Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
- Thread starter
- #21
Sehemu ya tatu tayariWapi stori jamani, lete nyunyuzi mkuu.
T[emoji769]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sehemu ya tatu tayariWapi stori jamani, lete nyunyuzi mkuu.
T[emoji769]
Duh! Hatari. Lete stori kijana, inanifanya nibaki kucheka tu.CLASS CHATTING - 03.
SIKU YA TATU
Niliamka asubuhi na mapema, nikajiandaa na kuanza kuelekea chuoni kama kawaida. Kichwa changu kilimuwaza sana Anita na kuona kwamba muda wowote ule basi ningeweza kuchukua mzigo, nikawa nao na lile dau lililokuwa kwa washikaji basi ningelichukua.
Wakati nikiwa njiani, tena nikiwa nimepita njia ya kwao kabisa, nikamuona akiwa kituoni, nilichokifanya ni kusogea na kisha kupiga honi, alipoliona gari langu, mbona haraka sana akalifuata.
Mimi: Karibu...
Anita: Asante..
Akajiweka kitini. Siku hiyo alivalia kisketi chake kifupi, alipokaa tu, basi ikapanda juu, mapaja yakawa nje, mtu mzima midadi ikanipanda, nikaona kwa nini nisilegeze moyo tu! Ila nikahofia kwa kuona kama utakuwa umejirahisisha kwa kumwambia fastafasta angeanza pozi zake, nilimfahamu vilivyo Anita.
Anita: Bado una hasira na mimi?
Mimi: Kiduchu tu...ila una vipozi f’lani visivyokuwa na msingi...
Anita: Jamani nisameheeee mwenzio, unakuwa na hasira mpaka naogopa.
Mimi: Nikwambie kitu Anita?
Anita: niambie (Akajiweka sawa kitini)
Mimi: Huwa ninajitambua, nina vijihasira flani hivi, ukinizingua, nakuzingua, halafu sipendi kupotezewa muda, ukinipotezea muda, nakuchukia, halafu huyo nasepa zangu....
Anita: Basi naomba unisamehe....
Mimi: Usijali...
Tulikuwa tukipiga vistori tu, kila wakati kazi yake kubwa ilikuwa ni kubadilisha vimikao tu pale kitini, mara akunje nne, mara akibinue kikalio chake, mara apandishe miguu mpaka kwenye dashbodi, yaani kwa kifupi, mtu mzima nilikuwa nategwategwa.
Anita: Nashukuru...
Aliniambia baada ya kufika chuoni, akateremka, sikutaka kuteremka, yaani sikutaka kuonekana naye ili niwape uhakika wale marafiki zangu kwa kuona kwamba labda wangeweza kushinda wale hela yangu.
Akateremka na mimi kuondoka na gari hapo, hata sehemu ya kuegesha gari langu nilibadilisha. Siku hiyo, mwenyewe akawa ananitumia meseji tu kwenye simu, nikaona si mbaya kama nikichati naye...hivyohivyo..
Anita: Leo nina furaha sana....
Mimi: Ya nini tena?
Anita: Kunisamehe....
Mimi: Usijali basi, una nafasi leo?
Anita: Nafasi ya nini?
Mimi: Ushaanza.....
Anita: Jamani si ndiyo nauliza....sasa nitasema nina nafasi na wakati sijajua ya nini!
Mimi: Nataka nikutoe out...sehemu fulani hivi...
Anita: Kule pa siku ile uliposema ungenitoa?
Mimi: Yaap...upo tayari?
Anita: Saa ngapi?
Mimi: Mbili usiku...
Anita: Sawa...
Basi ndiyo hivyo, kwa klasi, kama kawaida yangu sikutaka kujionyesha, mwenyewe nilikuwa bize na mambo yangu na hata washikaji hawakujua kama kweli mtoto nilikuwa naye beneti.
Nilichokuwa nikiwafanya ni kama daktari, yaani wao walikuwa wagonjwa na kila wakati nilikuwa nikiwapa moyo kwamba watapona lakini ukweli ni kwamba wangekufa.
Nilishaona dalilii kwamba Anita alipagawa kwangu, hivyo mimi ndiye niliyetakiwa kufanikisha mpango mzima. Nilichokifanya, kama kawaida yangu nilikuwa kimya, kama sikupenda kuona kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake, tukaondoka chuo huku masela wakiniuliza tu, vipi? Utaweza? Utamla? Mbona hatuoni hata dalili? Au umeshindwa? Kila wavyotuma meseji zao, niliwalia doro.
Ilipofika saa moja, harakaharaka nikamcheki kwenye simu, nilitaka nijue kwanza kama itawezekana au la.
Mimi: Inakuwaje sasa?
Anita: Poa...
Mimi: Upo wapi?
Anita: Kwa mama mdogo...
Mimi: Wapi?
Anita: Mabibo...
Mimi: Mmh! Nitaweza kukuona kweli?
Anita: Kwa leo...sidhani, naomba tufanye siku nyingine.
Kwanza nikanywea, sikuamini kama kweli siku hiyo napo nilitakiwa kukosa utamu...huyu Anita alitaka kunizingua tu, yaani alikuwa akiingia na kutoka, nilimmaindi sana lakini sikuwa na jinsi, nilichokifanya ni kumpigia simu, nikamuuliza tena kwamba itawezekana kuonana lakini jibu lake eti likawa lilelile kwamba isingewezakana.
Mimi: Hivi kweli itashindikana jamani?
Anita: ndiyo! Haraka ya nini Chilo? Tufanye hata siku nyingine.
Sikutaka kuendelea kufuatilia, nilichokifanya ni kuichukua namba yake na kuiandika sehemu kisha nikafungua mtandao mmoja na kuiingiza namba yake, mtandao ambao uuliunganishwa na GPS kujua mahali alipokuwa.
Sehemu ya kuingiza namba, nikaingiza namba yake kisha kubonyeza sehemu iliyoandikwa GPS Locator...baada ya hapo, ikatokea ramani ya dunia, ikaanza kuitafuta namba yake, ikavutwa Tanzania, Dar es Salaam na mwisho wa siku kuonyesha kwamba namba yake ilikuwa sehemu iitwayo Tandale, yaani mtaa uleule nilipokuwa, nikapata uhakika kwamba hakuwa Mabibo kama alivyosema, alikuwa akinidanganya.....hasira zikanipanda.
Nikaanza kumtafuta kwenye simu kihasirahasira....
*****
Sikutaka kumchelewesha, hapohapo nikampigia simu, tena nilionekana kukasirika haswaaa, haiwezekani msichana aniletee zake za kuleta, yaani ajione yeye mjanja hata zaidi yangu. Simu haikuita sana, ikapokelewa.
Mimi: Wewe Anita.
Anita: Abee.
Mimi: Mbona unanifanyia makusudi sana?
Anita: Makusudi ya nini tena?
Mimi: Unataka kuonana nami au hautaki?
Anita: Ninataka ila nipo mbali na nyumbani.
Mimi: hivi unanifanya mimi mtoto?
Anita: Kwa nini tena jamani?
Mimi: Nisikilize, umeniambia upo Mabibo, unaidanganya na wakati upo kwenu.
Anita: Nani kakudanganya, nipo Mabibo, haki ya Mungu tena.
Mimi: hebu niondolee ujinga wako! Hivi internet inaongopaga? Toka lini ukaona kifaa cha mzungu kinadanganya! Upo nyumbani kwenu ila umeamua kunizingua, sasa sikiliza......
Anita: Chilo...
Mimi: Nini?
Anita: Nani kakudanganya nipo home?
Mimi: Unabisha?
Anita: Sipo nyumbani, kweli tena.
Mimi: Sasa nimeshafika kwenu, naingia ndani halafu nakuulizia, nataka niamini.
Anita: Chilo, usifanye hivyo, baba yupo.
Mimi: Baba yako hayupo, ametoka, nimepishana naye njiani.
Anita: Haki ya Mungu tena, yupo.
Mimi: Umejuaje kama yupo na wakati upo Mabibo? Mimi niliyekuwa Tandale nimekwambia hayupo, wewe uliyekuwa Mabibo umesema yupo, umejuaje?
Kimyaaaa...
Unajua mi ndo maana sometimes naona watoto wa kike wanazingua tu. Yaani ishu ya kuonana nami aliifanya iwe complicated kinoma na wakati ilikuwa ishu ya kawaida tena ya mara moja kabisa.
Kweli nikasepa nyumbani na kuelekea kwao, nilitaka nimuhakikishie kwamba alikuwa muongo. Nilipofika kwao, haikuwa ishu kuingia ndani japokuwa kulikuwa na mlinzi, nikazama zangu ndani kwani mlinzi alinizoea, si unajua mshikaji wa kitaa.
Nilipofika ndani tu, nikakutana na dada wa kazi. Kwanza, dizaini fulani akashtuka, hakuamini mimi kuwa pale muda ule.
Mimi: Hujambo Zubeda?
Zubeda: Sijambo! Shikamoo.
Mimi: Poa tu. Anita yupo?
Zubeda: Yupo, nikakuitie?
Mimi: Ndiyo! Kwani hakutoka?
Zubeda: Hakutoka, yupo ndani, ngoja nikamuite.
Nilitaka kushangaa bhana, inakuwaje Mzungu awe muongo, GPS ilionyesha kwamba alikuwa kitaa kwao kasizi, sasa aniambie yupo Mabibo, wapi na wapi. Baada ya muda, huku akionekana kuwa na aibu, Anita huyo akatoka nje, nilipomuona, sikufichi msela wangu, nilishikwa na hasira.
Anita: Naomba unisamehe...
Mimi: Wewe mpumbavu kweli Anita...yaani wewe mpumbavu sana....
Sikutaka kuongea zaidi, nilichokifanya, nikageuka kama mwanajeshi, kisha huyo nikasepa zangu. Sipendi kukuficha, napenda kuwa mkweli tu, yaani siku hiyo nilikasirika sana, sikutaka kumuona Anita tena kwani alinifanya mimi mtoto na wakati nilikuwa mtu mzima.
Usiku huohuo, mtoto akaanza kutuma meseji za samahani, yaani kila iliyoingia, ilikuwa na samahani kubwaaaa, sikujali, sikumjibu meseji zake, nilibaki kimya huku nimetulia tu, kila nilipokuwa namfikiria, alinikasirisha zaidi.
Anita: Naomba unisamehe Chilo wangu.
Kimyaaaaa
Anita: Naomba unisamehe jamani sitorudia tena....
Kimyaaaaa
Anita: Najua nimekukosea, sikutakiwa kukudanganya Chilo, ila nimefanya hivyo kwa kuwa bado naogopa, sijiamini kabisa, naomba unisamehe...
Kimyaaaaa
Sikutaka kujibu meseji yake yoyote ile, niliamua kwa nia moja kwamba ni lazima nifanye kama mwanaume mwenye msimamo, mtoto wa kike ni mtu wa kawaida sana na sometimes ni lazima ajue kwamba kuna wanaume wenye misimamo migumu ambayo haikuweza kuyumbishwa na kitu chochote kile.
Unapojifanya mlegevu kwa msichana, ni lazima utasumbuka sana, ni lazima uwe na msimamo kwani baadhi ya wanawake wengine, wanapenda wanaume wenye misimamo, wanaosimama kama wanaume na si wale wanaobadilikabadilika kama kinyonga.
Anita aliniomba sana msamaha lakini wala sikuwa na muda, sikutaka kumjibu meseji yake yoyote ile, niliuchuna kama sikuziona meseji zake. Naye hakuacha, yaani ni kama aliambia kwamba akiendelea kutuma mesji basi ningelainika kumbe si hivyo, ninaposema kwamba nimekasirika, huwa ninakasirika kweli na sitaki ujinga kabisa.
Anita: Japokuwa hutaki kunijibu, nakutakia usiku mwema.
Kimyaaaa....
Je, nini kitaendelea?
Sehemu ya 04 tayariDuh! Hatari. Lete stori kijana, inanifanya nibaki kucheka tu.
T[emoji769]
Uliamua kumkazia sana, kijana anaejielewa huwa hataki shobo.Sehemu ya 04 tayari
Sehemu ya 5 inakuja hiyooooooooooooooooooUliamua kumkazia sana, kijana anaejielewa huwa hataki shobo.
T[emoji769]
Stimu imekata ghafla dah!CLASS CHATTING - 05
SIKU YA TANO
Kama kawaida yangu nikaamka asubuhi. Siku hiyo sikutaka kwenda chuoni, sikujisikia vizuri hivyo nikaamua kupumzika nyumbani. Washikaji zangu, masela wa kweli wakaanza kunitafuta kwenye simu, Chilo upo wapi? Unafanya nini? Wahi chuo, leo mtoto Anita katokelezea kinoma, mtoto anang’aa kinoma, wahi uje umuone, naona kama ana haraka fulani hivi’
Nilitumiwa meseji hizo na washikaji, sikuwa na muda, nilikuwa hoi kitandani. Sikutaka kumcheki kwa hewa huyo Anita wao, nilimpotezea lakini upande wa pili nilijua tu kuna siku angenasa, mimi si ndiyo mzee wa mitego bwana.
Basi ilipofika saa tatu na nusu, kimeseji hicho, nikaulizwa nilikuwa wapi, meseji haikutoka kwa mtu mwingine bali Anita.
Mimi: Nyumbani.
Anita: Huji chuo.
Mimi: Kufanya nini?
Anita: kusoma.
Mimi: Siji.
Anita: Kwa nini?
Mimi: Naumwa...
Anita: Jamani pole sana mpenzi...tatizo nini?
Mimi: Nasumbuliwa na kichwa, hilo tu....
Anita: Naomba kitu.
Mimi: kipi?
Anita: nije nikuone jamani!
Unafikiri nilikataa basi, nikakubali, nikamwambia njoo. Muda ukazidi kwenda mbele, nikaona kama mtu mwenyewe anakuja kuniona, basi ilibidi nitengeneze mazingira mazuri, yaani kama ni kule Tandale kwa kina Nyemo, basi ningekwenda kuazima mashuka, air freshner na mambo mengine, si unajua kidogo uonekane supasupa.
Ilipofika saa kumi na moja, nikatwangiwa simu, kucheki kioo, mtoto Anita, akaniambia kwamba anakuja nyumbani. Meseji ile, vilevile, nikaiscreenshot na kuwatumia masela, nilitaka waone kwa macho yao na wajue kwamba mtoto angeliwa siku hiyo hivyo hela yangu iandaliwe kabisa.
Miraji: Oyaaa....mtoto anakuja?
Mimi: Kwani meseji inasemaje?
Miraji: Anasema anakuja....
Mimi: Basi jua hivyo...ndiyo hivyo anachinjwa....
Miraji: Daaah! Kweli unakwenda kumla Anita?
Mimi: Kwani kuna ugumu! Mbona simpo tu....mimi si ndiyo mkali wenu....tulieni, mtanyooshwa tu.
Basi ndiyo hivyo nikaanza majigambo yangu! Washikaji hawakuamini kama kweli siku hiyo ndiyo hivyo mtoto mtoto alikuwa akiliwa.
Hamisi: Kwa hiyo! Tuje kupiga chabo?
Mimi: Hahaha! Acheni ujinga, hamjishtukii kuuona utupu wa watu wazima...hebu subirini.....
Hamisi: Daah! Ila mtoto yupo poa sana, haina noma, kamilisha kila kitu, ila ukitufuata, njoo na uthibitisho...
Mimi: Haina noma.
Ndiyo hivyo, saa kumi na mbili jioni, mtoto huyo kwenye simu, alikuwa amekaribia na nyumbani hivyo nikatoka nje na kumchukua. Kama washikaji walivyoniambia kwamba siku hiyo mtoto alitokelezea, ilikuwa kweli kabisa, Anita huyu....duuuh! alikuwa balaa aiseee.
Nikamwangalia kwa macho ya matamanio, na mwisho wa siku nikaingia naye gheto.
Anita: Wewe ndiye mgonjwa?
Mimi: Ndiyo! Naumwa kweli...hebu nifanyie masaji kwanza...
Anita: Mmh! Aya, ya mgongo au?
Mimi: Potepote...nivue nguo?
Anita: Naogopa kukuchungulia.
Mimi: Acha hizo.....
Hapohapo nikavua nguo, nikabaki na boksa, nikajilaza juu, mikono yake laini ikaanza kupitapita mgongoni kwangu, akaanza kuniminyaminya.......nilibaki nikiugulia tu....aishiiiiii....agghhh...hapohapo......
*****
Kuna kitu nilichokifahamu sana maishani mwangu kuhusu wasichana, ukimwambia msichana aje nyumbani halafu siku hiyo usimuonyeshee mbwembwe zozote zile ni lazima atakuona boya na ndiyo maana wanaume wengi wanaokuwa na huo uboya, wanapogombana na wasichana hao, utasikia wakiambiwa, hivi wanaume wakiambiwa watoke, na wewe utatoka? Hivi kuna mwanaume ambaye anaweza akamkosa mwanamke wakiwa chumbani? Kuna mwanaume mwenye uwezo wa kumwacha mwanamke chumbani kama wewe?
Nililijua hilo na nikajisemea kama kweli na mimi nitamwacha, unaweza kusikia kesho chuo kizima wamejua kwamba manzi alikuja gheto halafu nikamkosa, sasa ningefanyaje? Nani anataka kuonekana boya? Kwangu, walaaaaa....sitaki kabisa mchezo huo, kama amekuja, kinachofuata ni kumaliza kazi tu.
Mimi: Shuka chini kidogo....
Anita: Nishuke chini tena?
Mimi: Ndiyo! Hapo mgongoni, shuka mpaka kiunoni....
Anita: Sawa.
Uzuri wa Anita bhana hakuwa mbishi, nilichomwambia, alikifanya tena kwa nguvu zote, basi akashuka chini, karibu na kiuno na kuanza kukiminyaminya, yalikuwa ni mambo ya masaji yaliyonifanya niwe hoi.
Nikabaki nikiugulia, miguno iliyomaanisha kama nikiachiwa nafasi, sirembi. Basi akaendelea na kuendelea, baadaye akasema amemaliza hivyo nilitakiwa kugeuka na kulala chali, nikafanya hivyo.
Aliendelea kunifanyia masaji huku nikiwa hoi kabisa, nilishindwa kuvumilia, napo nikamwambia ashuke chinichini, akashtuka.
Anita: Nishuke chini?
Mimi: Yeah...chini ya kiuno...
Anita: Mmh! Jamaniiiiiii
Kweli bwana, huko si ndiyo kulikuwa na mzuka kwenyewe. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa peke yangu home, ukimya ulitawala huku taa ikiendelea kuwaka. Wakati akiendelea, yaani ghaflaghafla tu umeme huo ukakatika, kukawa na giza la hatari.
Mimi: Afadhali......
Anita: Afadhali ya nini?
Mimi: Umeme kukatika....
Nilipomwambia hivyo tu, nikamvuta karibu na kwangu. Aisee washikaji, hata kama umeme umekatika halafu upo ndani na mtoto, nahisi macho yanapewa uwezo mkubwa wa kuona, japokuwa kulikuwa na giza, lakini Anita nilimuona, nikamshika na kumvutia kwangu....akawa anahema juujuu.
Mimi: Inakuwaje sasa?
Anita: Kuhusu nini? (Aliuliza kwa sauti ya mahaba)
Kuna aina tatu za kujibu maswali, kuna kujibu swali kwa swali, kujibu swali kwa jibu na pia kujibu swali kwa kuwa kimya. Hiyo njia ya tatu ndiyo niliyoitumia, aliponiuliza, sikujibu zaidi ya kuinuka na kumsogeza karibu zaidi.
Tulibaki tukiangalia, kilichofuata, nikaanza kutoa nguo zake, moja baada ya nyingine huku nikiwa kwenye haraka kubwa kana kwamba niliambiwa nisipofanikiwa kwa dakika moja, ndiyo basi tena.
Anita alikuwa wangu tu, asingeweza kutoka, wakati ndiyo kwanza nimemlaza vizuri kitandani, umeme huo, nikaona siyo tatizo, nikaenda na kuizima taa na kurudi kitandani.
Wote tulikuwa watupu kabisa, kilichofuata ni kuanza kuchokozana hapa na pale, akisema baba njoo huku, mimi namjibu nimekwishakuja mama, kuna tatizoooo? Ulikuwa ni wakati wa kuandaana kwanza, nilitaka kumuingiza katika ulimwengu wa mahaba, hivyo sikutakiwa kuwa na presha, kipindi hicho mzee mzima sikuvua boksa yangu, ilibaki vilevile mwilini ikiendelea kuchafuka.
Mimi: Kifua chako......
Anita: Kimefanya nini?
Mimi: U mbichi kabisa, najiona kuokota dodo benki....
Anita: Hahah...hebu nikune kwanza...
Mimi: wapi kunawasha? Hapa? Huku? Niambie basi, wapi jamaniiiii?
Wakati nasema hivyo, huku nikimuuliza kama ni hapa au kule, mikono yangu ilikuwa makini kabisa. Stimu zikawa high, yaani hata kama kuna mtu angenifuata na kuniambia Chilo kuna watu wanakuvamia na mapanga, wakikukuta hapa wanakuua, kwangu poa tu, siyo tatizo.
Wakati tukiendelea kushikanashikana hapa na pale, ghafla nikaanza kusikia honi nje ya nyumba yetu, walikuwa wazazi wangu ndiyo wanarudi nyumbani, Anita akashtuka sana.
Anita: Wakina nani tena?
Mimi: Watakuwa wazazi...daaah!
Anita: kwa hiyo unakwenda kufungua?
Mimi: Ndiyo! Si unajua hakuna mwingine humu zaidi yangu.
Hakuna siku ambayo niliwalaani wazazi kama siku hiyo, waliniondolea stimu, nikaanza kujiuliza, kwa nini siku hiyo waliwahi kurudi tofauti na siku nyingine? Kila nilichojiuliza, nilibaki nikiwalaumu tu.
Baba: Haujambo?
Mimi: Sijambo shikamoo...
Baba: Marahaba....
Wakaingia ndani, harakaharaka nikaelekea chumbani na kuanza kuongea na Anita ambaye tayari alivaa nguo zake na kutaka kuondoka.
Mimi: Kwa hiyo?
Anita: Tufanye siku nyingine mpenzi....leo, mambo yashaharibika.
Mimi: Poa, haina noma.
Je, nini kitaendelea?
Hongera sana
kanungila acha uongo kwa hiyo sura huwezi kuwa na miaka 22
😂😂😂😂😂kanungila acha uongo kwa hiyo sura huwezi kuwa na miaka 22
[emoji23]kanungila acha uongo kwa hiyo sura huwezi kuwa na miaka 22