SI KWELI Wasira: Maridhiano ni lazima bila hivyo kuna watu watakaa jela milele

SI KWELI Wasira: Maridhiano ni lazima bila hivyo kuna watu watakaa jela milele

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

"Tunapozungumzia maridhiani tunamaanisha Makubaliano ya kitaifa, kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha siyo mtu mzuri kwetu na kwenye taifa ni hatari. Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"- Amesema Wasira

Wasira 2.jpg
Wasira 1.jpg


​
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii, imeibuka Taarifa inayoeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Stephen Wassira ameeleza kuwa maridhiano ni lazima la sivyo kuna watu wataozea jela.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao uebainisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika pia kilichpchapisha taarifa hiyo kumuhusu Stephen Wassira.

Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu umeonesha kuwa Taarifa hiyo imechapishwa na watu wengi Januari 30, 2026 ambapo wote wameandika ujumbe wa aina moja bila kutaja ni wapi na llini kiongozi huyo alitoa nukuu hiyo.

Aidha hakuna kumbukumbu zozote za hivi karibuni zikimuonesha Wassira akizungumza na waandishi wa habari ama kwenye mikutano ya hadhara siku ya Januari 30, 2026.

Katika vipindi tofauti Wasira amewahi kuzungumzia kuwa maridhiano ni jambo la lazima na kama mtu hatotaka basi hatolazimishwa lakini hakuwahi kueleza kuwa atakayekataa ataozea jela. Tazama hapa na hapa ambapo alieleza kuwa;

Sasa kama yupo mtu hataki mazungumzo, hataki amani, hataki maridhiano, hataki kusema na wenzake tutamuacha tu aongee na miti na majani baadae atakapochoka kuongea na miti na majani atakuja tutaongea lakini maridhiano ni jambo la lazima ukikataa unataka nini?
Mtu kama huyu unawaza; unashindwa hata kujuwa bado anahangaikia nini katika uhai wake katika umri huu!

Kuna kitu gani kitakachomwongezea heshima katika kushiriki kwenye uovu dhidi ya taifa lake lililomtunza hadi kufikia umri huu!

Anahangaikia nini, pesa za kununulia sanda la maiti yake; na kusahau kuwa anashiriki katika kuharibu matumaini ya watoto na wajukuu na vitukuu atakavyoviacha nyuma?

Anahangaikia nini hasa wakati huu katika maisha yake.
 
Maneno ya kifedhuli ya Wassira nimeyafurahia sababu amenisaidia kuwatia hasira watu.
Hawa CCM hawaambiliki hawasikii, hawabadiliki.
Wanataka watu waandamane tena kudai kesi ya Lissu itolewe hukumu au aachiwe huru haraka.
Safari hii maandamano yatakuwa makubwa sana ya kumtaka Lissu aachiwe huru.
Hawataamini.
Waache wajidanganye watu wanaogopa kuandamana tena.
Ni zaidi ya kuandamana.

Ukisikia mzee kama huyu anaweweseka namna hiyo ujuwe wanayo hofu kubwa sana ndani ya Genge hilo.

Ni kwamba wamefikia mwisho wa matumaini yoyote ya kubaki madarakani, hata kwa kutumia nguvu.

Vinginevyo, hana sababu kabisa ya kuja na kutamka maneno kama haya hadharani. Yeye anao uhakika gani kuwa watakuwepo madarakani milele, kama siyo ya kuwa na wasiwasi juu ya hali inavyowaendea vibaya wakati huu.
 
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

"Tunapozungumzia maridhiani tunamaanisha Makubaliano ya kitaifa, kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha siyo mtu mzuri kwetu na kwenye taifa ni hatari. Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"- Amesema Wasira

Huyu anaendelea ujinga WA kuuza akiba yetu. Hapa hatuna Kiongozi
 
Uhaini imeende wapi

ndomana lisu alisema huyu mzee debetupu

maridhiano ya kudumu ni badiliko la katiba na sheria bora nchini na sio mdomomchafu wa wasira na gengelake
Usisahau kushtakiwa na kufungwa jela kwa wote waliohusika na mauaji ya Oktoba 29 hasa Samia na washirika wake wote.
 
Anadhani sisi ni Watanzania wale mapoyoyo wa miaka yao ya 70
Sasa maneno kama haya yanaongeza thamani gani katika mchango wako katika kutafuta ukombozi wa nchi hii toka kwa watu waovu kama hawa?

Unao uhakika kweli kwamba waTanzania wa enzi hizo walikuwa ni "mapoyoyo"?

Hii habari uliipata wapi. Wazazi wako walikuwa ni mapoyoyo?

Inatia mashaka sana, kama kweli watu wa aina yako mnaelewa mnachokipigania kwa michango ya namna hii.
 
Mzee naona uwezo kiakili umepungua sana. Ona sasa anamdhalilisha kiongozi wake Samia. Kumbe Lissu siyo mhaini, bali yupo gerezani kwa sababu amekataa maridhiano fake na wauwaji.
 
Mzee naona uwezo kiakili umepungua sana. Ona sasa anamdhalilisha kiongozi wake Samia. Kumbe Lissu siyo mhaini, bali yupo gerezani kwa sababu amekataa maridhiano fake na wauwaji.
Maridhiano baada ya oktoba 29, sababu lissu na TEC wanahusika
 
Sasa maneno kama haya yanaongeza thamani gani katika mchango wako katika kutafuta ukombozi wa nchi hii toka kwa watu waovu kama hawa?

Unao uhakika kweli kwamba waTanzania wa enzi hizo walikuwa ni "mapoyoyo"?

Hii habari uliipata wapi. Wazazi wako walikuwa ni mapoyoyo?

Inatia mashaka sana, kama kweli watu wa aina yako mnaelewa mnachokipigania kwa michango ya namna hii.
Kiwango cha ujinga wa Watanzania wa enzi izo huwezi kukifananisha na wa sasa
 
Uwendawazimu wa uzeeni , kama juu wa Wasira, ni laana kwa jamii yake. Wakati wazee wenzake wenye hekima, kama mzee Warioba, wanaheshimika, Wasira anaonekana ni takataka!!
 
Kiwango cha ujinga wa Watanzania wa enzi izo huwezi kukifananisha na wa sasa
Unajuwaje. Wewe ulikuwa ni mmoja wao?
Ujinga juu ya nini. Hivi hili neno linatumika tu bila ya kujuwa maana yake ni nini?

Umefanya utafiti kulinganisha ujinga wa wakati huo na uliopo sasa, ukapata jibu kuwa ujinga uliomo miongoni mwa jamii wakati huu ni pungufu zaidi ya wakati ule; juu ya maswala gani?
 
Mzee amenena maneno ya makufuru dhidi ya mpigania haki Lisu ambaye wmezuiliwa gerezani bila kosa lolote.

Leo mzee Wasira ameropoka na kusema wanamzuia kwakuwa hataki maridhiano.

Soma mwenyewe hapa chini.

"Tunapozungumzia maridhiani tunamaanisha Makubaliano ya kitaifa, kiutendaji na amani ya kudumu, sasa wewe ukikataa inaonyesha siyo mtu mzuri kwetu na kwenye taifa ni hatari. Kwaiyo hupaswi kuwa huru, utakaa chini ya uangalizi milele"- Amesema Wasira

Uzuri uso wake unaongea kuwa anakaribia kaburi
 
Back
Top Bottom