Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
SIKU YA KWANZA
Mimi: Oya inakuwaje? Mbona leo umechelewa hivyo?
Anita: Usafiri ulikuwa shida kweli yaani, nilisubiri gari mpaka nikakoma, yalikuwa yakipita tu.
Mimi: Pole sana, kwa hiyo inakuwaje leo?
Anita: Nakusikiliza wewe tu, ukiniambia nije kwenu, nakuja, ukiniambia tuonane sehemu yoyote, nakuja.
Mimi: Kweli jamani?
Anita: Huamini?
Mimi: Mmmh! Aya, nitakujulisha, nasubiri ticha atoke klasi kwanza ili nichaji simu, nitakucheki, namba yako si ileile?
Anita: Ndiyo! Ileile, sijabadilisha.
Mimi: Poa...ila naona ticha anazingua sana aiseee...
Anita: Hata mimi naona hivyohivyo...kwanza imekuwaje mpaka kuanza kuchati na mimi, kitambo.
Mimi: Basi tu, nimemisi kuchati na wewe jamani!
Anita: Mh! Aya!
Hizo zilikuwa chatting fulani nilikuwa nachati na mrembo wa darasa anayeitwa Anita. Hatukuwa tukitumia simu, meseji zetu hizo tulikuwa tukiandikiana kwa kutumia vikaratasi, yaani mimi naandika, nampa mshikaji wangu aliyekuwa pembeni, anampa Anita, halafu ananijibu tena.
Yaani tulikuwa kama watoto ila ndiyo hivyo mambo yalikuwa yakisonga. Umeme ulizingua, ulikatika halafu simu haikuwa na chaji, ticha yupo klasi, so kuwasiliana tukawa tunawasiliana kwa vimeseji tu, siyo mimi peke yangu, yaani hata madenti wengine ilikuwa hivyohivyo, kwa kifupi, tulizoea kufanya hivyo.
Anita alikuwa manzi fulani hivi, mtoto mzuri, mtoto wa haja, alijazia kweli huku nyuma, macho yake yalikuwa mazitoooo...kulikuwa na mademu wengi kwa klasi, ila Anita, alikuwa babโkubwa. Wanaume hapo klasi walimtaka sana, ila walipomwambia, mtoto akajishembeduashembedua, akawapiga masela vya mbavu hivyo wakaachana naye.
Anita alikuwa biashara nzuri sana, klasi, tulikuwa na katabia kamoja hivi, yaani anakuja mtu, tunamwambia demu fulani huwezi kumchukua, akisema anaweza, tunawekeana dau halafu anakwenda, tunampa muda, kama wiki mbili hivi awe amefanikiwa. Dau linategemea, labda laki moja kwa laki moja, halafu mtu anakwenda.
Sasa watu walishaliwa sana hela zao kwa Anita, kila mtu aliyetaka kula hela, anakwambia nenda kamchukue Anita, anakupa wiki mbili, ukichemka, basi umeliwa. Kalikuwa kamchezo fโlani amazing, na nilishawala watu hela zao, waliniambia niende nikamchukue Rachel, wakanipa wiki mbili, yaani wiki moja tu, nilikuwa naye chumbani, nikawala hela yao.
Hawakuishia hapo, kuna mdada aliitwa Fatuma, wakabisha kwamba siwezi kumchukua eti kwa sababu Cosmas alimshindwa, Eduardo alimshindwa, nikawaambia tuweke hela, tukaweka, nikawala kwani ndani ya siku nne, Fatuma akawa oyaoya.
Sasa kaupinzani kalikuwa kwa huyu Anita, watu walichemka sana, walimfuata kwa mikwara lakini hawakufanikiwa, ikawa ukitaka kuliwa hela yako, sema unamfuata Anita, lazima uliwe kwani alikuwa mgumu mno mpaka watu kuhisi kwamba labda mtoto alikuwa silidi.
Mimi: Ila tatizo lako unazingua sana....
Anita: Nani? Mimi? Akuu..wala sizingui.
Mimi: Kwa hiyo leo uhakika?
Anita: Wewe tu.
Unajua Anita alikuwa mzinguaji sana, kukubaliana naye lilikuwa jambo dogo lakini kwenye utekelezaji ndiyo ilikuwa shughuli. Omari aliwahi kumfuata, mtoto akalegea, akamrembulia macho sana jamaa, akajipa uhakika kwamba atakula mzigo na hela zetu, kilichotokea, wiki mbili zikakatika, hakuna kitu.
Mimi si ndiyo mbishi wao, nikaona mbona simpo tu, yaani Anita anishinde? Ana nini? Kama niliwahi kuwachukua wengine, yeye atanishindaje? Nikapiga moyo konde, nikaweka dau la shilingi laki mbili, watu watano wakajitokeza, nao wakaweka laki mbilimbili, nikaona poa, nikapewa wiki mbili niwe nimemaliza, nikasema sawa.
Tukachati sana kwa vikaratasi, baada ya ticha kutoka, nikachaji simu harakaharaka ili baadaye nianze kuchati naye kwenye simu.
Ngoja nikwambie kitu, watu hawakunielewa, nilikuwa mjanja sana, watu walipokuwa wakimfuata, walimfuata waziwazi ili kututisha tulioweka dau, sasa walipokuwa wakishindwa, tulijua mapema kwamba walishindwa ila kwangu, nilitaka kumfuata kimyakimya, yaani ukifuatilia, hujui kama mimi na yeye tuilikuwa tunachati.
Mimi: Leo una ratiba gani?
Anita: Saa ngapi?
Mimi: Mbili usiku.
Anita: Mmh! Nitakuwa home tu, kuna kitu?
Mimi: Ndiyo! Nataka nikupeleke sehemu fulani hivi!
Anita: Wapi?
Mimi: Surpriseeee...
Anita: Sawa.
Mbele yangu niliona mafanikio kwa kudhani kwamba kila kitu kingekwenda poa. Nikajiona Sharukh Khan kwamba hakukuwa na demu yeyote ambaye angenikataa, mtoto alikubali kutoka nami out...kuna nini tena!
Kumbuka hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kabisa, tulipotoka chuo, nikaelekea nyumbani, sikutaka kuchati naye sana, nikamuweka kiporo kwanza. Watu walikuwa wakisikilizia tu, walisubiri siku 14 ziishe ili wachukue hela zao, si unajua Anita ndiye alikuwa mgumu wa darasa.
Ilipofika saa moja na nusu usiku, nikamcheki kwa simu, kwanza ikaita weeee, alipokuja kuipokea, swali la kwanza kuniuliza, eti โWewe nani?โ
Mimi: Unasemaje?
Anita: Naongea na nani?
Mimi: Jamani Anita...kweli namba yangu haukuwa nayo, uliifuata au unanifanyia kusudi tu?
Anita: Wewe nani?
Mimi: Naitwa Chilo.
Anita: Hahaha! Kumbe wewe..niambie sasa.
Mimi: Poa! Upo wapi?
Anita: Nipo nyumbani! Kuna nini?
Mimi: Kwani tulizungumza nini chuoni kwenye vikaratasi?
Anita: Nimesahau, hebu nikumbushe.
Sikiliza mshikaji wangu, Anita hakusahau, kwanza alijua anazungumza na nani ila alishajua kwamba namtaka hivyo akahakikisha kwamba ananisumbua na mwisho wa siku nisipate kitu kama ilivyokuwa kwa wana wengine.
Kumpata halikuwa tatizo, nilitaka kumfanyia mambo ambayo hakutegemea ili mwisho wa siku achukuliwe kiulaini kabisa, nilichokifanya ni kuwaandaa washikaji zangu wa kitaa, kama wanne hivi na mademu wawili, hao walikuwa kwa kazi maalumu ambayo ingenifanya nimchukue Anita.
Mimi: Nataka nije nikutoe out bwana...
Anita: Oooh..kumbeeee...naomba tufanye siku nyingine, leo nimechoka.
Mimi: Kuchoka si tatizo Anita, huku huji kukimbia wala kufanya kazi, nitakufuata kwa usafiri wangu, hivyo hautochoka kihivyo...make me happy bhanaa....
Anita: Chilo! Try to understand!
Mimi: Sawa.
Kulikuwa na kaugumu ila kila nilipokumbuka milioni moja iliyowekwa mezani, nilipagawa na kujitolea kwa nguvu zote. Siku hiyo, mshindi alikuwa yeye, nikakubaliana naye, hivyo nikaendelea kufanya yangu huku moyo ukiwa unauma kweli, wakati mwingine nilijuta kwa nini niliweka laki mbili zangu mezani.
Washikaji wakawa wananipigia simu na kuniuliza, ilikuwaje? Nimefanikisha? Nitamuweza? Sikutaka kuwajibu, mi nikatulia zangu na hata simu sikutaka kupokea, nikaona jibu zuri kuwajibu ni kuniona nikiwa nimemchukua huyu mtoto na kuendelea na watoto wengine ambao walinipa.
Je, nini kitaendelea?