Stephen Masele: Kusimamia haki si utovu wa nidhamu

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amesema kusimamia misingi ya haki za binadamu asitafsiriwe kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Alisema hayo jana baada ya kutoka katika mahojiano na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu.

Masele ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa Bunge la Afrika (PAP) alihojiwa kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 5.34 asubuhi hadi saa 9.18 alasiri na kamati hiyo inayongozwa na mwenyekiti wake, Emmanuel Mwakasaka.

Baada ya mahojiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la utawala bungeni, Masele alisema anaamini kamati itamtendea haki huku Mwenyekiti Mwakasaka akisema baada ya kumaliza kumhoji na kupitia mahojiano hayo Watanzania watajuzwa.

Kamati hiyo ilimhoji Masele ikitekeleza agizo la Spika Job Ndugai alilolitoa Mei 16 alipolitangazia Bunge akimtuhumu mbunge huyo kwa utovu wa nidhamu na kumtaka kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiendelea na vikao vya PAP.

Chanzo: Mwananchi
 
Anaetakiwa kufikishwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu ni Ndugai kwa makosa yafuatayo;
  1. Kuonyesha dharau kwa Bunge la Afrika (PAP), kikao halali cha African Union (AU)
  2. Kutumia lugha ya kashfa, yenye kuhukumu na kudhalilisha kwa viongozi wa kitaifa (CAG - kufikishwa kwa pingu; Masele - kufanya mambo ya ovyo ovyo)
  3. Kudharau (undermine) ofisi ya raisi wa Tanzania (kuvunja mkataba wa Bandari Bagamoyo ni sawa na kuweka mkokoteni usukume ng'ombe, afadhali tungeacha SGR)
  4. Nk
 
Baada ya mahojiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la utawala bungeni, Masele alisema anaamini kamati itamtendea l

Kila mtu mwenye akili timamu anastahili kumpongeza na kujivunia hatua na msimamo wa Maselle kwenye sakata la PAP, he made us proud kwa kusimamia Nidhamu, haki za binadamu, utu na heshima ya mwanamke. Big up Maselle
 
Ndugai alitaka kuficha sababu ya kumuita masele.huyu mzee duh
 
Hapo bado maamuzi ya AU? Mbona naona kuna kauonevu? Demu wake aliwe nayeye apugwe kweli?
 
Hivi wapiga kura wake wameshindwa kuandamana kumtetea mbunge wao?
 
Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amesema kusimamia misingi ya haki za binadamu asitafsiriwe kuwa ni mtovu wa nidhamu.

Alisema hayo jana baada ya kutoka katika mahojiano na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu tuhuma za utovu wa nidhamu.

Masele ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa Bunge la Afrika (PAP) alihojiwa kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 5.34 asubuhi hadi saa 9.18 alasiri na kamati hiyo inayongozwa na mwenyekiti wake, Emmanuel Mwakasaka.

Baada ya mahojiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la utawala bungeni, Masele alisema anaamini kamati itamtendea haki huku Mwenyekiti Mwakasaka akisema baada ya kumaliza kumhoji na kupitia mahojiano hayo Watanzania watajuzwa.

Kamati hiyo ilimhoji Masele ikitekeleza agizo la Spika Job Ndugai alilolitoa Mei 16 alipolitangazia Bunge akimtuhumu mbunge huyo kwa utovu wa nidhamu na kumtaka kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akiendelea na vikao vya PAP.

Chanzo: Mwananchi
Kiukweli huyu ni mbunge shujaa sana, niliwahi kushauri siku nyingi nyuma, atamkwe ni shujaa wa taifa, sijui kwa nini hajatamkwa.
P.
 
Hii Kamati inaonekana ni chombo fulani cha kuficha udhaifu wa mtu fulani
Hii Kamati inaelekea kuwa ni Kamati ya Ndugai ....... kamati ya Bunge haiwezi kuwa hiyo!!

Kila anayepelekwa pale na Ndugai lazima akutwe na kosa ....... except Bashite peke yake!!
 
Ila kaka Paskali hawajamtolea azimio mpaka hii leo. Anabahati sana
 
Huyu Mwakasaka amekuwa kibaraka wa Ndugai as if yeye sio mbunge wa kuchaguliwa....ni kiongozi dhaifu,mnafiki,mzandiki na fala kuliko mwenyeviti wengine wote wa hii kamati kuwahi kutokea.
Anaitia aibu familia yake na wananchi waliomchagua.
Ni mbunge wa wapi niwape pole wananchi wake?
 
Anaetakiwa kufikishwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu ni Ndugai kwa makosa yafuatayo;
  1. Kuonyesha dharau kwa Bunge la Afrika (PAP), kikao halali cha African Union (AU)
  2. Kutumia lugha ya kashfa, yenye kuhukumu na kudhalilisha kwa viongozi wa kitaifa (CAG - kufikishwa kwa pingu; Masele - kufanya mambo ya ovyo ovyo)
  3. Kudharau (undermine) ofisi ya raisi wa Tanzania (kuvunja mkataba wa Bandari Bagamoyo ni sawa na kuweka mkokoteni usukume ng'ombe, afadhali tungeacha SGR)
  4. Nk
Kweli aisee!!
 
Character Assassination inayotumiwa kuwadhalilisha watu sio mtindo mzuri wa uongozi.Kila binadamu anapenda aheshimiwe hata kama yeye ni subordinate kwako mpe heshima yake
 
Yetu macho tu na masikio,ila viongozi wanaitaji kuwa na busara Sana,hata masele angeitwa kimya kimya kusingekuwepo na tabu ila kea ivi kill mtu katega sikio tujue mwisho wa picha
 
Back
Top Bottom