esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ru ji (Stiegler’s Gorge) umean- za kwa kasi kubwa. Amesema mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy Electric za Misri umeanza kwa kasi baada ya vifaa vyote husika kukishwa eneo la mradi.
Waziri Kalemani alisema hayo juzi baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo mkubwa na kujionea jinsi ulivyoanza kwa kasi kwa vifaa vyote atakavyotumia mkandarasi wa ujenzi kuwasili.
“Kila kitu kipo eneo la mradi na hatua ya ujenzi inaendelea na umeanza kwa kasi, wakandarasi wapo eneo la mradi na wasimamizi ambao ni wazawa...kulingana na matayarisho ya mkandarasi alivyonipitisha hatua ya ujenzi sasa zinaenda kutekelezwa kwa vile mabuldoza na matingatinga na magari yapo eneo la mradi, na kazi hii itakamilika kama ilivyopangwa Juni mwaka 2022,” alisema.
Waziri Kalemani alisema wakandarasi walio eneo la mradi wanasema hawana vikwazo na wanaendelea na ujenzi wa mradi huo. Aliitaka kampuni ya ubia inayojenga mradi huo kutoa kipaumbele cha kutumia wataalamu wa ndani wenye uwezo katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa mradi huo mkubwa nchini.
Aliwataka wakandarasi wanao- jenga kingo ya kuzuia maji katika mradi huo wa aina yake nchini kujenga kwa kutumia muda mfupi ili waweze kumaliza ujenzi huo na kuendelea na hatua nyingine za ujenzi huo. “Ujenzi wa kingo ya kuzuia maji mkandarasi alipanga kutumia miezi 12 lakini tumemwomba ajenge ndani ya miezi tisa au 10 ili kutoa fursa ya kuendelea na kazi nyingine kwani wafanya kazi 420,” alisema.
Pamoja na hayo, Waziri Kale- mani aliwaagiza wakandarasi wa kampuni inayojenga mradi huo kutumia vifaa vya ujenzi ambavyo vinapatikana ndani ya nchi isipokuwa vile visipopatikana hapa nchini.
“Hili ninarudia wakanda- rasi wa mradi hakikisheni vile vifaa vya ujenzi vinavyopatikana nchini kama nondo, saruji na bati isipokuwa ambavyo havipatikani kulinda viwanda vya ndani,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo aliwataka vijana kujitokeza kupata ajira katika mradi huo na wawe waaminifu wakati wa ujenzi wa mradi huo. “Miradi mingi mikubwa inayoendelea kumejitokeza wizi wa vifaa na mafuta unaofanywa na Watanzania wasio waaminifu,” alisema Chonjo na kuongeza vijana 400 waliojiunga na jeshi la akiba ndio watapewa kipaumbele katika mradi huo ili wawe ni walinzi kuona mradi hauhujumiwi kwa namna yoyote ile,” alisema.
Mkataba wa mradi huo uliosainiwa Desemba mwaka 2018, ni wa Sh trilioni 6.5 na utatekelezwa kwa miezi 36 kupitia Kampuni ya ubia ya Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka nchini Misri. Katika kuhakikisha mradi huo unapewa msukumo mkubwa, Oktoba 4, mwaka 2018, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea na kukagua maendeleo ya mradi na alimtaka kila mmoja aliyepewa jukumu la kusimamia mradi huo ahakikishe anawajibika kikamilifu ili mradi huo ufanikiwe.