Stori ya Kuzaliwa Noah: Baba wa gharika

Stori ya Kuzaliwa Noah: Baba wa gharika

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Enoki alimzaa Methusela aliyemzaa Lameki ambaye alikujaa mzaa Noah. Huyu Noah ndio wa kipindi cha gharika! (Kutoka 5:29).

Kipindi hicho malaika waasi wameshuka duniani kula 'good times' na watoto wazuri wa mama Gaia (dunia), ikapelekea kuzaliwa kizazi cha ajabu zaidi kuwahi tokea!. Kile kizazi unaambiwa kilikuwa kinajamiiana hadi na mijusi, Imagine!.

Basi kuna jamaa mcha Mungu sana alikuwepo aliyeitwa Methusela huyu jamaa aliishi na kuona yale maovu mengi sana (kwanza ndio mtu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani-Miaka 999) akamchagulia mke mtoto wake mkubwa anayeitwa Lameki, yule mke akapata mimba baadae akajifungua mtoto wa kiume. Tatizo likawa mtoto aliyezaliwa!.

Yule mtoto mwili ulikuwa mweupe kama barafu, una ng'aa kama ua rose na nywele nyeupe laini kama sufu!. Macho ya dogo yalikuwa mazuri sana kuyatazama na akiyafungua yanatoa mwanga mkubwa unaomulika nyumba kama jua. Dogo katoka zaliwa tu badala ya kulia akaanza tangaza utukufu wa mwenyezi Mungu!. Mzee Lameki akaogopa sana akijua kachapiwa mke tayari na wale malaika waasi walioshuka duniani, ikambidi akimbilie kwa baba yake kuomba ushauri!.

Kufika kwa Methusela akamwambia "Nimepata mtoto wa ajabu sana, sio kama sisi binadamu huyu ni kama wale Malaika. Inaonekana kabisa sio damu yangu, pale hawa jamaa wamenipigia mke na naogopa nini kitatokea huyu mtoto akiwa mkubwa. Nakuomba nenda kwa babu (Enoki) ukaulizie hii habari yeye amekaa nao sana hawa Malaika atakuwa na msaada kwa hili."

Ikabidi Methusela aende kuomba aweze ongea na baba yake kujua huyu mjukuu wake itakuaje. Enoki kusikia kisa akamtuliza Methusela kwamba akamwambie Lameki mtoto aliyezaliwa ni mtoto wake kabisa wala asiogope na ndio mtoto pekee yeye na watoto wake watatu watakaokuja bakia dunia wakati ambao Mwenyezi Mungu ataangamiza viumbe wote duniani kwa kuasi maelekezo yake!. Na mtoto wakamuite NOAH yaani 'comfort' au 'faraja' kipindi ambacho dhambi itaangamizwa duniani.

SOURCE: The book of Methuselah.

  • Kitanda hakizai haramu.
  • Usikurupue maamuzi kwenye mambo magumu.
  • Mipango ya Mwenyezi Mungu ya ajabu siku zote.
  • Mficha maradhi.....
 
we jamaa simulizi lako limekaa kishkaji sana, ila sie wengine tunamini biblia ya vitabu 66 tu hivyo vingine ni stori za wanatheolojia
 
Enoki alimzaa Methusela aliyemzaa Lameki ambaye alikujaa mzaa Noah. Huyu Noah ndio wa kipindi cha gharika! (Kutoka 5:29).

Kipindi hicho malaika waasi wameshuka duniani kula 'good times' na watoto wazuri wa mama Gaia (dunia), ikapelekea kuzaliwa kizazi cha ajabu zaidi kuwahi tokea!. Kile kizazi unaambiwa kilikuwa kinajamiiana hadi na mijusi, Imagine!.

Basi kuna jamaa mcha Mungu sana alikuwepo aliyeitwa Methusela huyu jamaa aliishi na kuona yale maovu mengi sana (kwanza ndio mtu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani-Miaka 999) akamchagulia mke mtoto wake mkubwa anayeitwa Lameki, yule mke akapata mimba baadae akajifungua mtoto wa kiume. Tatizo likawa mtoto aliyezaliwa!.

Yule mtoto mwili ulikuwa mweupe kama barafu, una ng'aa kama ua rose na nywele nyeupe laini kama sufu!. Macho ya dogo yalikuwa mazuri sana kuyatazama na akiyafungua yanatoa mwanga mkubwa unaomulika nyumba kama jua. Dogo katoka zaliwa tu badala ya kulia akaanza tangaza utukufu wa mwenyezi Mungu!. Mzee Lameki akaogopa sana akijua kachapiwa mke tayari na wale malaika waasi walioshuka duniani, ikambidi akimbilie kwa baba yake kuomba ushauri!.

Kufika kwa Methusela akamwambia "Nimepata mtoto wa ajabu sana, sio kama sisi binadamu huyu ni kama wale Malaika. Inaonekana kabisa sio damu yangu, pale hawa jamaa wamenipigia mke na naogopa nini kitatokea huyu mtoto akiwa mkubwa. Nakuomba nenda kwa babu (Enoki) ukaulizie hii habari yeye amekaa nao sana hawa Malaika atakuwa na msaada kwa hili."

Ikabidi Methusela aende kuomba aweze ongea na baba yake kujua huyu mjukuu wake itakuaje. Enoki kusikia kisa akamtuliza Methusela kwamba akamwambie Lameki mtoto aliyezaliwa ni mtoto wake kabisa wala asiogope na ndio mtoto pekee yeye na watoto wake watatu watakaokuja bakia dunia wakati ambao Mwenyezi Mungu ataangamiza viumbe wote duiani kwa kuasi maelekezo yake!. Na mtoto wakamuite NOAH yaani 'comfort' au 'faraja' kipindi ambacho dhambi itaangamizwa duniani.

SOURCE: The book of Methuselah.

  • Kitanda hakizai haramu.
  • Usikurupue maamuzi kwenye mambo magumu.
  • Mipango ya Mwenyezi Mungu ya ajabu siku zote.
  • Mficha maradhi.....
Japo imekaa kisela sela, ila kiimani nimeelewa
 
we jamaa simulizi lako limekaa kishkaji sana, ila sie wengine tunamini biblia ya vitabu 66 tu hivyo vingine ni stori za wanatheolojia
Hiyo story mbona ipo kwenye kitabu cha Enoko ambacho Biblia hiyo ya vitabu 66 inakitambua..... Soma hapo sura ya 106 utaikuta full story
Screenshot_2018-10-27-00-14-43.png

Na kuhusu Henoko kitabu kutambuliwa kwenye Bible tunaona Yuda akinakiri maneno kutoka book of Enoch

Yuda 1
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu

Mstari huu Yuda alinakiri directly kutoka Book of Enoch 1 sura ya 1:9

Kwahiyo kama Mitume wa Biblia walinakiri na kusoma BOOK OF ENOCH ambayo ina story hii ya NUHU je huoni kama unadai unaamini Biblia ya vitabu 66 itakupasa uamini hao mitume ambao pia WANAAMINI book of ENOCH!!

Kazi kwako

Cc lifecoded Kudo Malcom Lumumba
 
naomba unitajie vipimo vya safina ya noah
Ndefu kutosha urefu wa Twiga
Pana kuwatosha wanyama wanene kama Tembo na Kiboko
'swimming pool' ilikuwepo kuishi Sangara na Sato
Iligawanywa vyumba kuruhusu Simba na Swala kukaa ndani pamoja!.
Vyumba 'self contained' vilikuwepo kuiweka familia ya Noah kwenye good mood kipindi chote!.
 
we jamaa simulizi lako limekaa kishkaji sana, ila sie wengine tunamini biblia ya vitabu 66 tu hivyo vingine ni stori za wanatheolojia
Hata hivyo vitabu 66 vilikusanywa na wanatheolojia toka maandiko ya stori za mwaka 48!.
Hawakuwahi kaa Malaika kuunda biblia duniani wala mbinguni.
🙂🙂
 
Hiyo story mbona ipo kwenye kitabu cha Enoko ambacho Biblia hiyo ya vitabu 66 inakitambua..... Soma hapo sura ya 106 utaikuta full storyView attachment 912357

Na kuhusu Henoko kitabu kutambuliwa kwenye Bible tunaona Yuda akinakiri maneno kutoka book of Enoch

Yuda 1
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu

Mstari huu Yuda alinakiri directly kutoka Book of Enoch 1 sura ya 1:9

Kwahiyo kama Mitume wa Biblia walinakiri na kusoma BOOK OF ENOCH ambayo ina story hii ya NUHU je huoni kama unadai unaamini Biblia ya vitabu 66 itakupasa uamini hao mitume ambao pia WANAAMINI book of ENOCH!!

Kazi kwako

Cc lifecoded Kudo Malcom Lumumba
We jamaa me nachokukubali hupiti shortcut kama vilaza sie! [emoji23] [emoji23]
 
Hahahhaha kwa hii source ngoja wafia dini waamke asubuhi patakua hapatoshi humu mkuu 😛😀
Umewaelimisha sana, wataogopa kuja ushatokea mzee wa kuwapinga kwa vifungu! [emoji23]
 
Back
Top Bottom