Story : Jamaa wa pool table alivyowaingiza 18 wadau team jobless

Story : Jamaa wa pool table alivyowaingiza 18 wadau team jobless

Kmmmke 😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
Unakuta game ya mwisho hyo ya laki na 20 hata wale wadhamini walistuka maninaaa unakuta jamaa anapaka poda mikononi hapo ndo unajua hiki cha kike...

Eeeh ikawaje mkuu
Mwanangu na mie Leo Kuna bibie kanipuna kimasikhara tu nilimuona zoba kumbe sio πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna mahali alikuja kijana mmoja mgeni akakuta wenyeji akauliza hakuna mchezaji tucheze bukubuku mwenyeji mmoja akasema labda buku mbili mbili jamaa akasema sawa

Wanacheza mgeni akaliwa game 5 mgeni akasema twende ten ten mgeni akaliwa game 3 ikawa jumla kaliwa 40000 mgeni akasema twende laki mwenyeji hakua na pesa ila kwa uchezaji wa mgeni mwenyeji alipata wadhamini ikafika laki na 20 mgeni akamuambia twende yote mwenyej akakubali mgeni alivyo shika stik game liliisha na ela zikaondoka
Siku hizi betting kwa kucheza pool table imekuwa kawaida sana sijui tatizo ni nini.
 
Hili tukio nadhan lilitokea mkoa kagera hili wilaya biharamulo miaka miwili kama si mi3 toka litokee ilikuwa mida ya moja usku..
 
Nakubaliana na mleta mada mimi miaka ya 2000 ilikuwa haipiti siku lazima nicheze ingawa nilikuwa average sikuwa pro.

Sasa wale ma wanakuwa na madalali wao wanazunguka kwenda kuangalia wapi wanapenda kucheza kamali na hii kama ni dar basi dar yote.

Kwa hiyo akipigiwa simu anafika na enzi zile ukiona mtu amefika na fimbo yake unashtuka unajua huyu sio wa kawaida.

Kiufupi mkiwa wenyeji akatokea mgeni anapanda dau ni wa kukaa mbali nae.
 
Back
Top Bottom