Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Lile dude liliporomosha uchumi, kwenye kauli za wassira kuna ujumbe wa polepoleWa kusemwa kutoka kwa wakinzani wameisha.Sasa ni mwendo wa kuvaana wao kwa wao.
Bwrge hili, linazid tanua ufa badala ya kuzibaMakamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira ameeleza kuwa hofu kubwa iliyokuwepo miaka minne iliyopita wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ilitokana na mfumo dume uliokuwepo nchini pamoja na hofu waliyokuwa nayo waliokuwa marafiki wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wakihofia mabadiliko ambayo yangefanywa na serikali ya awamu ya sita.
Wasira ameyaeleza hayo leo Alhamisi Agosti 28, 2025 Kawe Jijini Dar Es Salaam, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wanaohudhuria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Kitaifa ya Chama Cha Mapinduzi, akiutaja pia ugonjwa wa Uviko-19, kudorora kwa uchumi pamoja na kifo cha Hayati Magufuli kama majanga makuu aliyofanikiwa kupambana nayo Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka 2021.
"Kila mtu alikuwa na hofu ya aina yake kwasababu ya matatizo ya mfumo dume wengine walifikiri upo uhusiano kati ya Urais na uanaume, wengine walikuwa na matatizo tofauti, wengine walikuwa rafiki wa marehemu na ni haki yao lakini walikuwa na hofu kwamba mabadiliko yale yatawaacha wapi, walitofautisha matakwa yao na matakwa ya watanzania na matatizo tunayoyasikia huko nje yanayokana na hofu hiyo." Amesema Ndg. Wasira.
Katika hatua nyingine Wasira amempongeza Rais Samia kwa utekelezaji mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoikuta na ile aliyoianzisha yeye binafsi ikiwemo ukuzaji wa uchumi ambapo ameeleza kuwa wakati Rais Samia anaingia madarakani uchumi ulikuwa umeporomoka kutoka asilimia 6.9 hadi asilimia 4, huku pia akifanikiwa kuimarisha umoja, amani na mshikamano kwa Watanzania.
Siri huwa zinatoka tu kwa kuropokaKwahiyo wasira yeye hakuwa rafiki yake Magufuli? Sawa marafiki wa wanamtandao ni wakati wenu huu
Hilo hata Samia mwenyewe alisemaga kwamba aliambiwa adui yake mkubwa ni wana ccm wenzakeniliwahi kusema humu...
watu wa samia hawakutegemea Tundu lissu atakua mwiba kwao...
akili zao zinajua magufuli na watu wake ndio wapinzani wao...
lissu alikuja kama surprise, na hawakujua wamfanye nini...
Mr. Baboon! Hizo ndizo sera????Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira ameeleza kuwa hofu kubwa iliyokuwepo miaka minne iliyopita wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ilitokana na mfumo dume uliokuwepo nchini pamoja na hofu waliyokuwa nayo waliokuwa marafiki wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wakihofia mabadiliko ambayo yangefanywa na serikali ya awamu ya sita.