Yupo sahihi, tujiulize mambo gani ambayo makonda kayaanza na akayamaliza kwa kufanikiwa
Tusidanganyane, kuna mambo unaweza ukayaanzisha Duniani na yakafika mwisho kwa kupimika, MF. kujenga nyumba, kujenga reli, kushona nguo.
Lakini huwezi ukaniambia jambo kama la kupambana na Machangudoa, '' Ombamba ", Shisha, Dawa za kulevya, ETI unaweza kulianzisha na likafika mwisho. huu ni uovu na dhambi, hakuna uovu au dhambi ambayo huwa inaisha kwa kupimika. sana sana utaangalia kama wahusika wamepungua lakini huwezi kusema UOVU huu umeisha, NEVER. (nakubali kuelimishwa kwenye hili )
Hebu tujiulize, Kina Mtume Daudi, Musa, Yesu (Issa Bin Mariam), Muhammad walikuja na vitabu kama Zaburi, Taurati, Injili na Qur'an kuhubiri kuacha uovu, je UOVU umeisha hapa Duniani..??
Kama mitume hawa watakatifu wakisaidiwa na miujiza kibao toka kwa MUUMBA MWENYEZI MUNGU walishindwa, sembuse Mchapakazi Paul Christian Makonda.?
Tukubali tu kuwa Makonda anatimiza wajibu wake kwa sasa, na tumuunge mkono, tusitegemee eti Makonda atayamaliza, vinginevyo tutakuwa na Makengeza ya AKILI.
Big Up, Mchapakazi Paul Christian Makonda, fitina na chuki zao watazimeza wao wenyewe. kila mtu hapa Duniani anatimiza wajibu flani, kisha unaondoka hata kama jambo halijamalizika, ndio mitume watakatifu waliondoka hali ya kuwa Duniani dhambi inazidi kushamiri.