Stori ya kweli ya maisha yangu, pitia unaweza kujifunza kitu

Stori ya kweli ya maisha yangu, pitia unaweza kujifunza kitu

double click

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
569
Reaction score
949
Natumaini mko salama katika ujenzi wa taifa hii ni story ya kweli kuhusu maisha yangu nimeamua leo kuisema ila kuna ambavyo mnaweza kujifunza.

Nilipomaliza chuo(nilisoma kilimo) niliamua kwenda wilaya ya kilosa mkoa wa Morogoro katika utafutaji nilienda huko kulima mazao haya ya bustani hasa nyanya, hoho na vitunguu nashukuru Mungu kiukwel alinibariki nikawa napata pesa kupitia kilimo.

Nilifanikiwa kupata bint tumuite H tukaanza nae mahusiano ya kimapenz kiukwel ndan ya muda mfupi yule bint tulifanikiwa kupendana sana had ndugu zake wakafahamu kuwa niko na bint yao

Kuna siku moja jiran yao na huyo mwanamke aliniita akaniulza unamjua vyema huyu bint nikasema namfahamu lakin sana ila akaniambia kaa subir utakuja kuona[emoji24][emoji24][emoji24]

Tuliishi kwa amani na upendo ila siku moja nikiwa niko kazin kwenye shughuli zangu za shamba nikapigiwa simu nirud nyumbani kuna matatizo kiukwel nilichukua usafir wangu haraka kurud nyumban nilipofika nilikuta umati mkubwa sana wa watu, ando nikamuona huyo mpenz wangu akiwa amelala chin....kuuliza kulikoni nikaambiwa amepandisha majini(kile nilichoambiwa nitaona ndio hiki)

Baada ya masaa kadhaa mpenz wangu alikaa sawa na kumbukumbu zikaanza kumuijia nilikaa siku mbili tatu nikamuuliza kwan huwa una majin akaniambia ndio na anayo toka muda mrefu wameshapambana had kwa waganga lakin hawakupata mafanikio mie nikamuahid kuwa nitamsaidia ili awe sawa(kosa)

Kiukwel niliwashirikisha ndugu zake juu ya lengo langu la kutaka kumsaidia binti nilianza jitihad za kutafuta waganga ili niweze kumsaidia nilipata waganga weng ila kuna mmoja tu ndio alifanikiwa kumsaidia mpaka akapona

Mganga alivyokuja siku ya kwanza alihitaj kikao cha faragha na mimi akaniambia kuwa kuna vitu anataka kuniambia kama nikiviamin tunaweza kufanya kazi, alisema yafuatayo

1. Kuwa hili tatizo alilonalo mpenz wangu chanzo kikuu ni familia yake yaan familiacyao ni ya kichawi na ndio wanaomloga

2. Nikubali kufa pia maana vita ninayoingia sio ya kitoto

3. Ninaweza nikafirisika yaan mirad yangu yote niliyonao badae inaweza ikayumba na nikawa maskin( mirad nitayotoa pesa kumsaidia huyu mwanamke)

Kwa kuwa nilikuwa nampenda nilikubali hvo vyote ili mradi huyu mwanamke wangu apone

Kiukwel safari huyu mwanamke mpak anapona ni ndefu sana ila kuna matukio meng san hapa nmepitia km kutembea uchi, kukutana na mauza uza kama mapembe n.k (siwez kusimulia kwa kuwa ni meng sana) i

Kiufup ni kuwa bibi yake ni huyu mwanamke alikuwa ni mchaw sana aliuua watoto wake 5 kati ya tisa ili kulipa damu kwenye chama chao cha kichawi.

Finally mwanamke wangu alipona na familia nzima ikawa na furaha na akafaniwa kushika ujauzito na Mungu akamsaidia akajifungua mtoto wa kiume niliipenda sana na kuijali familia yangu ila kipind cha nyuma shangaz yake mkubwa na huyu mwanamke aliwah kuniambia familia uliyoingia sio nzur ish nayo kwa akili na pia mama yangu aliwah kuniambia kuwa akilala anaota kuwa mwanamke nilienao sio sahih kwangu hvo niachane na haraka ila kwa kuwa mapenz ni upofu niliamua kupuuzia yote na kuendelea na mambo yangu.

Maisha yalisonga mbele huku nikipata mafanikio nikajenga nyumba na nikafungua bar na nikawa na mashamba mengi.

Baada ya miaka kwenda ule utabiri kuwa utaanza kufirisika ulianza yaan mambo yangu meng yalianza kwenda ndivyo sivyo kuanzia shambani had kwenye biashara zangu kiukwel nilifuria sana sana had pale kijijin wakajua huyu jamaa tayar kafirisika.

Mpenzi wangu alivyoona nmeanza kukosa pesa alianza dharau na hakutaka kushiriki na mimi chochote hasa mapenz zilianza dharau had ndugu zake pia walianza kunidharau nilitumia pesa nying kutatua matatizo binafs ya mwanamke wng na mtoto na pia ndugu wa mwanamke wangu hasa mama yake aliekuwa anasumbuliwa na uvimbe clinic kila mwez na nilikuwa natoa pesa ndefu, kusomesha mtoto wa marehemu kaka yake n.k

Nilipitia ukame mkubwa sana nikaanza kuuza vitu vya ndani km vile tv na vitu vya kwenye biashara kama friji, tv n.k nilipona vitu vya ndan vimeisha nikaanza kuuza had simu zangu, nguo zangu, viatu n.k

Niliuza vitu ikiwemo had simu nikawa natembea na line tu mfukon....nilipoona mambo yamekuwa magumu nilimtafutia mwanamke wang kaz kwenye shirika fulan hv(kosa kubwa zaid) ili tuweze kusaidiana majukumu kipind hiko nip kwenye matatizo.

Mwanamke alipopata kaz alianza dharau sana na alifikia hatua akaanza kutembea na mmoja wa wafanyakaz wenzie wakawa wanapigiana simu na kuchat muda wote.

Nilipopeleka malalamiko kwa mama mkwe na wazaz wake walisema siwez kumuoa bint yao tyr amechumbiwa na mtu mwingne tokana na kukosa kwangu pesa nilidharauliwa sana.

Nilipitia meng san ila bado nilijaribu vumilia mwanamke alipoona nazid kumban kuwa nae alienda kwa mganga akitaka kuniloga niwe chiz ili niondoke (nilikuta makafara kabatin kwetu)

Mapenz yalizd kufifia na matus yakawa meng kutoka kwa wanaume wake niliamua kukimbia nyumban kwangu na kwenda kuish kwa mjomba wangu.

To cut story nilikuja kufanikiwa badae na yeye sasa hv ana maisha magumu sana.

Mungu n mwema
 
Lengo lao limetimia walitaka uachane na binti yao ambae tayari yupo kwenye hesabu za kichawi either kutolewa kafara kwa mungu wao lucifer au kumrithisha kiti cha uchawi.

Mama yake anaeongezewa damu KILA mwezi means ananyonywa damu na majini so ni lzm awe anaongezewa.
Usioe familia ya kichawi au waganga tegemea kupata yafuatayo kuzaa watoto wenye kifafa , watoto wenye shida ya sikocell.
 
Lengo lao limetimia walitaka uachane na binti yao ambae tayari yupo kwenye hesabu za kichawi either kutolewa kafara kwa mungu wao lucifer au kumrithisha kiti cha uchawi.
Mama yake anaeongezewa damu KILA mwezi means ananyonywa damu na majini so ni lzm awe anaongezewa.
Usioe familia ya kichawi au waganga tegemea kupata yafuatayo kuzaa watoto wenye kifafa , watoto wenye shida ya sikocell.
Nashukuru Mungu nilitoka huko salama
 
Tafakari Sana mtu yeyeto hata usiyemjua akikupa taadhari usioe / olewa na .... Au akikwambia huyo mtu unamjua?

Dini na mila zinakataza watu kuonjana kabla ya ndoa lengo kuu ni kuepusha upofu Ili upate mwenza sahihi, mkianza kutafunana huwezi ona mapungufu ya mwenzio.

Chunguza kama rafiki kwanza ridhika kisha ndo utafune. Wengi wametumbukia kwenye shida kuu baada ya kunaswa na ulimbo. Ukishaanza kulamba tu asali ni ngumu kuchunguza
 
Jitengeneze kabisa uvunje kabisa connection zao japo ni ngumu sababu tayari kuna mtoto umeunganishwa nao.
Mtoto hana kosa unaweza mkomboa au kumlinda kiroho asiwe connected na wapumbavu.
Asante kwa ushaur wako tyr nmeshaufanyia kaz maana mtoto wang sasa yuko karibu na familia yangu kuliko huo upande wa kichaw
 
Natumaini mko salama katika ujenzi wa taifa hii ni story ya kweli kuhusu maisha yangu nimeamua leo kuisema ila kuna ambavyo mnaweza kujifunza.

Nilipomaliza chuo(nilisoma kilimo) niliamua kwenda wilaya ya kilosa mkoa wa Morogoro katika utafutaji nilienda huko
Hongera sana kwa stori ambayo Ina mwisho zile za itaendelea zinakuja kuwaga miyeyusho sana

Kwenye maisha mwanamke wako anatakiwa asiwe na kazi nzuri kukuzid wengio wao sio wote lazima wataanza kukuletea dharau
 
Hongera sana kwa stori ambayo Ina mwisho zile za itaendelea zinakuja kuwaga miyeyusho sana

Kwenye maisha mwanamke wako anatakiwa asiwe na kazi nzuri kukuzid wengio wao sio wote lazima wataanza kukuletea dharau
Asante lengo ni wengi tujifunze maana dunia ina meng
 
Back
Top Bottom