SI KWELI Wasira: Maridhiano ni lazima bila hivyo kuna watu watakaa jela milele

SI KWELI Wasira: Maridhiano ni lazima bila hivyo kuna watu watakaa jela milele

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

"Tunapozungumzia maridhiani tunamaanisha Makubaliano ya kitaifa, kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha siyo mtu mzuri kwetu na kwenye taifa ni hatari. Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"- Amesema Wasira

Wasira 2.jpg
Wasira 1.jpg


​
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii, imeibuka Taarifa inayoeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Stephen Wassira ameeleza kuwa maridhiano ni lazima la sivyo kuna watu wataozea jela.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao uebainisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika pia kilichpchapisha taarifa hiyo kumuhusu Stephen Wassira.

Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu umeonesha kuwa Taarifa hiyo imechapishwa na watu wengi Januari 30, 2026 ambapo wote wameandika ujumbe wa aina moja bila kutaja ni wapi na llini kiongozi huyo alitoa nukuu hiyo.

Aidha hakuna kumbukumbu zozote za hivi karibuni zikimuonesha Wassira akizungumza na waandishi wa habari ama kwenye mikutano ya hadhara siku ya Januari 30, 2026.

Katika vipindi tofauti Wasira amewahi kuzungumzia kuwa maridhiano ni jambo la lazima na kama mtu hatotaka basi hatolazimishwa lakini hakuwahi kueleza kuwa atakayekataa ataozea jela. Tazama hapa na hapa ambapo alieleza kuwa;

Sasa kama yupo mtu hataki mazungumzo, hataki amani, hataki maridhiano, hataki kusema na wenzake tutamuacha tu aongee na miti na majani baadae atakapochoka kuongea na miti na majani atakuja tutaongea lakini maridhiano ni jambo la lazima ukikataa unataka nini?
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

View attachment 3536710
Lisu ataishi kushuhudia Wasira akishushwa kaburini kabla yake. Niko pale naangali mchezo.
 
Maneno ya kifedhuli ya Wassira nimeyafurahia sababu amenisaidia kuwatia hasira watu.
Hawa CCM hawaambiliki hawasikii, hawabadiliki.
Wanataka watu waandamane tena kudai kesi ya Lissu itolewe hukumu au aachiwe huru haraka.
Safari hii maandamano yatakuwa makubwa sana ya kumtaka Lissu aachiwe huru.
Hawataamini.
Waache wajidanganye watu wanaogopa kuandamana tena.
 
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.
=============
MARIDHIANO NI LAZIMA BILA HIVYO KUNA WATU WATAKAA JELA MILELE: MZEE WASIRA
"Tunapo zungumzia maridhiano tunamaanisha makubaliano ya kitaifa kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha sio mtu mzuri kwetu na kwenye Taifa ni hatari.
Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"

View attachment 3536710
Kasema kweli chungu.
 
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

"Tunapozungumzia maridhiani tunamaanisha Makubaliano ya kitaifa, kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha siyo mtu mzuri kwetu na kwenye taifa ni hatari. Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"- Amesema Wasira

Na wewe na wenzako mtakaa kuzimu milele. Mbingu mtaziona kwa mbali sana. Itakuwa kama kisa cha tajiri na Lazaro kwenye Biblia!
 
Back
Top Bottom