoja yake kwa umakini kabla ya kuitoa, amejikita kwenye kufukuza riziki.