Stories of change 2026; piga kura yako hapa

Je, unakubali JF ifufue shindano la stories of change mwaka huu wa 2026?(

  • Total voters
    15

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Usuli
Shindano la stories of change lilianzishwa na JamiiForums mnamo mwaka wa 2021 na kufanyika mfululizo kila mwaka hadi mwaka 2024. Katika hali isiyotarajiwa na wanachama wote wa JF, mwaka wa 2025 shindano hili halikufanyika kabisa.

Kama mnavyofahamu, shindano hili hufuatiwa na uchambuzi wa minakasha ya washiriki (kwa kutumia wataalamu wabobezi katika uandishi) na utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano. Mchakato wote huu unahusisha fedha kutoka kwa wafadhili. Ni wazi kuwa fedha za wafadhili hazitolewi kama njugu bali huombwa kwa kufuata utaratibu unaokubalika.

Kwa kuwa mwaka 2025 shindano halikufanyika ni wazi kuwa ufadhili ulikosekana. Kukosekana kwa ufadhili mwaka iliopita haimaanishi kuwa shindano hili limefika tamati.

Nini kifanyike?
Ili shindano lifufuliwe mwaka huu, nashauri watafutwe wafadhili wa ndani kufadhili shindano hili. Wafadhali ninaopendekeza ni pamoja na mabenki, kampuni za simu na kampuni binafsi za biashara kama vile MeTL, GSM, Bakhressa Group of Companies, na Civil Societies kama vile TLHRC, TLS, nk.

Nini wanaJF tufanye?
Kwa upande wetu wanaJF nashauri tupige kura za kuunga mkono na tutoe maoni kwenye huu uzi kwa wingi kadri itakavyowezekana. Uzi huu utatumika kama ushahidi wakati uongozi wa JF utakapoenda kuomba ufadhili kwa wahusika.

Wafadhili wanataka kuona mwitikio chanya wa wafadhiliwa. Kwa maana hiyo, nawaomba wanaJF wote tupige kura na tupigie debe suala la ufadhili ili mwaka huu tufufue shindano la stories of change hapa JF.

Nawasilisha.​
 
Yale mashindano yameka kitapeli sana mtu anaandika anapata uungwaji mkono mkubwa kuanzia watazamaji, wachangiaji unaona kabisa hili linafaa wao wanakuja kutoa watu wao Huko hata hawajulikani ndio wankuwa washindi. Vigezo vyao vilivyowekwa waz hawavifuati wanabuni vya siri ili kuwapa watu wao
 
Mkuu mbona vigezo viko wazi? Hayo unayosema ni sehemu tu ya vigezo na yanachukua asilimia ndogo. Majaji ndio wanatoa alama nyingi mkuu.
 
Mkuu mbona vigezo viko wazi? Hayo unayosema ni sehemu tu ya vigezo na yanachukua asilimia ndogo. Majaji ndio wanatoa alama nyingi mkuu.
sasa hizo alama hawasemi wanazingatia nini mashindano ya waz inatakiwa pia vigezo viwe wazi
 
sasa hizo alama hawasemi wanazingatia nini mashindano ya waz inatakiwa pia vigezo viwe wazi
Wanazingatia content za andiko lako na jinsi ulivyozidadavua mkuu. Na kwa kuwa watu wanaandika topics tofautitofauti, vigezo haviwezi kufanana.
 
Wanazingatia content za andiko lako na jinsi ulivyozidadavua mkuu. Na kwa kuwa watu wanaandika topics tofautitofauti, vigezo haviwezi kufanana.
Utapeli namna ya kupga hela tu watu wanapiga kur hapa una kura elfu kumi unaoongoza anakuja kushinda mwenye kura tano wewe uliona wapi??? inatakiwa vigezo vyote viwe wazi na majaji wao kura zao ziwe 10% tisini iwe JF Members
 
Mkuu kwenye mambo kama haya kuna kitu kinaitwa weight. Alama za majaji zinabeba weights kubwa kuliko alama za kura. Umenipata mkuu?
 
Umeandika uzi wako as if TCRA wameishaifungulia JF. Hujui kwamba hao wakitoa ufadhili kwenye shindano hilo, watakuwa wameshiriki directly kuipinga TCRA kwa kuifungia JF?
 
Umeandika uzi wako as if TCRA wameishaifungulia JF. Hujui kwamba hao wakitoa ufadhili kwenye shindano hilo, watakuwa wameshiriki directly kuipinga TCRA kwa kuifungia JF?
Muda wa kifungo uliisha tangu mwaka jana mkuu. Fuatilia vizuri kifungo kilianza lini na kumalizika lini. Wewe unadhani JF ilifungiwa milele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…