Steve Nyerere: Harakati za Makonda kwa Bongo movie ni batili na za kujitafutia umaarufu

Steve Nyerere: Harakati za Makonda kwa Bongo movie ni batili na za kujitafutia umaarufu

ikitokea ametekwa bashite atahakikisha amepatikana kabla ya jumapili

msiwe na hofu
 
Japo Steve Nyenyere ni mfupi lakini leo kaongea point
 
Yupo sahihi, tujiulize mambo gani ambayo makonda kayaanza na akayamaliza kwa kufanikiwa

Tusidanganyane, kuna mambo unaweza ukayaanzisha Duniani na yakafika mwisho kwa kupimika, MF. kujenga nyumba, kujenga reli, kushona nguo.

Lakini huwezi ukaniambia jambo kama la kupambana na Machangudoa, '' Ombamba ", Shisha, Dawa za kulevya, ETI unaweza kulianzisha na likafika mwisho. huu ni uovu na dhambi, hakuna uovu au dhambi ambayo huwa inaisha kwa kupimika. sana sana utaangalia kama wahusika wamepungua lakini huwezi kusema UOVU huu umeisha, NEVER. (nakubali kuelimishwa kwenye hili )

Hebu tujiulize, Kina Mtume Daudi, Musa, Yesu (Issa Bin Mariam), Muhammad walikuja na vitabu kama Zaburi, Taurati, Injili na Qur'an kuhubiri kuacha uovu, je UOVU umeisha hapa Duniani..??

Kama mitume hawa watakatifu wakisaidiwa na miujiza kibao toka kwa MUUMBA MWENYEZI MUNGU walishindwa, sembuse Mchapakazi Paul Christian Makonda.?

Tukubali tu kuwa Makonda anatimiza wajibu wake kwa sasa, na tumuunge mkono, tusitegemee eti Makonda atayamaliza, vinginevyo tutakuwa na Makengeza ya AKILI.

Big Up, Mchapakazi Paul Christian Makonda, fitina na chuki zao watazimeza wao wenyewe. kila mtu hapa Duniani anatimiza wajibu flani, kisha unaondoka hata kama jambo halijamalizika, ndio mitume watakatifu waliondoka hali ya kuwa Duniani dhambi inazidi kushamiri.
 
Mchapakazi Paul Christian Makonda anaweka mchango wake kwenye himaya yake i.e. Dar Es Salaam, sasa habari ya wakuu wa mikoa nchi nzima inatoka wapi tena.? Kwa hiyo Makonda ndio azunguke nchi nzima kuwahamasisha wakuu wa mikoa.?
Huyu Steve Nyerere ana elimu gani hawezi kuchambua hata hii dhana.

Kwa hiyo kwa akili ya Steve, Makonda asipambane na uhalifu wa kazi za wasanii jijini Dar mpaka Rais au Waziri mwenye dhamana atamke.? hapa Steve kapotoka. kila jambo huwa lina chanzo chake, mbona zoezi la ukaguzi wa silaha lilianzia Dar kwa Mchapakazi Paul Christian Makonda, na baadae likasambaa nchi nzima..?? Steve nadhani hafikilii vizuri.

Anyways, namkumbusha tu Steve, Mchapakazi Paul Christian Makonda, amekuwa sababu au chachu kubwa ya kuchochea baadhi mambo hapa Tanzania na baadae yanasambaa nchini kwa msukumo tofauti na uliokuwepo kabla.

Mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpeni. la sivyo na nyie mtapata dhambi ya kumdhulumu haki yake.

Rejea: Ukaguzi wa Silaha na Kampeni ya Dawa za kulevya.
 
Si mmekatazwa kutaja hilo jina kama hamna hoja wekeni katuni tucheke
 
Hako kajamaa bana...huwa nakaona kama sisimizi vile...


Hata Kawawa alikuwa hivyohivyo....ila muziki wake sasa!

ccm-1-25.JPG
 
kumbe vitu vingi vinavyoanzishwa Dar vinafeli?? Wanaume wa Dar tatizo nini eti??
 
Steve Nyerere amedai kuwa kupigania Bongo movie dhidi ya maharamia wa filamu feki ni batili na za kujitafutia umaarufu kwa kuwa hilo ni suala la kitaifa linalotakiwa kuratibiwa nchi nzima na wakuu wote wa mikoa na polisi na sio Dar tu kwa kuwa vitu vingi vinavyovyoanzishwa hapa Dar vinafeli,
Pia alisema pia Makonda aliwaita watu watano, na tasnia ya filamu haiongozwi na watu hao

Du kazi kweli kweli.
 
makonda anavyo hangaika wakati mwingine utafikiri mtoto,yaani kwa cheo alichopewa kukaa anahangaika kushindana kusikika kwenye media na hawa kina steve ufedhuli,steve yuko sawa kabisa japo mimi sio mshabiki wao hata kidogo
 
Back
Top Bottom