CLASS CHATTING - 03.
SIKU YA TATU
Niliamka asubuhi na mapema, nikajiandaa na kuanza kuelekea chuoni kama kawaida. Kichwa changu kilimuwaza sana Anita na kuona kwamba muda wowote ule basi ningeweza kuchukua mzigo, nikawa nao na lile dau lililokuwa kwa washikaji basi ningelichukua.
Wakati nikiwa njiani, tena nikiwa nimepita njia ya kwao kabisa, nikamuona akiwa kituoni, nilichokifanya ni kusogea na kisha kupiga honi, alipoliona gari langu, mbona haraka sana akalifuata.
Mimi: Karibu...
Anita: Asante..
Akajiweka kitini. Siku hiyo alivalia kisketi chake kifupi, alipokaa tu, basi ikapanda juu, mapaja yakawa nje, mtu mzima midadi ikanipanda, nikaona kwa nini nisilegeze moyo tu! Ila nikahofia kwa kuona kama utakuwa umejirahisisha kwa kumwambia fastafasta angeanza pozi zake, nilimfahamu vilivyo Anita.
Anita: Bado una hasira na mimi?
Mimi: Kiduchu tu...ila una vipozi f’lani visivyokuwa na msingi...
Anita: Jamani nisameheeee mwenzio, unakuwa na hasira mpaka naogopa.
Mimi: Nikwambie kitu Anita?
Anita: niambie (Akajiweka sawa kitini)
Mimi: Huwa ninajitambua, nina vijihasira flani hivi, ukinizingua, nakuzingua, halafu sipendi kupotezewa muda, ukinipotezea muda, nakuchukia, halafu huyo nasepa zangu....
Anita: Basi naomba unisamehe....
Mimi: Usijali...
Tulikuwa tukipiga vistori tu, kila wakati kazi yake kubwa ilikuwa ni kubadilisha vimikao tu pale kitini, mara akunje nne, mara akibinue kikalio chake, mara apandishe miguu mpaka kwenye dashbodi, yaani kwa kifupi, mtu mzima nilikuwa nategwategwa.
Anita: Nashukuru...
Aliniambia baada ya kufika chuoni, akateremka, sikutaka kuteremka, yaani sikutaka kuonekana naye ili niwape uhakika wale marafiki zangu kwa kuona kwamba labda wangeweza kushinda wale hela yangu.
Akateremka na mimi kuondoka na gari hapo, hata sehemu ya kuegesha gari langu nilibadilisha. Siku hiyo, mwenyewe akawa ananitumia meseji tu kwenye simu, nikaona si mbaya kama nikichati naye...hivyohivyo..
Anita: Leo nina furaha sana....
Mimi: Ya nini tena?
Anita: Kunisamehe....
Mimi: Usijali basi, una nafasi leo?
Anita: Nafasi ya nini?
Mimi: Ushaanza.....
Anita: Jamani si ndiyo nauliza....sasa nitasema nina nafasi na wakati sijajua ya nini!
Mimi: Nataka nikutoe out...sehemu fulani hivi...
Anita: Kule pa siku ile uliposema ungenitoa?
Mimi: Yaap...upo tayari?
Anita: Saa ngapi?
Mimi: Mbili usiku...
Anita: Sawa...
Basi ndiyo hivyo, kwa klasi, kama kawaida yangu sikutaka kujionyesha, mwenyewe nilikuwa bize na mambo yangu na hata washikaji hawakujua kama kweli mtoto nilikuwa naye beneti.
Nilichokuwa nikiwafanya ni kama daktari, yaani wao walikuwa wagonjwa na kila wakati nilikuwa nikiwapa moyo kwamba watapona lakini ukweli ni kwamba wangekufa.
Nilishaona dalilii kwamba Anita alipagawa kwangu, hivyo mimi ndiye niliyetakiwa kufanikisha mpango mzima. Nilichokifanya, kama kawaida yangu nilikuwa kimya, kama sikupenda kuona kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake, tukaondoka chuo huku masela wakiniuliza tu, vipi? Utaweza? Utamla? Mbona hatuoni hata dalili? Au umeshindwa? Kila wavyotuma meseji zao, niliwalia doro.
Ilipofika saa moja, harakaharaka nikamcheki kwenye simu, nilitaka nijue kwanza kama itawezekana au la.
Mimi: Inakuwaje sasa?
Anita: Poa...
Mimi: Upo wapi?
Anita: Kwa mama mdogo...
Mimi: Wapi?
Anita: Mabibo...
Mimi: Mmh! Nitaweza kukuona kweli?
Anita: Kwa leo...sidhani, naomba tufanye siku nyingine.
Kwanza nikanywea, sikuamini kama kweli siku hiyo napo nilitakiwa kukosa utamu...huyu Anita alitaka kunizingua tu, yaani alikuwa akiingia na kutoka, nilimmaindi sana lakini sikuwa na jinsi, nilichokifanya ni kumpigia simu, nikamuuliza tena kwamba itawezekana kuonana lakini jibu lake eti likawa lilelile kwamba isingewezakana.
Mimi: Hivi kweli itashindikana jamani?
Anita: ndiyo! Haraka ya nini Chilo? Tufanye hata siku nyingine.
Sikutaka kuendelea kufuatilia, nilichokifanya ni kuichukua namba yake na kuiandika sehemu kisha nikafungua mtandao mmoja na kuiingiza namba yake, mtandao ambao uuliunganishwa na GPS kujua mahali alipokuwa.
Sehemu ya kuingiza namba, nikaingiza namba yake kisha kubonyeza sehemu iliyoandikwa GPS Locator...baada ya hapo, ikatokea ramani ya dunia, ikaanza kuitafuta namba yake, ikavutwa Tanzania, Dar es Salaam na mwisho wa siku kuonyesha kwamba namba yake ilikuwa sehemu iitwayo Tandale, yaani mtaa uleule nilipokuwa, nikapata uhakika kwamba hakuwa Mabibo kama alivyosema, alikuwa akinidanganya.....hasira zikanipanda.
Nikaanza kumtafuta kwenye simu kihasirahasira....
*****
Sikutaka kumchelewesha, hapohapo nikampigia simu, tena nilionekana kukasirika haswaaa, haiwezekani msichana aniletee zake za kuleta, yaani ajione yeye mjanja hata zaidi yangu. Simu haikuita sana, ikapokelewa.
Mimi: Wewe Anita.
Anita: Abee.
Mimi: Mbona unanifanyia makusudi sana?
Anita: Makusudi ya nini tena?
Mimi: Unataka kuonana nami au hautaki?
Anita: Ninataka ila nipo mbali na nyumbani.
Mimi: hivi unanifanya mimi mtoto?
Anita: Kwa nini tena jamani?
Mimi: Nisikilize, umeniambia upo Mabibo, unaidanganya na wakati upo kwenu.
Anita: Nani kakudanganya, nipo Mabibo, haki ya Mungu tena.
Mimi: hebu niondolee ujinga wako! Hivi internet inaongopaga? Toka lini ukaona kifaa cha mzungu kinadanganya! Upo nyumbani kwenu ila umeamua kunizingua, sasa sikiliza......
Anita: Chilo...
Mimi: Nini?
Anita: Nani kakudanganya nipo home?
Mimi: Unabisha?
Anita: Sipo nyumbani, kweli tena.
Mimi: Sasa nimeshafika kwenu, naingia ndani halafu nakuulizia, nataka niamini.
Anita: Chilo, usifanye hivyo, baba yupo.
Mimi: Baba yako hayupo, ametoka, nimepishana naye njiani.
Anita: Haki ya Mungu tena, yupo.
Mimi: Umejuaje kama yupo na wakati upo Mabibo? Mimi niliyekuwa Tandale nimekwambia hayupo, wewe uliyekuwa Mabibo umesema yupo, umejuaje?
Kimyaaaa...
Unajua mi ndo maana sometimes naona watoto wa kike wanazingua tu. Yaani ishu ya kuonana nami aliifanya iwe complicated kinoma na wakati ilikuwa ishu ya kawaida tena ya mara moja kabisa.
Kweli nikasepa nyumbani na kuelekea kwao, nilitaka nimuhakikishie kwamba alikuwa muongo. Nilipofika kwao, haikuwa ishu kuingia ndani japokuwa kulikuwa na mlinzi, nikazama zangu ndani kwani mlinzi alinizoea, si unajua mshikaji wa kitaa.
Nilipofika ndani tu, nikakutana na dada wa kazi. Kwanza, dizaini fulani akashtuka, hakuamini mimi kuwa pale muda ule.
Mimi: Hujambo Zubeda?
Zubeda: Sijambo! Shikamoo.
Mimi: Poa tu. Anita yupo?
Zubeda: Yupo, nikakuitie?
Mimi: Ndiyo! Kwani hakutoka?
Zubeda: Hakutoka, yupo ndani, ngoja nikamuite.
Nilitaka kushangaa bhana, inakuwaje Mzungu awe muongo, GPS ilionyesha kwamba alikuwa kitaa kwao kasizi, sasa aniambie yupo Mabibo, wapi na wapi. Baada ya muda, huku akionekana kuwa na aibu, Anita huyo akatoka nje, nilipomuona, sikufichi msela wangu, nilishikwa na hasira.
Anita: Naomba unisamehe...
Mimi: Wewe mpumbavu kweli Anita...yaani wewe mpumbavu sana....
Sikutaka kuongea zaidi, nilichokifanya, nikageuka kama mwanajeshi, kisha huyo nikasepa zangu. Sipendi kukuficha, napenda kuwa mkweli tu, yaani siku hiyo nilikasirika sana, sikutaka kumuona Anita tena kwani alinifanya mimi mtoto na wakati nilikuwa mtu mzima.
Usiku huohuo, mtoto akaanza kutuma meseji za samahani, yaani kila iliyoingia, ilikuwa na samahani kubwaaaa, sikujali, sikumjibu meseji zake, nilibaki kimya huku nimetulia tu, kila nilipokuwa namfikiria, alinikasirisha zaidi.
Anita: Naomba unisamehe Chilo wangu.
Kimyaaaaa
Anita: Naomba unisamehe jamani sitorudia tena....
Kimyaaaaa
Anita: Najua nimekukosea, sikutakiwa kukudanganya Chilo, ila nimefanya hivyo kwa kuwa bado naogopa, sijiamini kabisa, naomba unisamehe...
Kimyaaaaa
Sikutaka kujibu meseji yake yoyote ile, niliamua kwa nia moja kwamba ni lazima nifanye kama mwanaume mwenye msimamo, mtoto wa kike ni mtu wa kawaida sana na sometimes ni lazima ajue kwamba kuna wanaume wenye misimamo migumu ambayo haikuweza kuyumbishwa na kitu chochote kile.
Unapojifanya mlegevu kwa msichana, ni lazima utasumbuka sana, ni lazima uwe na msimamo kwani baadhi ya wanawake wengine, wanapenda wanaume wenye misimamo, wanaosimama kama wanaume na si wale wanaobadilikabadilika kama kinyonga.
Anita aliniomba sana msamaha lakini wala sikuwa na muda, sikutaka kumjibu meseji yake yoyote ile, niliuchuna kama sikuziona meseji zake. Naye hakuacha, yaani ni kama aliambia kwamba akiendelea kutuma mesji basi ningelainika kumbe si hivyo, ninaposema kwamba nimekasirika, huwa ninakasirika kweli na sitaki ujinga kabisa.
Anita: Japokuwa hutaki kunijibu, nakutakia usiku mwema.
Kimyaaaa....
Je, nini kitaendelea?