Stereo Singasinga album yako kali sana, inabidi ujiongeze

Pengine YouTube channel yake bado haujakidhi vigezo vya kulipwa ndio maana hata hahangaiki nayo.
Pengine kuuza albamu yake ndio inampa mtonyo.
Yaani huwezi jua.
Harafu kwani yeye anasemaje?
 
You are not serious either, unatoa ushauri wa kihisia hisia tu, ati atoe "kichupa hata cha mkopo" unadhani hicho kitamfikisha wapi? unajua ubora wa kichupa cha mkopo kulinganisha na kichupa chenye uwekezaji?

Nafikiri anachohitaji ni serious management ndo itafanya yote ikiwemo suala la masoko ama kama anayo basi ishauri management yake, maana umeongea kana kwamba biashara ya muziki ni kama vile biashara ya vitumbu, umeanza na stereo halafu ukaishia na stereo ilihali kuna mnyororo mkubwa sana hapa katikati.

Una nia nzuri ya kumshauri ila approach yako ktk kumshauri haijakaa vizuri unalalamika lamika tu.
 
Yani kwa Tamaduni ..mimi list yangu iko HV

Nikki mbishi

Stereo

One the incredible

Songa

P the Mc

Gheto ambassador

Nash mc

Kad go

Zaiid

Disasta vina
Halipo songa mpandishe dizasta mkuu, Nikki Mbishi namuelewa sana shida sikuizi ananingusha sana sio niki yule kabisa
 
Huyo yeye kapandisha mzuka baada ya kumuona Rayvanny humo. Hajui chochote zaidi kuwa pungasese msukule pale Wasafi.
 
Biashara ya hiphop ni ngumu...mwanangu mwanangu kibao.

Alafu wasanii wa hiphop vichwa vyao kama haziwatoshi unaweka hela leo kesho unakuta kapewa interview katukana radio zote na hawatakagi kuongozwa.
toa mfano[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Labda sijui..Ila nadhani..HipHop ikiimbwa nnje ya kuyagusa maisha halisi ya Mtz huwa naonaga ni Kama takataka...then HipHop inatakiwa sio mamistari magumu ambayo hata hayaelewiki..

Sasa ..unakuta mtu anaimba HipHop za mapenzi..mistari migumu kinoma Yani...

Hivi Roma na Stamina wanaimbaga stail Gani wale...Kuna yule dogo aliyeimbaga Who I am , Mimi ni nani...jamaa anaimba real life...msikilizaji unapata meseji send unaona huu wimbo unanigusa...Kuna ile ya Stamina vs Pro JAy ya baba..it's real life ...

Ama angalia nyimbo za PRo Jay ni HipHop za mapenzi lakini zinaeleweka..

So wasanii wa HipHop wabadilike kuimba majimbo magumu magumu yasiyoeleweka plus yasiyo beba uhalisia wa real life ..wajiandae kufeli tu
 
Nikki mbishi anakwambia usipo ielewa jua haikua kwa ajili yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…