Story ya kusisimua kuhusu Jaymoe na Langa

Story ya kusisimua kuhusu Jaymoe na Langa

Siyo jana wala juzi, nafanya makamuzi
Niite mwana harakati, au mwana mapinduzi
Mistari yangu haikauki kama vile shahawa
Mistari yangu ina soko kuliko biashara ya madawa
Mi siyo Michael sinywi Guinness,
Ila nina power, mikocheni block 41 mi ni mzawa
-------------
Kuna mstari mmoja kama naukumbuka vizuri anasema........

Elimu dunia, kidogo elimu akhera
Nipo so high hunifikii hata kwa antena😂😂😂😂
 
Langa dah mtoto wakitaaa kabisa ,Adventure ,geza ulole ,na king'oko zinaliwa tu bangeeee .jamaa wa kishua kimtindo

Naona kama juzi tu kumbe miaka kibao imepita
 
Story ya Jaymoe na Langa iko hivi kwenye wimbo ya Jipange wa Jaymoe , Kuna mstari jay moe anasema

" Amani kwa kaka voda milionea/ Wastue wadogo zako waache poda wale mmea/

Hapa alikua akijaribu kumkumbusha Kaka voda awastue kina langa kua Unga sio mzuri

Langa Ni kama alipanic akaja kujibu

Amani kwa kaka voda milionea/ mwambie moe aache ushoga na umbea/

Kupitia hii line Jaymoe alihuzunika sana kwanini anajaribu kuwakumbusha kina langa kuacha matumizi ya unga ila anatukanwa, Haikuishia hapo

Baada ya Langa kuja kustuka kuwa madawa yanamuharibia akaanza kujirudi akatoa project kadhaa na zikafanya vizuri tuu

Mfano Am supplying & Rafiki wa kweli na Kifo jela ah taasisi

Sasa kipindi langa anajitafuta kurudi mainstream baada ya kutoa Am supplying , Kipindi anafanya ngoma ya Rafiki wa kweli ,iliyofanyiwa production na P funk majani,akawa anataka kwenye hii ngoma ya Rafiki wa kweli amshirikishe Jay moe , Lengo ilikua ni kuwaonyesha watu kuwa yeye na Moe hawana matatizo

Alivomtafuta jaymoe ikashindikana coz jaymoe alikua bado ana hasira kwann Langa alimtukana kwenye ile line ya

"Amani kwa kaka voda milionea/ Mwambie moe aache ushoga na umbeya"

Bhas ikabidi langa akomae mwenyewe ngoma nzima ,na ilivotoka ilifanya vizuri sana,

Ikabidi Langa kwenye Ngoma ya Kifo,Jela au taasisi aliweke sawa hilo swala

Kuna line anasema

"Amani kwa kaka voda milionea/ Mwambie Moe sili poda wala mmea/

Tukirudi kwa Jay moe, anakiri alivopata habari kuwa Langa amefariki, Alilia sana, na sababu kuu iliyomfanya Moe akalia ni kwamba kipindi Langa yuko hai alijaribu kumtafuta moe mara kadhaa ili wamalize tofauti zao ,ikiwa ni pamoja na kushirikishwa kwenye wimbo wa Rafiki wa kweli ila kiburi chake kikapelekea mpaka Langa anafariki hawaja maliza tofauti zao

Moe anasema hiki kitu kinamuuma sana.


Moja ya line kali nnazozikubali kutoka kwa the late langa ni

Wananichekea usoni kisogoni wananisema/
Wanatafuta mabaya wanajifanya hawaoni mema/

Rest in peace Lyrical And Naturally Gifted African (LANGA)
Umejitahidi kuandika ila RAFIKI wa kweli ndio wimbo wa mwisho marehemu kuutoa akiwa hai ama ulitolewa na mgt yake dk za mwisho kabla hajafa,
 
Katika nyimbo zote

RAFIKI wa KWELI na MATAWI YA JUU ndio ngoma bora sana kwa upande wangu.

Hiyo rafiki wa kweli nimependa sana pale aliposema NITAKUSAKA URAIANI kama NYOKA wa KIJANI.
 
Nakumbuka tuko shule Arusha, bro wangu na wenzake wa madarasa ya juu walikuwa wanamuita LANGA awachanie mistari ya kina Redman 🤣🤣🤣​
 
Back
Top Bottom