Tabia ya staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta Lulu ya kutojumuika nawenzake kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera klabu ya Bongo Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini, zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria shughuli za wenzie kama misiba au hata sherehe zilianza tangu alipotoka gerezani. Ilisemekana kwamba kilichosababisha viongozi wa Bongo Muvi kukasirishwa na kuamua kumweka kikao ili kumsema, ni kwamba ipo sikunaye yatamfika.
Baada ya kuzinyaka, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie Steven Mengere, Steve Nyerere ambaye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo ili kumuonya kwa tabia yake hiyo kwa kuwa yeye bado mdogo.
Alisema Lulu anatakiwa afuate nyayo za wakubwa zake ambao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali kwa kuwa ipo sikunaye yatamfika.
Lulu ni mtoto mdogo, hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda.
Sisi kama Bongo Movie tuna kawaida yakuhudhuria shughuli za wenzetu pale inapobidi lakini kama mtu anakuwa na udhuru huwa anatoa taarifa lakini yeye hana kawaida hiyo,anajiona amekamilika.
Naaamini ipo siku na yeye yatamfika kwa kuwa mitihani ni kawaida kwa binadamu, sidhani kama mtu atajitokeza na kumuunga mkono kwa tabia hiyo na siyo yeye tu anayejitenga, wapo nawengine wengi lakini yeye bado ni mdogo kwetu huenda hajui alitendalo ndiyo maana tunataka tumfunze jinsi ya kuishi na watu, alisema Steve.
Kwa upande wake Lulu alipotafutwa na kuulizwa juu ya jambo hilo hakuonesha mshtuko bali aliwaka: Huyo aliyesema hivyo atajijua mwenyewe mimi sina shughuli na mtu, aachanena mimi.