Pre GE2025 Stephen Wasira amjibu John Heche kuhusu umri wake kuwa mkubwa. Asema gari ni injini siyo bodi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Bara, Stephen Wasira, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kuhusu hoja ya umri wake, akisisitiza kuwa uwezo wa mtu hautokani na miaka aliyoishi bali akili alizonazo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Geita leo Januari 29, 2025, Wasira amesema umri wake hauathiri uwezo wake wa kufikiri wala kufanya maamuzi sahihi.

"Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi," alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.

Wasira ametoa mfano wa Donald Trump, ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa hivi karibuni, akisema kuwa licha ya umri wake mkubwa, Wamarekani walimchagua kwa sababu ya sera zake na si kwa kuangalia umri wake.

"Heche akitaka ushahidi aende Marekani akawaulize Wamarekani kwanini walimchagua Donald Trump mwenye umri kama wangu na wakamuacha Kamala Harris mwenye miaka 60," alisisitiza Wasira.

Kauli hiyo imekuja muda mchache baada ya John Heche, akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya CHADEMA, kudai kuwa Wasira amekaa serikalini kwa muda mrefu na hawezi kuleta mawazo mapya kwa kizazi cha sasa chenye changamoto za ajira.

"Nimemuona Mzee Wasira amekuwa serikalini tangu akiwa na miaka 20, mimi sijazaliwa… Wasira hawezi kuja na mawazo mapya kwa watu wamemaliza vyuo vikuu na hawana ajira," alisema Heche.

Chanzo cha maandishi haya au andiko hili ni kutoka Jambo Tv Online. Mimi Mwashambwa Sijaweka neno langu hata moja.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mzee atadhalilika sana kujibizana na timu ya kina Heche,aendelee tu ataipata fresh
 
Uyo mzee wenu mwambieni ,lissu na heche sio size yake
 
Huu umri wa Wasira unaotajwa siamini kama ni sahihi. Namfahamu tangu kipindi hajapelekwa kufanya kazi ubalozini Washington.

Umri wake hauwezi kupungua miaka 85.
Wenda alifoji cheti cha kuzaliwa ,wazee wa umri huu ,enzi zile hata utaratibu wa vyeti vya kuzaliwa haukua sawa
 
Hiyo TZA 112 ishajichokea....badala icheze na vitukuu inahangaika na kina Heche.

Kazi na umri we mzee.
 
Eti anajilinganisha na Trump wazee wa hovyo ni wengi tz na ndo wanafanya vijana wasitimize malengo yao too much old school kuna mzee mmoja alishastaafu kazi karibu miaka 7 huko ila bado anangangania kubaki kwa position anamwambia CEO yaan Department yote ni vijana wataharibu kazi tulitoa show moja hadi mwenyewe akanyoosha mikono maana production ilipanda 3 times tangu kampuni iwepo nchini na tukavuka malengo.

Wito wangu wazee hawa wanaitaji kupumzika na kulea wajukuu ikiitajika watamuomba ushauri ingekuwa uchaguzi ni wa huru na haki tungekuwa tunaongea mengine hapa tz
 
Kwenye hii hoja, Heche amechemka vibaya sana. Heche ni Jamii ya vijana walio tayari kuua wazazi wao kisa wana umri mkubwa!
 
Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55.
Hata miaka 55 ni umri mkubwa, mbona ameitaja kama ni miaka michache... ukiwa na hiyo miaka unatakiwa uwe umeshaanza kuwaza maisha baada ya kustaafu 🐼
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…