Pre GE2025 Stephen Wasira amjibu John Heche kuhusu umri wake kuwa mkubwa. Asema gari ni injini siyo bodi

Pre GE2025 Stephen Wasira amjibu John Heche kuhusu umri wake kuwa mkubwa. Asema gari ni injini siyo bodi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii hukuona kama ni hoja ya Msingi ya Heche kwamba nchini humu Kuna changamoto kubwa sana ya Ajira, Kiasi kwamba hata vyuo vikuu sasa hivi wanafunzi hawajiandai kuwa watumishi Bora wa taifa hili Bali wananjiandaa kuwa machawa wa viongozi wa chama Cha Mapinduzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Ajira na fursa za kujiajiri hakuna, Kwa sababu serikali imeshindwa kuwaza namna Gani itapanua wigo wa Ajira Kwa kuwezesha sekta binafsi na sekta ya kilimo kuaccomodate graduate ambao wanamwagika kwenye labour market Kila siku?
Mbona wewe ni bumunda kubwa sana
Mimi siyo Bumunda😀
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) Bara, Stephen Wasira, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz Bara, @HecheJohn, kuhusu hoja ya umri wake, akisisitiza kuwa uwezo wa mtu hautokani na miaka aliyoishi bali akili alizonazo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Geita leo Januari 29, 2025, Wasira amesema umri wake hauathiri uwezo wake wa kufikiri wala kufanya maamuzi sahihi.

"Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi," alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.

Wasira ametoa mfano wa @realDonaldTrump, ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa hivi karibuni, akisema kuwa licha ya umri wake mkubwa, Wamarekani walimchagua kwa sababu ya sera zake na si kwa kuangalia umri wake.

"Heche akitaka ushahidi aende Marekani akawaulize Wamarekani kwanini walimchagua Donald Trump mwenye umri kama wangu na wakamuacha Kamala Harris mwenye miaka 60," alisisitiza Wasira.

Kauli hiyo imekuja muda mchache baada ya John Heche, akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya CHADEMA, kudai kuwa Wasira amekaa serikalini kwa muda mrefu na hawezi kuleta mawazo mapya kwa kizazi cha sasa chenye changamoto za ajira.

"Nimemuona Mzee Wasira amekuwa serikalini tangu akiwa na miaka 20, mimi sijazaliwa… Wasira hawezi kuja na mawazo mapya kwa watu wamemaliza vyuo vikuu na hawana ajira," alisema Heche.

Chanzo cha maandishi haya au andiko hili ni kutoka Jambo Tv Online. Mimi Mwashambwa Sijaweka neno langu hata moja.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
mwambie babu wasira injini zina saizi nafkiri yeye saizi ya mwisho
 
Back
Top Bottom