tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Usuli
Shindano la stories of change lilianzishwa na JamiiForums mnamo mwaka wa 2021 na kufanyika mfululizo kila mwaka hadi mwaka 2024. Katika hali isiyotarajiwa na wanachama wote wa JF, mwaka wa 2025 shindano hili halikufanyika kabisa.
Kama mnavyofahamu, shindano hili hufuatiwa na uchambuzi wa minakasha ya washiriki (kwa kutumia wataalamu wabobezi katika uandishi) na utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano. Mchakato wote huu unahusisha fedha kutoka kwa wafadhili. Ni wazi kuwa fedha za wafadhili hazitolewi kama njugu bali huombwa kwa kufuata utaratibu unaokubalika.
Kwa kuwa mwaka 2025 shindano halikufanyika ni wazi kuwa ufadhili ulikosekana. Kukosekana kwa ufadhili mwaka iliopita haimaanishi kuwa shindano hili limefika tamati.
Nini kifanyike?
Ili shindano lifufuliwe mwaka huu, nashauri watafutwe wafadhili wa ndani kufadhili shindano hili. Wafadhali ninaopendekeza ni pamoja na mabenki, kampuni za simu na kampuni binafsi za biashara kama vile MeTL, GSM, Bakhressa Group of Companies, na Civil Societies kama vile TLHRC, TLS, nk.
Nini wanaJF tufanye?
Kwa upande wetu wanaJF nashauri tupige kura za kuunga mkono na tutoe maoni kwenye huu uzi kwa wingi kadri itakavyowezekana. Uzi huu utatumika kama ushahidi wakati uongozi wa JF utakapoenda kuomba ufadhili kwa wahusika.
Wafadhili wanataka kuona mwitikio chanya wa wafadhiliwa. Kwa maana hiyo, nawaomba wanaJF wote tupige kura na tupigie debe suala la ufadhili ili mwaka huu tufufue shindano la stories of change hapa JF.
Nawasilisha.