Steve Nyerere arekebishe mindset kwanza ndipo aje kwenye Uislamu, asije na mindset hii aliyokuwa nayo

Steve Nyerere arekebishe mindset kwanza ndipo aje kwenye Uislamu, asije na mindset hii aliyokuwa nayo

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
habari za siku nyingi ndugu msomaji,natumai ni mzima na Mungu aendelee kutubariki.

Hivi karibuni msanii wa movie Steve nyerere alionekana akilalamika juu ya yale yanayofanywa na waumini fulani wa Ukristo kwamba ni sio sawa na ni kukashifu dini.

Aidha bwana huyu alikuwa akitolea mifano na kulinganisha na dini ya kiislamu namna wanavyoheshimu dini yao kwa mambo mengi.

USHAURI WANGU ; asichoswe na ukristo kwa yale yanayofanywa na wakristo,kuna wakristo na ukristo,kama yeye ameamua na ni mfuasi kweli wa KRiSTO basi asikatishwe tamaa na yanayofanywa na wakristo kwa sababu yeye anafuata dini na sio watu wa dini hiyo.

Akija na hii mindset kwenye uislamu pia hatodumu kwa sababu wapo watu wa aina hiyo pia wanaokashifu uislamu na ilhali wao pia ni waislamu,hivyo nako atahama ? atahamia wapi ambako hakuna hayo ?

Hivyo kama anataka kuhama aamue kwa sababu ya kwamba ameona ndio njia ambayo imemridhisha kiimani na sio vinginevyo.

Kuna baadhi ya mashekhe wanasema kwamba wakristo wanaheshimu viongozi wao wa dini na kuwathamini na kutolea mifano mambo mengi mazuri kwao,je steve akisikia haya kwa mashekhe atarudi kwenye ukristo ?

Kwenu kwa maoni.
 
Ulilonena mkuu linaukweli 100% asije hakajua UISLAM umepoa tu kma anavyoona kwa njee

Maana akija uku akikuta kuna shuda kidogo atakimbia tena au?!

Sisi WAISLAM tunafundishwa kuifata Din na sio mashekhe! Mashekhe ni watu tu wanabadilika lakin Uislam kamwe haubadiliki!!

Huyo tivu ake afate ukristo unasema nini co kuwafata wakristo wanasema nini na kma anataka kuja kwa uislam bac afanye haraka

Wanao Silimu ni wenye hakili
Mungu umuongoa anaemtaka

UISLAM NI HAKI
 
Tatizo dini yenu bado Ipo kwenye promotion ya propaganda za kutafuta members. Akijiunga mwehu mmoja ambaye zamani alikuwa maarufu, basi kelele zitapigwa dunia nzima, Fulani ni wetu, Fulani ksjua ukweli na kuchangiwa fedha, wenzenu walishatoka huko, ili kumpokea mhamiaji yoyote lazima awe sio amekuja kwa kuahidiwa Bali ameifahamu kweli, na kabla ya kupokelewa anapigwa shule ya Imani yake mpya kwa miaka 3 kimya kimya kwa siku wanakuja maelfu kwa maelfu haitangazwi, ila Kuna mchezaji mchanga juzi hapa utafikiri sijui ni malaika ksjiunga
 
Ulilonena mkuu linaukweli 100% asije hakajua UISLAM umepoa tu kma anavyoona kwa njee

Maana akija uku akikuta kuna shuda kidogo atakimbia tena au?!

Sisi WAISLAM tunafundishwa kuifata Din na sio mashekhe! Mashekhe ni watu tu wanabadilika lakin Uislam kamwe haubadiliki!!

Huyo tivu ake afate ukristo unasema nini co kuwafata wakristo wanasema nini na kma anataka kuja kwa uislam bac afanye haraka

Wanao Silimu ni wenye hakili
Mungu umuongoa anaemtaka

UISLAM NI HAKI
"Hakili" eeh basi sawa kama ndio hivyo
 
Yah mkuu ndio maana nikatoa haya maoni.

Ajue kwamba hata huku uislamuni kuna mambo huwa tunatolewa mifano kwa wakristo namna wanavyoyaendesha vizuri.

Hofu yangu steve asijekuwa anatafuta kiki tu maana sidhani kama hana ufahamu wa kulitambua jambo hili
 
dini yenu bado Ipo kwenye promotion ya propaganda za kutafuta members
SIo kweli kwa sababu wengi hata watu maarufu wanaosilimu wanasilimu kwa mitazamo yao wenyewe hakuna ambaye huwafuata na kuanza kuwapiga somo na kuwashawishi,so kwa mantiki hiyo hoja yako siikubali.

Ili iwe inatafuta watu ingekuwa hao wanaosilimu watu maarufu tuone kwamba walikuwa wanashawishiwa ila hatulioni jambo hilo.
 
Nadhani mmekutana wote akili ndogo hamkueleewna,aliongelea watu wanavyouchezea ukristo hasa wasanii na wakristo wako kimya,ukitaka kusoma rangi mkashifu mtume wao ukione cha moto wanakuua,Yesu anadhihakiwa ila wakristo wanamuachia Mungu atoe hukumu
 
Ni rahisi mkristo kusilimu kuliko muislam kuingia ukristo kutokana muundo wa imani ya kikristo
Ilivyo.
Ukristo ni imani flan complex sanaaa kuilewa ndiyo maana inawekwa kundi moja na quantum physics katika masomo ya ulimwengu.
Ukiuelewa ukristo na ukasikia kuna mtu anaslimu ni lazima ucheke na useme" one man down, roho ya mtu mmoja imepotea. ". 😂😂
 
Back
Top Bottom