Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,170
Enoki alimzaa Methusela aliyemzaa Lameki ambaye alikujaa mzaa Noah. Huyu Noah ndio wa kipindi cha gharika! (Kutoka 5:29).
Kipindi hicho malaika waasi wameshuka duniani kula 'good times' na watoto wazuri wa mama Gaia (dunia), ikapelekea kuzaliwa kizazi cha ajabu zaidi kuwahi tokea!. Kile kizazi unaambiwa kilikuwa kinajamiiana hadi na mijusi, Imagine!.
Basi kuna jamaa mcha Mungu sana alikuwepo aliyeitwa Methusela huyu jamaa aliishi na kuona yale maovu mengi sana (kwanza ndio mtu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani-Miaka 999) akamchagulia mke mtoto wake mkubwa anayeitwa Lameki, yule mke akapata mimba baadae akajifungua mtoto wa kiume. Tatizo likawa mtoto aliyezaliwa!.
Yule mtoto mwili ulikuwa mweupe kama barafu, una ng'aa kama ua rose na nywele nyeupe laini kama sufu!. Macho ya dogo yalikuwa mazuri sana kuyatazama na akiyafungua yanatoa mwanga mkubwa unaomulika nyumba kama jua. Dogo katoka zaliwa tu badala ya kulia akaanza tangaza utukufu wa mwenyezi Mungu!. Mzee Lameki akaogopa sana akijua kachapiwa mke tayari na wale malaika waasi walioshuka duniani, ikambidi akimbilie kwa baba yake kuomba ushauri!.
Kufika kwa Methusela akamwambia "Nimepata mtoto wa ajabu sana, sio kama sisi binadamu huyu ni kama wale Malaika. Inaonekana kabisa sio damu yangu, pale hawa jamaa wamenipigia mke na naogopa nini kitatokea huyu mtoto akiwa mkubwa. Nakuomba nenda kwa babu (Enoki) ukaulizie hii habari yeye amekaa nao sana hawa Malaika atakuwa na msaada kwa hili."
Ikabidi Methusela aende kuomba aweze ongea na baba yake kujua huyu mjukuu wake itakuaje. Enoki kusikia kisa akamtuliza Methusela kwamba akamwambie Lameki mtoto aliyezaliwa ni mtoto wake kabisa wala asiogope na ndio mtoto pekee yeye na watoto wake watatu watakaokuja bakia dunia wakati ambao Mwenyezi Mungu ataangamiza viumbe wote duniani kwa kuasi maelekezo yake!. Na mtoto wakamuite NOAH yaani 'comfort' au 'faraja' kipindi ambacho dhambi itaangamizwa duniani.
SOURCE: The book of Methuselah.

- Kitanda hakizai haramu.
- Usikurupue maamuzi kwenye mambo magumu.
- Mipango ya Mwenyezi Mungu ya ajabu siku zote.
- Mficha maradhi.....