Steve Nyerere: Ni unafiki Wasanii kufuta picha za kampeni CCM, mnadhani wataacha kuwatukana? Tayari Rais tunaye

Steve Nyerere: Ni unafiki Wasanii kufuta picha za kampeni CCM, mnadhani wataacha kuwatukana? Tayari Rais tunaye

Msanii wa Bongo Movie Steven Nyerere kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram ameandika kuhusiana na Muenendo wa wasanii wengi kufuta picha zao wakiwa katika kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema ni unafiki na kutokuwa na msimamo

"Mstafuuu,....Nimeona Wasanii wengi Wanafuta Picha za Kampeni, Na wengine wana Archive Wakiamini baadaye watazirudisha ni Utoto mkubwa Unafanyika,..Unafuta Picha ili Iweje, Je Unadhania Picha zinaweza kusababisha watu wasikutukane Tunasahau Umaarufu Sifa yake ya kwanza Kukosolewa kutukanwa kudhalilishwa ,Hata ufanye Zuli lipi hapa Duniani lazima wakosoaji Wapo na bahati mbaya zaidi Wakosoaji wetu ni wale wao hawakuwahi kujaribu wala kufanya lolote kwenye hili Taifa

Nimeona Wasanii wengi Wanafuta Picha Za kampeni, Najiuliza kwa lipi mpaka mfute ,...Je ni makosa msanii kufanya kampeni kwa chama chochote anacho kipenda

Unafiki wa hali ya juuu sana ,Lakini Pia ni Uchochezi wa chini kwa chini Ambao sio kitu kizuri kabisa ,..Wakati mnapiga Simu na kuomba Shooo Wakati mnapiga simu kuomba kushiriki naimani mlikuwa na Akili timamu na mlijua Siasa ni mchezo mchafu Vuta nikuvute mlitambua kuna picha na mkajua kupost pia leo hata siku 20 Mikwala kidogo mnafuta Picha Hii inawafanya hata jamii kuwaona Amna misimamo,...Unapo Amua kusimama na Mtu simama naye Iwe Mvua Iwe Jua

Na Unapo Amua kuingia kwenye kampeni yoyote Tambua kuna Faida na hasara pia, ..Tambua lazima kuna hari mtapitia hapo ndipo sehemu sahihi ya kubaki na misimamo yako kwa heshima kubwa uliyo Jenga

Kufuta picha zote za kampeni ni Unafiki ,Kujisafisha wakati hata hao wanaotoa jasho kukutukana ni kwa vile walikosa hiyo nafasi uliyopata wewe kwa hiyo usidhani kuna Furaha kwenye mioyo yao

Lakini kikubwa zaidi Uchaguzi Umekwisha na tayari Tunaye Rais,...na muda si mrefu serikali Inaingia kazini kuhudumia Watanzania kwa maslahi mapana Tanzania

Kuna muda Tukubaliane kusimamia misimamo
Kuna Muda Tukubali kusimamia kile tulicho kiamini
Kuna muda Tuamini heshima nyingine inakuja kwa msimamo wako

Tusonge mbele hakuna kitakacho futika Ukifuta picha Tunabaki kwenye kumbu kumbu tu Ya Technology

Tusonge mbele kujenga Taifa lenye Utu na kufanya kazi

HUKU MNATAKA NA HUKU MNATAKA KILA MAHALA MNATAKA KUONEKANA WAZURI SIO SAWA NI UNAFIKI MKUBWA UCHONGANISHI MKUBWA SIMAMA NA MSIMAMO WAKO ACHA KUYUMBISHA ROHO YAKO"- Ameandika Steve Nyerere
Ivi nani mkubwa kati ya Steve Nyerere na Andrew Nyerere?
 
Steve ana maoni gani kuhusu kesi ya uhaini ya Niffer.

Je ameshagngilia
 
Kama haikuwa utoto wakati wanaziweka (wanalipwa ) na sasa hivi wanaona hazilipi wala sio kwamba Chama kinalipia uwepo wa hizo picha basi nadhani ni vema kwao kuzifuta - After all it's all about Quid Pro Quo - Mtu anafanya kile kinachomlipa na ni Utoto kwa mtu kulazimisha wanaofuta wasifute (Yeye kama anaona zinalipa akae nazo au awalipe hao wanaofuta ili wasifute)
 
Back
Top Bottom