Pre GE2025 Stephen Wasira amjibu John Heche kuhusu umri wake kuwa mkubwa. Asema gari ni injini siyo bodi

Pre GE2025 Stephen Wasira amjibu John Heche kuhusu umri wake kuwa mkubwa. Asema gari ni injini siyo bodi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata miaka 55 ni umri mkubwa, mbona ameitaja kama ni miaka michache... ukiwa na hiyo miaka unatakiwa uwe umeshaanza kuwaza maisha baada ya kustaafu 🐼
Mzee Wasira yupo vyema sana kiakili na kimwili.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) Bara, Stephen Wasira, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTz Bara, @HecheJohn, kuhusu hoja ya umri wake, akisisitiza kuwa uwezo wa mtu hautokani na miaka aliyoishi bali akili alizonazo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Geita leo Januari 29, 2025, Wasira amesema umri wake hauathiri uwezo wake wa kufikiri wala kufanya maamuzi sahihi.

"Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi," alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.

Wasira ametoa mfano wa @realDonaldTrump, ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani katika uchaguzi wa hivi karibuni, akisema kuwa licha ya umri wake mkubwa, Wamarekani walimchagua kwa sababu ya sera zake na si kwa kuangalia umri wake.

"Heche akitaka ushahidi aende Marekani akawaulize Wamarekani kwanini walimchagua Donald Trump mwenye umri kama wangu na wakamuacha Kamala Harris mwenye miaka 60," alisisitiza Wasira.

Kauli hiyo imekuja muda mchache baada ya John Heche, akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya CHADEMA, kudai kuwa Wasira amekaa serikalini kwa muda mrefu na hawezi kuleta mawazo mapya kwa kizazi cha sasa chenye changamoto za ajira.

"Nimemuona Mzee Wasira amekuwa serikalini tangu akiwa na miaka 20, mimi sijazaliwa… Wasira hawezi kuja na mawazo mapya kwa watu wamemaliza vyuo vikuu na hawana ajira," alisema Heche.

Chanzo cha maandishi haya au andiko hili ni kutoka Jambo Tv Online. Mimi Mwashambwa Sijaweka neno langu hata moja.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

..Mzee Wassira badala ya kueneza sera za chama, na kuelezea mema yaliyofanywa na serikali ya CCM, anatumia mwingi kujitetea kuhusu umri wake.
 
Machawa badala ya kumshauri asijibizane na kina Heche, wao wanachochea
Machawa hawanaga akili, mkuu, uyu mzee anakuja fanya jambo ambalo ninaweza peleka nchi kubaya , maana anajua hana cha kupoteza, tutabaki kwenye sintofaham , tunzeni hii, sasa ameanza ita watu vibaka.

Akijibiwa bibaka ndani ya inchi hii ni akina nani atajibu nini sasa
 
We mzee, hebu tuheshimiane bana😅😅

Kunifananisha na huyo ajuza unanivunjia haki zangu
Mzee anasema yeye ni injini. Huyu Mzee kachoka, Gari yenye injini na haina matairi itaenda wapi? Itaishia kupiga makelele hapo hapo ilipo. Bora Gari yenye matairi bila injini, unaweza kuivuta toka Mwanza hadi Dar na ikafika
 
,lissu na heche
HAWA SI NI WAROPOKAJI TU... WANA NINI CHA ZAIDI YA UROPOKAJI

Nini maana ya kuropoka?
kuongea, kuandika au kupiga kelele kwa sauti kubwa, isiyodhibitiwa, au kwa njia ya hasira, mara kwa mara kusema mambo ya kuchanganyikiwa au ya kipuuzi
 
Mzee anasema yeye ni injini. Huyu Mzee kachoka, Gari yenye injini na haina matairi itaenda wapi? Itaishia kupiga makelele hapo hapo ilipo. Bora Gari yenye matairi bila injini, unaweza kuivuta toka Mwanza hadi Dar na ikafika
injini ya bito ya 1934 hako kazee wasira kamekongoroka idara zote
 
Wasira hakuna mtu hapo kuna galasa na mzimu kaja kuwaloga tu
 
HAWA SI NI WAROPOKAJI TU... WANA NINI CHA ZAIDI YA UROPOKAJI

Nini maana ya kuropoka?
kuongea, kuandika au kupiga kelele kwa sauti kubwa, isiyodhibitiwa, au kwa njia ya hasira, mara kwa mara kusema mambo ya kuchanganyikiwa au ya kipuuzi
Uropokaji anao kikongwe wasira yeye anajiongelea hovyo hovyo tu wakati mwingine hajui hata anasema nini, wewe chawa bila shaka ni mnufaika wa Tenda za ccm kwa sasa ndiyo maana umejitoa fahamu kutetea kikongwe kilichopwa kuwa kijijini kikilea vitukuu
 
Hako kazee kamewasusa vitukuu hakataki kukaa nyumbani kawalee kameamua kukalia siasa za maji taka watakapiga pressure hadi kazeeke zaidi na kuishia kujiuzulu mapema ccm wafanye uteuzi tena
 
Huyu mzee ana michepuko kila kona, afu eti anajiita msabato.
 
Mimi nina umri mkubwa lakini akili ni za miaka 55. Heche (John) akitaka akaulize madaktari wa India na Muhimbili, wamesema nina akili safi kabisa. Gari ni injini, siyo bodi," alisema Wasira huku akiwataka wapinzani wake kuzingatia hoja badala ya umri wake.
Niliona clip moja ya Dr.Janabi inasema stress zinapunguza kinga mwilini na hivyo huleta uwezekano wa kupata kansa.
sasa najiuliza uzee ukiongeza na stress zisizo za lazima nadhani matokeo ni mabaya. zaidi
 

Attachments

  • IMG-20250122-WA0047.jpg
    IMG-20250122-WA0047.jpg
    32.8 KB · Views: 2
Machawa hawanaga akili, mkuu, uyu mzee anakuja fanya jambo ambalo ninaweza peleka nchi kubaya , maana anajua hana cha kupoteza, tutabaki kwenye sintofaham , tunzeni hii, sasa ameanza ita watu vibaka.

Akijibiwa bibaka ndani ya inchi hii ni akina nani atajibu nini sasa
Hamna hoja yoyote Ninyi zaidi ya Uropokaji tu
 
Kauli hiyo imekuja muda mchache baada ya John Heche, akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya CHADEMA, kudai kuwa Wasira amekaa serikalini kwa muda mrefu na hawezi kuleta mawazo mapya kwa kizazi cha sasa chenye changamoto za ajira
Hii hukuona kama ni hoja ya Msingi ya Heche kwamba nchini humu Kuna changamoto kubwa sana ya Ajira, Kiasi kwamba hata vyuo vikuu sasa hivi wanafunzi hawajiandai kuwa watumishi Bora wa taifa hili Bali wananjiandaa kuwa machawa wa viongozi wa chama Cha Mapinduzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Ajira na fursa za kujiajiri hakuna, Kwa sababu serikali imeshindwa kuwaza namna Gani itapanua wigo wa Ajira Kwa kuwezesha sekta binafsi na sekta ya kilimo kuaccomodate graduate ambao wanamwagika kwenye labour market Kila siku?
Mbona wewe ni bumunda kubwa sana
 
Back
Top Bottom