Kuna yule baharia alitaka kusababisha wenzake wafe kwa meli wakamtupa baharini akamezwa na samaki siku 3 halafu akatemwa kule alipotakiwa kwenda ambapo alikuwa hataki na aliagizwa na Mungu..[emoji1787][emoji1787]
Haikutosha vipi kwa mose ati alitawanya bahari waisraeli wakapita!.. nilipopenda zaidi ati shetani alienda mbinguni kuongea na Mungu ili amjaribu yule msela aliepewa mapunye mwili mzima,utajiri wake ukapotea,familia yake ikafa! How can it be wengine wafe kisa kujaribiwa kwa mtu mmoja!![emoji3]
Vipi kuhusu Israel ati alipigana na malaika usiku kucha mwisho wa siku malaika akaamua amtengue nyonga yakobo..[emoji1787] jamani kama ni kupima uwezo Mungu si anajua uwezo wa kila mtu Sasa vipi kutumiana malaika waje tupigane nao ngwara..??[emoji23]
Tuachane na yote ati Adam na Eva walipokula tunda Mungu alipokuja akaanza kuwauliza ati nani kawaambia wapo uchi baada ya kula tunda!.. wakati huohuo tunaambiwa Mungu anayajua yote mwanzo Hadi mwisho sasa alikasirika nini na wakati alikuwa anajua kila kitu!
Alimuumba shetani huku akijua ya kuwa atakuja msaliti..[emoji1787] what a movie..??