carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amemtaja Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema kwamba amekuwa msema kweli, hivyo apongezwe badala ya kushambuliwa mitandaoni.
Wasira amesema hana ubaya na mtu ambaye ameamua kuwa mkweli kama Lema na hasa alipowataka wenzake kuachana na wanaharakati wa nje.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 3, 2026 wakati akifunga kampeni za uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Chamwino kwa upande wa CCM katika Kijiji cha Mnase ambako amemuombea kura mgombea wa chama hicho, Dk Netho Ndilito.
“Sina ugomvi na Lema, kwanza alikuwa mbunge mwenzangu, lakini jana aliamua kusema ukweli kwamba wanaharakati walisaidia uchaguzi wa Chadema mwaka jana, wakamtoa Mbowe na kumuingiza Lissu na Heche, sasa wameanza kuingia mambo mengine,” amesema Wasira.
Wasira amesema CCM haina ugomvi na Chadema ndiyo maana hakitaki kusuluhishwa na mtu wa nje na kwamba wenzao wanatoa masharti ya kutaka mazungumzo yamhusishe Lissu ambaye bado yupo kwenye mamlaka nyingine.
“Tunachotaka ni kushindana kwa hoja, siyo kueneza matusi ambayo hayajengi hata kidogo, twendeni kwa hoja ili tuwaambie ukweli wananchi kila chama kina malengo gani,” amesema Wasira.
Chanzo : Mwananchi