Nenda pale Stand ya mkoa, uliza kwa wale Askari polisi, Watakuelekeza zinakopatikana.
Ila acha hasira barabarani, Wanaudhi ni wengi, bodaboda Bajaji na Daladala.
Leo niko kibaha, nilisimama pale maliasili, wanaposima trafiki kwa lengo la kulichunguza gari, askari mmoja akaja, akaniomba leseni na stika ya nenda kwa usalama.
Stika ilibanduka ila niliihigadhi, nilipomuonyesha wala hakutaka tena kuiona leseni. Ubungo mwanzo mwa daraja ukitokea mbezi, nimesimamishwa, nikaulizwa tena nimewaonyesha nimepita zangu, Hivyo nakushauri upunguze hasira barabarani, itakusaidia hao ndiyo kazi yao, na kiburi siyo Maungwana.