Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Hivo vitabu tunavoita vya wageni tuwaachie hao wageni na dini zao hata tuvijadili vipi we cant change a thing ndo imekua hivo na itaendelea hivo.
Wanaoamini wameshaamini kama wewe huamini umechagua unachoamini

Mimi naona kuna hichi kitabu kinachotuhusu wote iwe unakiamini au la tuwekeze nguvu kwenye kukijadili na ndio kitabu pekee ambacho kina nafasi ya kubadilishwa maudhui yake ili kitufurahishe sote

Kinaitwa KATIBA
 
Vitabu vya dini ni kanuni tu zilizotungwa na watu na si Mungu, zile ni hadithi zimetungwa ili kukandamiza watu au ku control watu wasifikirie zaidi na kukosa maendeleo. Angalia watu wanaondekeza sana dini, wengi wao ni wanafki, wachawi, wafuga majini. In short, dini ni usanii tu na ndiyo maana unaona siku hizi wamejaa wachungaji wa kila aina watumiao uchawi kurubuni waumini wao huku wakiwala uroda bila wenyewe kujijuwa.
 
Kwamba Mungu aliumba dunia na kila kilichomo (sawa) kisha akaumba mwanaume na kuumba mwanamke kwa kumtoa ubavu mmoja mwanaume (sawa).

Kisha hao wawili (Adam na Eva/Hawa) wakazaa watoto wawili (Kaini na Abeli) - (sawa).

Kisha Abeli akawa mfugaji na Kaini akawa mkulima (sawa). Lakini Mungu alipendezwa zaidi na sadaka za Abeli kuliko za Kaini (sawa). Kaini akamuua kaka yake kwa wivu (sawa).

Mungu akampa adhabu Kaini kwa kumfukuza bustanini awe anatanga tanga huku na huko duniani (sawa).

Kaini akamwambia Mungu kuwa akitangatanga watu atakaokutana nao watamuua (shida inaanza kuja hapa). Mungu akamwekea alama usoni ili walimwengu wasimuue (shida inaendelea). Kaini akaenda huko nchi ya Nodi mashariki mwa Eden.

Kisha kaini akalala na mkewe akamzaa mtoto aitwae Henoki. (Sio sawa).

Reference: Soma kitabu cha Mwanzo 4:1-17.

Hii story haija balance kabisa hasa hapo mwishoni. Kama Mungu aliumba Adam na Hawa na wakazaa watoto wawili tu ina maana duniani palikuwa na watu wanne tu. Je hao watu aliokuwa akiwaogopa Kaini ni akina nani? Je huyo mwanamke alielala na Kaini na kuzaa nae mtoto alitoka wapi?

Wataalamu hebu naomba mtusaidie hapa.

Labda jibu liko hapa:

Kaini na ndugu yake Abeli walikuwa wa kwanza kati ya watoto kadhaa waliozaliwa na Hawa. (Mwanzo 4:1, 2) Kaini alipofukuzwa kwa kumuua ndugu yake, alilalamika hivi: “Yeyote atakayenikuta ataniua.” (Mwanzo 4:14) Kaini alikuwa akiogopa nani? Biblia inasema kwamba Adamu “akazaa wana na mabinti.” (Mwanzo 5:4) Ni wazi kwamba wazao hao wengine wa Adamu na Hawa wangeweza kumshambulia Kaini.

Soma zaidi hapa:
 
Quran tu ndo kitabu pekee kinachoeleweka na hakina shaka kabisa.
Kurokana na Lugha iliyotumika Quran inasomwa na Waislamu wenyewe kwa asilimia 99 tofauti biblia ambayo imekuja kwa kila Lugha kila ya taifa kiasi imewapa wengi kuijua kwa kuisoma ata wewe, ni ngumu kuonyesha madhaifu ya kitabu chako kitakatifu unachokiamini.
 
Kwa nini unasema kuashiria liliwahi kutokea na sia kuashiria linalokwenda kutokea??
Yes naamini 100% mkuu,kamuulize yule mmarekani Neil Armstrong au Edwin waliona nyufa kubwa huko mwezini kuashiria kuna Jambo liliwahitokea walipotembelea mwaka 1969
 
Ngano ni hadithi fupi inayosimuliwa kwa kusudi la burudani na pia mafundisho.Ni mambo ambayo hayajawahi kutokea kuhalisia.Ukitafakari kwa kina utagundua sehemu kubwa ya dini nyingi zimejengwa katika msingi huu.

Story gani ujawahi kuiamini kama ni ya kweli na halisi katika kitabu cha dini YAKO?
Naomba uniwekee story mbili tu kisha uthibitishe ya kuwa hizo ni ngano ? Yaani uweke na ushahidi.
 
Vitabu vya dini ukitumia logic, HUTOBOI. Maana kuna vingine havimake sense kabisa. Kufika mbinguni kazi sana.

Kuna muda unasoma unaona kabisa hii chai sasa, hasa yule mwamba aliyemezwa na samaki siku 3. Kwamba alikuwa tumboni amekaa tu. Sijui anapumuaje huko tumboni.

Mungu kama unatusikia tusamehe tu baadhi yetu
Naomba unipe misingi ya Logic kwayi inakufanya iwe mizani ya kupima usahihi wa mambo.

Unaijua lakini "Logic" ni nino au umesikia tu kwa watu wakisema "logic" ?
 
Wataalam eti wanasema...inawezekana Adam alipata watoto wengine zaidi ya Kaini, abeli na Seth ambao watakuwa wa kike. Means kaini alizaa na dada yake.
Zamani wanawake walikuwa hawatambuliki hata kuandikwa kwenye vitabu
Walikua hawatambuliki wala kuandikwa..mbona waliwatambua hao akina eva..sara..na wengine acha upompoma tumia lojiki kuhoji sio uduwanzi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliandikwa wachache.
Hata amri za mungu zinawahusu wanaume..kuna ile 'usizini'. Niliwahi ambiwa hapa jf kuwa mwanaume ndo anazini na si mwanamke.
Kuna nyingine inasema usitamani mwanamke/mke wa mwenzio ina maana kutamani mume wa mwenzio ni ruksa
we Mwanamke wewe nitamani mimi basi
 
Kuna muda unasoma unaona kabisa hii chai sasa, hasa yule mwamba aliyemezwa na samaki siku 3. Kwamba alikuwa tumboni amekaa tu. Sijui anapumuaje huko tumboni.
Sasa chai hapo iko wapi ? Kwani kitu hakiwezi kuwa hai ndani ya kitu kingine ?

Lakini habari ya kumezwa na Samaki Chewa ni habari ya haki na huu ni katika muujiza.

Allah mtukufu anasema :


139. Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.

140. Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.

141. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.

142. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.

143. Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,

144. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.

145. Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.

146. Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.

147. Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.

148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda. (as-Saffat : 139 - 148)
 
Back
Top Bottom