Story kutoka kwa WATU: Maisha yanachangamoto kweli

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
"Maisha yana changamoto nyingi sana.

Nakumbuka mwaka 2019 Nilihamia kwenye nyumba moja huko kilakala. Hiyo siku nafika tu pale, nikamkuta mpangaji mwenzangu na akaniambia hapa ni jau yeye mwenyewe ana mipango ya kuhama sababu mzee mwenye nyumba ni chuma ulete. Nikapuuzia.

Nikaendelea kuishi pia na majirani wakawa wanasema maneno hayo hayo, nikawa napuuzia maneno yao.

Niliishi pale vizuri tuu ila nikawa nawekeza pesa zangu kwenye kibubu kila siku nikienda kazini nikirudi na elfu 40 basi natia 20 kwenye kibubu na nikipata 10 naweka 5. Yaani hela ndogo kuweka kwenye kibubu ni 2000 na malengo yangu nikanunue pikipiki.

Eeeh baada ya miezi nane kupita nikasema nivunje kibubu, nilichokiona kwenye kibubu nilikuta 27000 tu.

Sikupiga mahesabu wakati naweka ila nilichokuwa nategemea hata nikute hata milioni moja, yaani sitasahau halafu mzee alipogundua kuwa nimemstukia kuwa yeye ni chuma ulete akanitumia barua nihame kodi yangu ikiisha.

Kweli nilikua siamini kama kuna chuma ulete kuanzia hapo, nikaamini maana walikua wanaishi na mkewe na hawana kazi yoyote na wanakula milo yote mitatu tena saafi.

Sitakaa nisahau yule mzee alinirudisha nyuma sanaaa".
G Man, Dar.
WatuNiStory
 
Haya mambo huwa siyaamin sana,labda mpaka siku yatakaponitokea
 
Enhe ikawaje??? Kabla hujaendelea Mwambie Abdallah aniletee Kahawa Na kashata mbili apo ndo tuendelee Na story...
 
"Maisha yana changamoto nyingi sana.

Nakumbuka mwaka 2019 Nilihamia kwenye nyumba moja huko kilakala. Hiyo siku nafika tu pale, nikamkuta mpangaji mwenzangu na akaniambia hapa ni jau yeye mwenyewe ana mipango ya kuhama sababu mzee mwenye nyumba ni chuma ulete. Nikapuuzia.

Nikaendelea kuishi pia na majirani wakawa wanasema maneno hayo hayo, nikawa napuuzia maneno yao.

Niliishi pale vizuri tuu ila nikawa nawekeza pesa zangu kwenye kibubu kila siku nikienda kazini nikirudi na elfu 40 basi natia 20 kwenye kibubu na nikipata 10 naweka 5. Yaani hela ndogo kuweka kwenye kibubu ni 2000 na malengo yangu nikanunue pikipiki.

Eeeh baada ya miezi nane kupita nikasema nivunje kibubu, nilichokiona kwenye kibubu nilikuta 27000 tu.

Sikupiga mahesabu wakati naweka ila nilichokuwa nategemea hata nikute hata milioni moja, yaani sitasahau halafu mzee alipogundua kuwa nimemstukia kuwa yeye ni chuma ulete akanitumia barua nihame kodi yangu ikiisha.

Kweli nilikua siamini kama kuna chuma ulete kuanzia hapo, nikaamini maana walikua wanaishi na mkewe na hawana kazi yoyote na wanakula milo yote mitatu tena saafi.

Sitakaa nisahau yule mzee alinirudisha nyuma sanaaa".
G Man, Dar.
WatuNiStory
Wewe unaweka hela bila kuhesabu, halafu unamsingizia mzee chuma ulete?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kweli Kiranga aisee
Mkuu, weka hela benki, achana na habari za kibubu.

Tena tafuta benki inayoweza kukupa taarifa za hela zako hata kwenye simu.

Hii si karne ya kibubu.

Unaweza kukuta hela zimeliwa na panya ukalia mwenyewe.
 
Kuna dogo mmoja anafanya biashara sasa utakuta amerudi na pesa za sarafu kama 30 na anapeleka hesa kwa bosi wake kila baada ya wiki , kwa hiyo unaweza kut amepeleka salafu kama 200000 pale dukani anapoleka hela makondacta wa daladala wanakuja kuomba chenchi siku moja walijikuta kama 1000000 haijulikani ilipo baada ya tukio lile wakapiga marufuku kutoa chenchi wakaaambia madogo wapeleke not waachane na salafu
 
Mkuu, weka hela benki, achana na habari za kibubu.

Tena tafuta benki inayoweza kukupa taarifa la hela zako hata kwenye simu.

Hii si karne ya kibubu.

Unaweza kukuta hela zimeliwa na oanya ukalia mwenyewe.
Asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom