GE2025 Stephen Wasira: Rais Samia aliposhika madaraka marafiki zake Hayati Magufuli walikuwa na hofu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hili lizee ni miongoni mwa watu waliozuia upatikanaji wa katiba mpya kwa kuchakachua rasimu ya Warioba;kwa mujibu wa Polepole!!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Masato Wasira ameeleza kuwa hofu kubwa iliyokuwepo miaka minne iliyopita wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ilitokana na mfumo dume uliokuwepo nchini pamoja na hofu waliyokuwa nayo waliokuwa marafiki wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wakihofia mabadiliko ambayo yangefanywa na serikali ya awamu ya sita.

Wasira ameyaeleza hayo leo Alhamisi Agosti 28, 2025 Kawe Jijini Dar Es Salaam, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wanaohudhuria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Kitaifa ya Chama Cha Mapinduzi, akiutaja pia ugonjwa wa Uviko-19, kudorora kwa uchumi pamoja na kifo cha Hayati Magufuli kama majanga makuu aliyofanikiwa kupambana nayo Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipoingia madarakani mwezi Machi mwaka 2021.

"Kila mtu alikuwa na hofu ya aina yake kwasababu ya matatizo ya mfumo dume wengine walifikiri upo uhusiano kati ya Urais na uanaume, wengine walikuwa na matatizo tofauti, wengine walikuwa rafiki wa marehemu na ni haki yao lakini walikuwa na hofu kwamba mabadiliko yale yatawaacha wapi, walitofautisha matakwa yao na matakwa ya watanzania na matatizo tunayoyasikia huko nje yanayokana na hofu hiyo." Amesema Ndg. Wasira.

Katika hatua nyingine Wasira amempongeza Rais Samia kwa utekelezaji mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoikuta na ile aliyoianzisha yeye binafsi ikiwemo ukuzaji wa uchumi ambapo ameeleza kuwa wakati Rais Samia anaingia madarakani uchumi ulikuwa umeporomoka kutoka asilimia 6.9 hadi asilimia 4, huku pia akifanikiwa kuimarisha umoja, amani na mshikamano kwa Watanzania.

Huyu Mze akamatwe na yeye, hafai kabisa kuonekana hadharani kama Kikwete.
 
Kwa hiyo saiv mpinzani wa samia ni Magufuli sio chadema wala act wazalendo?
 
Huyu Mzee ana siasa za kitoto, sasa nchi tukiendesha Kwa siasa za kitoto, tutakuwa kweli.

Akitumia mfano huo ana maanisha na marafiki WA sasa nao wanaogopa, utawala WA mwingine, ndio maana wamechnga 100bn ili kujilinda, na kuwagaiaya wajinga kiasi cha hizo 10bn, iliwakifika huko juu wajirudishie hiyo 100 bn. Na faida juu.
 
Back
Top Bottom