Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

Nime subscribed huu uzi nitaridi kukusoma kwa uzuri mkuu.
 
*KUTANA NA MIJI MIKONGWE ZAIDI DUNIANI AMBAYO BADO IPO MPAKA SASA.*




Miji mikongwe zaidi duniani!
Kadri idadi ya watu inavyoongezeka duniani, kwa baadhi ya nchi hulazimu kuunda mikoa mipya au miji mipya ili kuendana na kasi ya ukuaji huo kwa ajili ya kurahisisha huduma mbalimbali za jamii. Lakini nenda uendako, idadi ya watu itaongezeka na miji itaongezeka lakini miji ifuatayo itabaki kuwa miji mikongwe zaidi duniani.



*1. Damascus,Syria.*

Ni mji mkuu wa nchi ya Syria ambao pia ndio mji mkubwa zaidi kijiografia nchini humo. Unakadiriwa kuwa na population ya watu zaidi ya milioni 4.5. Mji huu unakadiriwa kuwepo tokea kipindi cha kati ya miaka ya 10,000-8,000 B.C, hivyo kuufanya kuwa mji mkongwe zaidi duniani.

Mji huu pia ndio kiungo muhimu zaidi cha nchi ya Syria kwani ndio moyo wa shughuli zake zote za iutawala, kibiashara na kitamaduni.

Vivutio vikubwa vinavyofanya watalii kumiminika katika mji huu ni kushuhudia majengo ya kale yenye mvuto wa kipekee.



*2. Athens,Greece.*

Athens ni mji mkuu wa Ugiriki unaokadiriwa kuwa na wakazi milioni 3. Ni mji wenye watu wanaofuata imani za kiromani,Ottoman na Byzantine.

Ni mji unaoaminika kutoa philosophers,waandishi, dramastics na wasanii wengi na nguli zaidi duniani, sifa inayoufanya kuwa wenye sifa za kipekee kabisa.

Ni mji wa kihistoria ambao una muonekano wa juu(High city), kutokana na kuwa umejengwa kwenye miinuko inayofanya kuwa na muono mzuri kuangalia chini.

Kutokana na mji huu kutambulishwa kuwa ni archeological research center, umesheheni makumbusho ya kihistoria kama National archaeological museum,The byzantine and Christian museum na The new acropolis museum.

Na kama ukifanikiwa kutembelea Athens, basi usithubutu kutotembelea bandari ya Piraeus ambayo ni bandari muhimu huko Mediterranean kwa karne nyingi zilizopita kutokana na eneo lake lilivyo kijiografia.



*3. Byblos,Lebanon.*

Ni mji wa zamani katika nchi ya Lebanon, na unashikilia nafasi ya tatu kwa ukubwa kwa kuwa mji mkongwe zaidi duniani ukikadiriwa kuwepo kwa zaidi ya miaka 5000. Na cha kufurahisha zaidi ni kwamba neon la kiingereza Bible likimaanisha biblia limetoholewa kutokana na jina la mjii huu,Byblos. Ni mji lovely kwa utalii.

Siku hizi umekuwa ni mji wa kisasa ukiwa na majengo ya kioo, kitu kinachoufanya uvutie zaidi kutokana na muunganiko wa utamaduni na usasa.(Traditions meets moderm).



*4. Jerusalem, Israel.*

Ndio mji unaotembelewa zaidi nchini Israel na vilevile ni kituo muhimu cha kidini duniani. Jerusalem ni mji unaojulikana kama ni mji mtakatifu kwa wayahudi, wakristo na waislamu. Kwa mujibu wa biblia, mji wa Jerusalem ulifanywa kuwa mji mkuu wa Israel na Daudi.

Siku hizi Jerusalem una wakazi wanaokadiriwa kufikia 800,000 huku wayahudi wakiwa wengi zaidi, wakikadiriwa kufikia asilimia 60 ya wakazi wote wa mji huo.

Ni mji ulioanzishwa miaka 4000 iliyopita na umegawanywa katika vipande vine ambavyo ni sehemu ya wakristo,waislamu,waarmenia na wayahudi, hali inayoufanya kuwa ni mji unaokumbwa na machafuko ya mara kwa mara na mashambuliza ya kujitoa muhanga kutokana na matabaka hayo, hali iliyofanya mwaka 1981 kuwekwa kwenye orodha ya mji wa urithi wa dunia uliopo katika hatari.


*5. Varanasi,India.*

Mji wa kiroho wa Varanasi, unapatikana kandokando ya kingo za mto Ganges na umejumuishwa katika orodha ya miji ya kale zaidi duniani. Wahindi wanaamini kuwa ni mji ulioasisiwa na mungu Shiva katika karne ya 12.BC.



*6. Chochula,Mexico.*

Ukiwa na zaidi ya umri wa miaka 2500, mji wa Chochula umejengeka kutoka katika muunganiko wa vijiji mbalimbali kama Olmecs,Tolteas na Azteas na unakadiriwa kuwa na wakazi elfu 60.
Chochula maana yake ni "place of flight", na hapo awali ulijulikana kama Acholollan.

Kivutio kikubwa katika mji huu ni "Great pyramid of Chochula ambayo inajulikana kama mnara mkubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na binadamu. Ni mnara unaojumuisha njia mbalimbali chini ya ardhi na mapango yenye urefu wa kilometa 8.

*7. Jericho,Palestina.*

Unakadiriwa kuwa na umri wa miaka elfu kumi na moja na kukadiriwa kuwa na wakazi elfu 20.
Katika kitabu Hebrania katika biblia, mji huu unatambulishwa kama,"A city of palm trees."

Mji wa Jericho unapatikana katikati ya palestina na hivyo kuwa ni mji kiungo muhimu kubiashara.
Katika karne ya 20, mamlaka ya Jericho yalikuwa chini ya utawala wa Jordan na Israel.Mwaka 1994 mamlaka yalihama na kuwa ya Palestina.

Vivutio vikuu vya Jericho vinajumuisha Tell es Sultan, Hisham's palece na Shalom al Yisrael Synagogue Masaic floor.

*8. Allepo, Syria.*

Ni mji mkubwa zaidi nchini Syria ukikadiriwa kuwa na wakazi wanaofikia milioni mbili. Ni mji wenye faida sana kijiografia kwani unapakana na barabara ya Silk ambayo ndiyo inayounganisha Asia na eneo la Mediterranean.

Ni mji unaodaiwa kuwepo kwa miaka 8000 iliyopita na unajulikana pia kwa jina la "The soul of Syria."

*9. Plovdiv,Bulgaria.*

Ni mji unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 4000 B.C. Kwa karne nyingi mji wa Plovdiv umekuwa chini ya tawala mbalimbali, ingawa kiuhalisia hapo mwanzoni ulikuwa mji wa Thracian. Baadaye walitawaliwa na Romans.

Katika zama za kati,Plovdiv walikuwa chini ya utawala wa Bulgaria,Byzantine na Ottoman. Lakini mwaka 1885 ndio hasa mji huu ukawa rasmi sehemu ya Bulgaria, na kuwa mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.

*10. Luoyang,China.*

Mji wa Luoyang unatajwa kuwa na umri wa miaka 4000 B.C huku ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kufikia milioni saba.

Wakati miji mingi mikongwe duniani inaonekana kupatikana zaidi Mediterranean, Luoyang unasimama kama mji mkongwe unaopatikana Asia. Ni kati ya mji uliojumuishwa katika Seven Great Ancient Capitals of China.

Mji wa Luoyang una mengi ya kujivunia lakini mojawapo ni The longmen Grottoes, ambayo ilitajwa kama eneo la urithi wa dunia mnamo mwaka 2000. Na pia mahekalu mbalimbali ya Buddhist yameufanya mji wa Luoyang kuwa kivutio kikubwa watalii kutoka duniani kote.

Luoyang pia ni maarufu kutokana na White horse temple, ambayo ni temple ya kwanza kuanzishwa nchini China.
 
HAKIKA GADDAFI AMENITOA MACHOZI, UPENDO WAKE ULIOKITHIRI UZALENDO NDIO HUO ULIOFUPISHA MAISHA YAKE.

Leo nimeikumbuka hotuba iliyonisononesha sana mwaka 2011. Hotuba ya aliyekua kiongozi wa Libya Kanali Mu'uammar Qaddafi. Aliiandika siku chache kabla ya kifo chake.

Kwa kutambua kuwa humu wapo wanaojua Kingereza na wengine hawajui, nimeitafsiri kwa Kiswahili.

--QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru."

-- Mu'uammar Qaddafi.
 
SNIPER AELEZEA OPERATION YAO ILIVYOKUWA HADI KUFANIKISHA KUMPIGA RISASI ZILIZOMUUA OSAMA BIN LADEN.

Tangu kuuawa kwa kiongozi wa
Kundi la Al-Qaeda Osama bin Laden
kumekuwa na fununu nyingi
zinazoeleeza mazingira ya kifo chake
pamoja na ujumla wa maisha yake
wakati akiwa mafichoni.

Akiwa mtu mwenye tabasamu na
ucheshi wa mbali, askari (jina
linahifadhiwa) anatoa maelekezo
kwa mwandishi wa habari aliyetaka
kujua historia ya maisha yake
jeshini. Ndani ya mgahawa
uliofurika watu waliochangamka kwa
vinywaji, askari mwanamaji anaanza
kueleza namna alivyojiunga na Jeshi
la Wanamaji la Marekani hadi
kufikia nafasi ya kuwa mlenga
shahaba mkuu.

Anasema anakumbuka kile
kilichomsukuma kuchukua uamuzi
wa kujiunga na jeshi ni kama sehemu
ya hasira iliyomkumba baada ya
kuachwa na mpenzi wake al iyedumu
naye kwa kipindi kirefu.

Unajua tukio la kuachwa na mpenzi
wangu lilinivunja moyo sana… na
ndiyo nikachukua uamuzi kwenda
jeshini.

Anasema kuwa siku yake ya kwanza
alipokwenda kuomba kazi
anakumbuka alimwambia ofisa
mmoja wa jeshi kuwa alikuja hapo
kuomba kazi ya kulenga shahaba
(sniper).
Pale nilimkuta askari mfukuzi,
mkufunzi akaniuliza unataka nini…
nikamwambia nataka kuwa mlenga
shahaha, lakini yeye akaniambia
kuwa tayari walikuwa na walenga
shabaha.

Hata hivyo alifaulu kuandikishwa na
baadaye kupelekwa kwenye mafunzo
yaliyimwongezea ujuzi wa kazi na
hatimaye kuungana na vikosi vya
wanajeshi wa maji vilivyosafiri
sehemu mbalimbali duniani. Kama
ilivyo kwa askari wengi wanamaji,
askari huyu alishiriki kwenye
operesheni mbalimbali za kijeshi
ikiwemo zile zilizohusu katika nchi
za Afghanistan na Iraq.

Anasema operesheni yake kubwa ya
kijeshi ilikuwa nchini Afghanistan
ambako vikosi vya Marekani
vilivamia katika eneo hilo katika kile
kilichoelezwa na kukabiliana na
utawala wa Taliban ambao ulitajwa
kuwa na ushirikiano wa karibu na
Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda.

Uzoefu mkubwa wa kijeshi niliupata
wakati nikiwa Afghanistan ambako
nakumbuka nilishiriki kikamilifu
kukabiliana na wanamgambo wa
Taliban. Tulipofaulu kuwafurusha
wanamgambo hao tuliendelea
kubakia nchini huko kuimarisha hali
ya usalama na kusaidiana na
wananchi wa eneo lile kurejesha hali
ya usalama.

Kichwa changu kilikuwa tayari
kimeshazoea mizinga na
makombora, maana wakati
mwingine umekaa sehemu ghafla
unasikia kombora linavurumishwa
mbele yako… Ghala nyuma unasikia
mlio wa bunduki.. Kusema kweli
nilijifunza mengi wakati nikiwa
Afganistan.

Wakati huo Marekani ilianzisha
operesheni za kukabiliana na Kundi
la Al-Qaeda ambalo lililodaiwa
kutekeleza tukio la kigaida katika
majengo yake mjini New York na
Washington.

Shabaha ya Marekani ilikuwa
kukabiliana na kiongozi wa kundi
hilo, Osama bin Laden ambaye
wakati huo ilisemekana
amejichimbia mafichoni katika
Milima ya Afghanistan.
Marekani haikuishia kuingia kijeshi
nchini Afghanistan pia iliivamia Iraq
na hatimaye kuuangusha utawala wa
Saadam Husen aliyekuwa akiongoza
Chama cha Baath ambacho kilikuwa
na uhusiano pia na baadhi ya
makundi ya kigaidi.

Anakumbuka kuwa jinsi alivyorejea
nyumbani Marekani na kisha
kuungana na wanamaji wenzio
ambao waliunda kikundi cha
wataalamu wachache walikuwa na
shabaha ya kuleta mageuzi ya
utendaji ndani ya vikosi vya
wanamaji hasa kwa kutumia uzoefu
waliopata wakati wakiwa kwenye
operesheni za kijeshi katika nchi za
kigeni.

Unajua ukishajiingiza kwenye
mambo haya ya kulenga shabaha
hujali tena lolote, wewe unachoona
ni kwamba umeletwa duniani kwa
kazi maalumu na hiyo kazi lazima
uitekeleze kwa wakati uliopangwa,
anasema askari huyo akimwelezea
mwandishi mmoja wa habari namna
alivyoshiriki kwenye kikosi maalumu
kilichoshiriki kwenye operesheni ya
iliyofanikisha kuuawa kwa kiongozi
wa Kundi la Al-Qaeda, Osama bin
Laden.

Kwa masharti ya kutotajwa jina wala
kuonyeshwa picha yake, askari huyo
anasema kuwa, “Tulipomaliza kazi
nchini Afghanistan tulirudi
nyumbani na kuendelea na mazoezi
yetu ya kuogelea katika Ufukwe wa
Miami. Tukiwa kule ghafla tukapata
taarifa baadhi yetu tulihitajika
kwenda Virginia kwa ajili ya kazi
maalumu.

Kusema kweli hatukujua nini
tunachokwenda kukifanya maana
tulielezwa kuwa kuna kazi ya
dharura. Wengi wetu tukabaki
tunahisi labda tunataka kupelekwa
Libya, wengine wakasema labda
tutaenda Japan kukabiliana na athari
za kimazingira baada ya tetemeko
kubwa la ardhi kulikumba taifa hilo.
Katika siku ya kwanza tulivyopata
taarifa, kusema kweli
walitudanganya. Tulizungushwa
maeneo mbalimbali na kila mara
maofisa wetu walikuwa wakitupa
maelezo ya kutia matumaini
wakisema kuwa tusiwe na wasiwasi
tutaarifiwa punde kwani kulikuwa
hakuna jambo lolote la kutisha.

Anasema kuwa baada ya kukaa kwa
siku kadhaa walipelekwa moja kwa
moja hadi yaliko makao makuu ya
upelelezi CIA, ambako walipokelewa
na maofisa wa ngazi juu
aliyewagawanya kwenye vitengo bila
kuwapa maelekezo yoyote.

Wakati tunakwenda tuliambiwa
tungekutana na Waziri wa Ulinzi,
maofisa wa ngazi za juu wa jeshi
pamoja na wataalamu wengine wa
kijeshi. Tulipata hisia jambo
tulioloitiwa huko huenda likawa
kubwa. Tulipofika pale tulikusanywa
kwenye chumba kimoja na baada ya
muda alitokeza mwanamke mmoja
ambaye kwa sura alionekana kuwa
mtu jasiri na mwenye kuelewa kile
anachokizungumza.

Tuliona tumeletewa
televisheni..vifaa vya kivita na
pembeni kulikuwa na ramani kubwa
ambayo hata hivyo ilifunikiwa na
kitambaa . Hatukujua kile
kilichokuwa kinaendelea. Yule
mwanamke aliposimama ndipo
pumzi ikatushuka,” Anaelezea kuwa
walipatiwa maelekezo kuhusiana na
sehemu ambayo inasadikika Kiongozi
wa Al-Qaeda, Osama bin Laden
ndiyo ilikuwa makazi yake.

Yule askari wa kike akiwa katika
hali ya kujiamini, alituonyesha
ramani na kutufafanulia shabaha ya
kuitwa kwenye chumba kile.
Nilishtuka lakini kadiri
nilivyomtazama yule askari
niliamini kile alichokuwa akikisema.
Tulionyeshwa nyumba moja ambayo
iko pekee yake katika eneo la
Abbottabad.

Baada ya hapo tukaingia kwenye
mazoezi makali tukijifunza namna
ya kuingia kwenye nyumba ile na
namna tukavyoweza kumudu
purukushani zozote zinazoweza
kujitokeza.
Mafunzo yetu yalidumu kwa muda
wa wiki kadhaa na kisha tulipangiwa
siku ya kuondoka kuelekea Pakistan.
Anasema kuwa msafara wa kuelekea
Pakistan alianzia nchini Ujerumani
walikoweka kituo na kisha kuruka
moja kwa moja hadi nchini Pakistan
kupitia eneo la Jalalabad.

Unajua wakati tunakatiza anga ya
Pakistan niliingiwa na hofu sana
pengine vikosi vya pale vingeilenga
ndege zetu na kuzitungua maana
kulikuwa hakuna taarifa zozote kwa
Serikali ya Pakistan kuwa Majeshi ya
Marekani yalikuwa yakiingia nchini
humo.

Tulipita eneo lile na hatimaye kufika
Abbottabad. Tulikuwa tumejipanga
vya kutosha. Msafara wetu ulikuwa
na helikopta, ndege za kivita pamoja
na vifaru kukabili hali yoyote korofi
ambayo ingejitokeza.
Nilishangaa kuona kile
nilichoonyeshwa kwenye picha za
satelaiti wakati nikiwa kwenye
mazoezi Marekani ndicho
nilichokishudia pale.

Tulishuka kwenye helikopta haraka
na kisha kuizingira nyumba mara
moja. Kuna wengine walitanda juu
ya paa, wengine madirishani na
wengi walikuwa angani kwenye
helikopta.

Tulipofika mlangoni tulikuta tundu la
risasi, tukashtuka kidogo,
nikamwambia mwezangu acha woga
hebu twende, nikasukuma mlango
hadi ndani.
Wakati kabla hatujaingia ndani
tulisikia sauti ikiita bla, blab la,,,
kumbe ilikuwa sauti ya mmoja wa
walinzi wa Osama ambaye alikuwa
amevalia fulana nyeupe na pajama
nyeupe pia.

Tulimdhibiti na kupanda hadi
ghorofa ya pili ambako tuliwakuta
kina mama wakiwa wanahangaika
na kupiga kelele.
Hatukutaka kuwadhuru tuliwaweka
chini ya ulinzi, nami nikaendelea
kupanda juu hadi ghorofa ya tatu.

Nilipofika chumba cha juu
nilimwona mtu mmoja mrefu kupita
wote, ndevu zake alikuwa ameonyoa
kiasi. Alikuwa ameweka mikono yake
begani kwa mwanamke mmoja
ambaye baadaye nilikuja kugundua
alikuwa mkewe Jamal.
Nadhani alikuwa anafanya vile kama
njia mojawapo wa kujikinga. Alikuwa
amevalia kofia na kuendelea
kuzunguka huku na kule na yule
mwanamke.

Nakumbuka alikuwa mwembamba.
Pembeni yake kulikuwa na silaha
aina ya AK 47, ambayo baadaye
aliishika mkononi.
Binafsi sikutaka kupoteza muda,
nilinyanyua bunduki yangu na
kumiminia risasi mbili usoni na
kisha nikamshudia namna
alivyoanguka chini na kukata roho.

Na huo ndio ukawa mwisho wa Osama kuvuta pumzi ya dunia hii.
 
HUU NDIO MPANGO KABAMBE ULIOFANIKISHA FUMAZI LA KINGONO KATI YA RAIS BILL CLINTON NA MREMBO MONICA LEWINSKY.

Ilikuwa ni mwaka 1995 wakati huo Bill Clintoni akiw katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi mareka akiwa na umri wa miaka 46.Monica yeye alianz kufanya kazi Ikulu katika ofisi ya katibu mkuu kiongo (Chief of Staff) Leon Paneth tangu June, 1995 kam mfanya kazi mwanafunzi (Intern) akiwa ametok kuhitimu chuo cha Lewis & Clark college.Ni hapo B Clinton alipomuona na kuvutiwa na binti huyo aliekuw bado mchanga na mbichi wa miaka 21 tu na kwa muji wa Monica walianza mahusiano na Rais Novemb mwaka huohuo.

ILIKUWAJE?
Baada ya Rais kuwa na mahaba na Monica na hiv kunogewa nayo msaidizi wa katibu mkuu kiongozi Evelyn Liberman alishtukia mchezo na April 19 aliamua kumwamisha Monica katika ofisi ya msema msaidizi wa wizara ya Ulinzi (Pentagon) bwana Ke Bacon.Bi Evelyn alitoa sababu kuwa amemwamish kutokana na Monica kuonyesha tabia zisizofaa na kitoto “inappropriate and immature behavior". Laki pia watendaji wengine walikuwa wakitilia shaka ukarib uliopitiliza kati ya Monica na Rais. Ni katika ofisi hi za pentagon ndipo Monica akakutana na Linda Trip binti aliyekuwa mfanyakazi wa idara ya Ulinzi katik wizara hiyo wakaunda urafiki.
Kutokana na ukaribu wa kiutendaji kati ya Pentago na Ikulu bado Monica alikuwa na nafasi kubwa y kuwa anafika Ikulu mara kwa mara na mara zo alitumia muda mwingi sana katika ofisi ya Rais ki ambacho bado hakikuwa kikiwafurahisha wafanyaka wa Ikulu na hivyo October 1997 Ikulu iliandaa mpan wa kumwamisha tena bi Monica na kumtaka aham ofisi za umoja wa mataifa UN. Ni balozi Bill Richardso alieombwa ampangie kazi Monica lakini baada ya usa wa kazi bi Monica aliikata nafasi hiyo na hiv kubakishwa Pentagon.
Ikumbukwe mpaka wakati huo hakuna aliekuwa n ushahidi pasi shaka kuwa Monica ana “date” na Ra Clinton.Ni mwaka huo hasa baada ya kuona anazi kuwekewa vipingamizi vingi vya kukutana na Rais mar kwa mara ndipo alipoanza kumueleza Linda Trip rafiki yake wa wizara ya ulinzi juu ya mahusiano ya na Rais.Alimweleza kuwa kati ya November 1995 mpak March 1997 alishakutana kimwili na Rais Clinton mar tisa.Linda baada ya kusikia hivyo aliwasiliana n mwanausalama Agent Lucianne Goldberg aliempa kifa cha kurekodia simu na hivyo Linda akamtegeshe Monica na kurekodi simu zote alizokuwa akiwasiliana n Rais Clinton.Ni katika kipindi hicho pia kuna siku Lind Tripp alikutana ana Monica akiwa anatoka kwen ofisi ya Rais nywele zikiwa zimemvurugika na rangi y mdomoni ikiwa imebanduka.

SKENDO ILIIBUKAJE?
Baada ya Monica kugoma kutoka Pentagon lilitoka shinikizo kutoka Ikulu na haraka aligundua anafukuzwa kazi hivyo aliamua kuacha kazi kw kuahidiwa na Rais kuwa atamtafutia kazi nyingine Rais Clinton kwa kumtumia msaidizi wake Betty Cur aliyekuwa akijua kinachoendelea kati ya Rais na Monica aliamua kumtumia rafiki wa karibu wa Clinton bwana Vernon Jordan amtafutie kazi Monica.
Sasa baada ya Linda Tripp kukamilisha kukusany ushahidi wake ajenti Goldberg alimwelekeza Lind apeleke mkanda huo kwa mwanasheria wa kujitegem Kenneth Starr aliyekuwa akichunguza skendo nyingi za Clinton kama ile ya Whitewater , White House F filter Controversy na ile ya White House Travel offi controversy .Baada ya kumfikishia Kenneth yeye sas angepeleka kwa Paula Jones(Kuna sababu maalum y kufanya hivi).
Mkanda ulipomfikia Paula Jones alimwita Monica n kumwambia madai hayo Monica alikataa na ndipo ha walipowasiliana na mwandishi wa habari Micha Isikoff wa gazeti la Newsweek. Mnamo Janua 17 ,1998 Michael katika Drudge report alipoamu kuirusha hiyo habari kwa mara ya kwanza. Janua 21, 1998 gazeti kubwa la Washngton Post nalo likaruk na hiyo skendo na ikaanza kuwa kubwa na isi mithilika.
Kwa mara ya kwanza January 26, 1998 Rais Clinto akiwa anaongea na waandishi wa habari Ikulu akiw sambamba na mkewe bi Hilarry alikataa katakat kujihusisha kimapenzi na Monica. Hata alipoletew rekodi za maongezi yao Rais alikataa na kuondok haraka kwa kudai kuwa anaharaka ya kwend kuandaa spichi ya kuwasilisha hali ya uchumi ya Taifa.

NINI KILIFUATA BAADAE?
Habari ni ndefu ila itoshe tu kusema baada ya ha yapo mengi sana yaligundulika na kuendelea n kulitokea msukumo kuwa Rais ajiuzulu na yeye Februa 6,1998 akajibu “Kwa imani watu wa nchi hii waliyonip kwa kunichagua kuwa Rais wao kamwe siwezi waach kwa sababu hii”. Hilary clinton mkewe nae aliamu kuziba masikio na February 11, 1998 alinukuliw akisema “Suala hili si zito sana litakwisha tu” .
 
KUTANA NA WAKE HAWA WA MARAIS WENYE UBABE WA HALI YA JUU KWA WAUME ZAO MPAKA KWA RAIA.

Mke wa Rais alipojua udhaifu wa mume wake, kwamba anampenda sana acha afanye vituko. Nchi ikasimama. Vurugu zote yeye. Nani wa kumzuia na ndiye usingizi wa Mkuu wa Nchi?

Watu waliufahamu ukali wa Rais lakini wakawa wanastaajabu ukimya wake juu ya vitendo vya mkewe. Wengine wakasema Rais ni Bushoke, wapo waliodai Rais huchimbwa mkwara wa kunyimwa unyumba ndiyo maana alikuwa mpole.

Lucy Kibaki, Mungu amrehemu, aliitikisa Kenya miaka 10 ya Urais wa mume wake, Mwai Kibaki, kati ya mwaka 2002 mpaka 2012.

Lucy hakuwa wa mchezo, alivamia chombo cha habari na kushambulia wahariri. Aliwahi kumpa makofi mpiga picha wa gazeti la Nation kwenye kadamnasi. Watu wakashangaa. Mume wake akawa kimya.

Mwaka 2007, katika sherehe ya Siku ya Jamhuri, iliyofanyika Ikulu, MC alimtambulisha Lucy Kibaki kwa majina ya Lucy Wamboi Kibaki badala ya Lucy Muthoni Kibaki, basi MC mbele za watu akachezea makofi.

Kibaki alishuhudia lakini afanye nini? Lucy ndiye usingizi wake. Mama akazidi kutamba, akamtwanga makofi mtumishi wa Ikulu, Matere Keriri. Halafu akatamba: “Nikisema mimi ndiyo sauti ya mwisho.” Usimchezee mama Prezidaa!

Bunge la Kenya likachachamaa na kumsema Kibaki kwa kushindwa kumdhibiti mkewe. Lucy akamwambia mwanasheria Gitobu Imanyara, afungue kesi dhidi ya wabunge. Imanyara aliposema mashitaka yasingekuwa na nguvu, alichezea makofi.

Kibaki alikuwa na kawaida ya kuwaalika marafiki zake na kupata mvinyo kwenye baa ya Ikulu. Lucy akatimua marafiki wa Kibaki halafu akaagiza baa ifungwe.

Kipindi fulani vyombo vya habari viliripoti Kibaki alikuwa na mke mwingine tofauti na Lucy, basi mama akachachamaa, akamwagiza mumewe afanye mkutano na waandishi wa habari ili akanushe. Kibaki alikanusha huku Lucy akimsimamia.

HATA MAREKANI

Rais wa 19 wa Marekani, Warren Harding naye alikuwa mnyonge kwa mkewe, Florence Harding. Wakati huo, mpaka magazeti yaliandika kuwa nchi ilikuwa na inaongozwa na First Lady.

Florence aliagiza intelijensia kufanya kazi, alimwandikia Rais Harding cha kuzungumza kwa waandishi wa habari. Florence ndiye alikuwa kila kitu kwa Serikali ya Marekani. Florence aliwahi kusema yeye ndiye sauti ya Rais. Ni kama mtu mzima Robert Mugabe alivyo mpole kwa Grace.

Unajua jeuri yote ya nini? Ni mke kujua anapendwa. Mke wa Rais asiye na busara akishajua mume wake amependa mpaka ameoza kwake, basi hufanya vituko mpaka kumdhalilisha Rais mwenyewe na nchi yote.
 
MAMBO 8 YA KUSHANGAZA YANAYOFANYWA NA MWILI WAKO KUKULINDA PASIPO WEWE KUJUA.

Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.

1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.

Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.

2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.

Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.

3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.

4. KWIKWI (HICCUPING)
Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?

Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.

Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.

Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.

5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?

Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.

Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.

Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.

6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

7. MACHOZI (TEARS)
Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini

Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)

8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.

Je hutokeaje?

Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.

Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.

Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.

Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?

MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
 
WASABATO NI KINA NANI?

Nimeona vyema leo tuchambue kwa ndani juu ya watu wanaoitwa wasabato.

Wasabato ni watu ambao wanaheshimu na kuadhimisha siku ya sabato, jina lao linatokana na msisitozo wanaouweka kwenye kuiheshimu siku ya sabato. Pengine utauliza siku ya sabato ndo siku gani? Mbona katika lugha ya kishwahili hamna siku inaitwa sabato?

Neno sabato ni neno la Kiswahili lililotoolewa kutoka katika lugha ya kiebrania . katika lugha ya kiebrania neno hili linasomeka Shabbat lenye maana ya pumziko. Katika lugha ya kiebrania kuna siku inaitwa Shabbat, ambayo siku hiyo kwa Kiswahili inaitwa jumamosi. Angalia majina ya siku katika kiebrania na kiingereza,

English Name Hebrew "Name" Hebrew Meaning

kiingereza kiebraniia maana ya kiebrania

Sunday Yom Reeshone First day

Monday Yom Shaynee Second day

Tuesday Yom Shlee´shee Third day

Wednesday Yom Revee´ee Fourth day

Thursday Yom Khah´mee´shee Fifth day

Friday Yom Ha´shee´shee Sixth day

Saturday Shabbat Rest

Kutoka kwenye neno Shabbat (sabato) , wote wanaoiheshimu na kuitunza siku ya sabato(jumamosi/Shabbat) wanaitwa wasabato.

Wasabato hawa wamegawanyika katika makundi tofauti kama ifuatavyo.

1. JUDAISM / WASABATO WA DINI YA KIYAHUDI

Hawa ni wasabato ambao historia yao ni ya kale sana . wanapatikana sana katika nchi ya Israeli , dini yao chimbuko lake ni katika biblia hasa agano la kale, Pamoja kwamba wasabato hawa wanaiheshimu siku ya sabato, jambo linalowatofautisha na wasabato wengine, ni kule kuamini kwao kuwa Yesu siyo masihi .

Wasabato hawa wa dini hii ya kiyahudi hawaamini kuwa Yesu ndiye kristo/masihi. Wanakubali kuwa Yesu alikuwepo ila hawakubali kuwa Yesu ndiye masihi aliyetabiriwa kwenye biblia agano la kale. Wao bado wanangojea ujio wa masihi atakayezaliwa ambaye atazaliwa Israeli na kuliongoza taifa hilo kuwa taifa lenye kuheshimika dunia kote.

Wasabato hawa wa dini ya kiyahudi wanashikilia msimamo wa babu zao ambao ndio walikuwa wapinzani wakubwa wa Yesu. Unaposoma katika biblia agano jipya utakutana na watu wanaitwa waandishi, makuhani na mafarisayo ambao walikuwa wakimpinga sana Yesu. Imani ya watu hawa haikupotea ila waliendelea na Imani hii na sehemu kubwa ya wanachi wa Israeli waliendelea kuwa waumini wa dini hii. Hata muisraeli asiyekuwa na Imani yoyote ujikuta akijumishwa katika Imani hii. Taifa la Israeli linasisitiza sana uadhimishaji wa sabato sheria za nchi zinazuia kufanya shughuli kazi siku ya sabato, na mwezi wa kwanza 2018 bunge la taifa hilo lilipitisha sheria ya kuzuia biashara siku ya sabato (jumamosi).



2.WAKRISTO WASABATO/ KANISA LA KRISTO LA AWALI

Kundi lingine la wasabato ni lile la wakristo wa awali, Kundi hili lilizaliwa kutoka katika dini ya kiebrania au dini ya kiyahudi, Mwanzilishi wa kundi hili ni Yesu. Wafuasi wa mwanzo kabisa walikuwa mwanzo waumini wa dini ya kiebrania (dini ya taifa la Israeli). Walikuwa wakisali pamoja na juadaism katika masinagogi na mahekalu siku ya sabato (jumamosi) luka 4:16, matendo 13:42-43. Kutokana na kuamini kuwa Yesu ndiye masihi/kristo, kundi hili liletengwa na masinagogi ya kiyahudi (yohana 16:2). Jamii kubwa ya waumini wa kundi hili mwanzoni walikuwa ni wayahudi baadae wakaongezeka na jamii ya mataifa mengine. Wasabato hawa waliendelea kuiheshimu na kuiadhimisha sabato ( matendo 16:13).

Utanzaji wa sabato katika kundi hili ulikuwa tofauti na kundi lile lililo mkataa Yesu; wakati kundi lile lilizuia kuponya siku ya sabato (marko 3:2), kundi hili la wasabato-wakristo liliruhusu kuponya siku ya sabato, Wakati kundi lile lilisisitiza utoaji wa kafara siku ya sabato , kundi la wakristo- wasabato lilipinga utoaji wa kafara. Wakati kndi lile lilisisitiza tohara kama sehemu ya wokovu , kundi hili lilisisitiza tohara ya rohoni na ile ya mwili haikuwa na sehemu katika wokovu

Makundi haya mawili yote yaliiheshimu sabato (jumamosi) lakini yalitofautiana namna ya kuiheshimu.

Kundi hili la wasabato wa kikristo liliendelea kuwepo kwa wingi hadi karne ya tatu( 300 AD), Ambapo katika kusanyiko la Laodikia (Council of Laodicea 363-364) ilipitishwa kwamba wakristo wasiendelee kupumzika siku ya sabato / jumamosi badala yake wapumzike jumapili.( waweza soma wikipedia na vyanzo vingene vya historia kuhusu council of laodicea na malengo yake makuu).

Baada ya maamuzi haya waumini wengi wa kundi hili walihama na kuamua kuwa wajumapili (wanaopumzika siku ya jumapili) , Kundi hili la wasabato wakristo lilififia kiasi cha kuelekea kupotea kabisa maana yeyote aliyetaka kuendelea kuwa msabato alikabiliwa na mkono wa dola (selikali) ,mateso na kuuawa, ndipo wengi walijificha mapangoni na kuabudu kwa siri, kuendesha ibada za siku ya sabato ilikuwa kinyume na matakwa ya serikali ya Rumi.

3. SEVENTHDAY BAPTISTIST,

Kundi hili la wasabato ni matokeo ya vuguvugu la matengenezo huko nchini Uingereza katika miaka ya 1650. Matokeo ya matengenezo yaliyoibuliwa na Martine Lutter mwanzilishi wa lutheran church katika miaka ya 1500 yalileta uamsho mkubwa wa watu kutaka kurudi katika misingi ya Biblia. Japo martine Luther mwenyewe hakupokea fundisho la ubatizo wa maji mengi, wanamatengenezo waliofuta walikuja na fundisho la ubatizo wa maji mengi, Fundisho hili lilipelekea kuzaliwa kwa dhehebu la Baptist church katika miaka ya 1520, Ndani ya hili dhehebu lilijitokeza kundi lingine ambalo liliamua kurudi kwenye sabato ya biblia ambalo ni SEVENTHDAY BAPTIST (SDB). Viongozi wake wa awali kina Mr Andreas Fischer na mke wake walihukumiwa kifo mwaka 1520 na baadaye kuuwa . wafuasi wa kundi hili walikuwa tayari kufa kuliko kuiacha sabato. Oswald Glait ni miongoni mwa wahubiri waloisambaza sabato maeneo ya ulaya , hata hivyo naye alikamatwa na kutupwa mtoni. Kundi hili la SDB lilitambulika kama dhehebu na kufanya mkutano wake wa kwanza uko uingereza mwaka 1651. Kundi hili la wasabato halikufanikiwa kukua sana, Kwa sasa lina waumini karibu 50, 000 wengi wa waumini hawa wapo maeneo ya India na marekani. Kutoka katika kundi hili la wasabato kulikuwa na muumini ,mama mmoja aliyeitwa Rechael Oaks ambaye aliileta sabato kwa kundi la waadventista na kupelekea kuzaliwa kwa wasabato tunaowafahamu waitwao sda.

4.WAADVENTISTA WASABATO (sda)

Kundi hili ndilo limeifufua sabato kwa kiasi kikubwa tangu ilipofifia enzi za mfalme constantine na kuitawanya sehemu kubwa ya dunia. Kundi hili lilizaliwa rasmi kama dhehebu la kikristo mwaka 1863 chini marekani. Waanzilishi wake karibu wote walikuwa ni wajumapili toka madhehebu tofauti kama babtist church, methodist church. Baadhi yao ni kina Joseph bates, James White, Ellen white na J N Andrews. Hawa wote walipokea fundisho la utunzaji wa sabato kutoka kwa mama mmoja iliyekuwa msabato aitwaye Rechael Oaks aliyekuwa muumini wa dhehebu la SEVENTHDAY BAPTIST . Waadiventista walilipokea fundisho la sabato na baadae fundisho kuhusu sabato lilidhibitishwa na maono ya Ellen G white , binti ambaye kipindi hiki alikuwa akipokea maono. Binti huyu alipewa maono na kuoneshwa amri za Mungu kumi la amri ya sabato ilionekana ikingaa sana. Kabla ya maono haya baadhi ya waadiventista walikuwa wameisha pokea fundisho la sabato na kulikubali na walikuwa tayari wameanza kupumzika na kufanya ibada siku ya sabato badala ya jumapili, E G White mwinyewe alikuwa amelipokea fundisho hili tayari.

Utunzaji wa sabato katika kundi hili unafanana kwa karibu sana na namna ulivyofanyika katika kanisa la kristo la awali. Kundi hili ufanya oponyaji siku ya sabato, pia kutembelea wagonjwa na waitaji siku ya sabato ni jambo linaloruhusiwa. Kundi hili linaitunza sabato katika kumtazama Yesu na wanafunzi wake walichokifanya siku ya sabato. Kama kuna shughuli yoyote ambayo Yesu aliifanya siku ya sabato basi shughuli hiyo ni halali kufanyika siku ya sabato katika kikundi hiki.

Kundi hili la wasabato ndo kundi pekee miongoni mwa makundi ya wasabato ambalo limefanikiwa kukua na kusambaa duniani karibu kila nchi japo zipo nchi ambazo halijawa na uongazi lakini waumini wapo.

 Kwa ufupi nadhani umeelewa maana ya wasabato, na umefahamu makundi ya wasabato na tofauti zao. Somo hili liwasaidie wale wanaochanganya wasabato waliomkataa Yesu na wasabato wafuasi wa Yesu.

(Marko 2: 27-28) Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
 
*STAAJABIKA NA UFILIPINO.*



Huenda ukiulizwa kuhusu Filipino utamtaja Manny Pacquiao, Neno Philipine linatokana na Mfalme Philip wa Uspanish (King Philip) aliyewahi kuishi kwenye viswa hivyo na kuzaana, wafilipino wengi wana asili ya Uspain -The islands were dubbed "the Philippines" afterKing Philip II of Spain.

Ufilipino ndio nchi inayokabiliwa na hatari kubwa ya kukumbwa na vimbunga vya Kitropiki kote ulimwenguni.

Kimbunga Haiyan ni mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya asili kuwahi kuikumba Ufilipino, lakini siyo janga pekee, nchi hiyo ya Kusini mwa Asia iko katika eneo linalokabiliwa na kitisho kikubwa cha vimbunga.

Unataka Kusheherekea sikukuu ya Noeli hadi ukinai? Ufilipino siku ya Noel (Chrismass) Husherekewa tangu Septemba Mosi hadi Januari Mosi na ndiyo sherehe ndefu kuliko zote duniani kusheherekewa na nchi mojaNi nchi ya pili kwa ukubwa wa visiwa duniani (archipelago) NCHI HII INA VISIWA 7,500 na kati ya hivyo ni visiwa 200tu ndivyo hukaliwa na watu ilihali visiwa 5000 bado havijaewa majina.

Asilimia 11 ya Raia wa Ufilipino wanafanya kazi ughaibuni, ukweli ni kwamba Filipino ndiyo nchi inayoongoza kutoa wauguzi wengi duniani yaani 25% ya wauguzi wote duniani wanatoka Ufilipino, uwapo Marekani, ukiacha wachina, Wafilipino wanafuatia kwa wingi wa Wahindi Kiasili waliopo USAFilipino inaongoza kwa nazi duniani ikiuza wastani wa tani milioni 20 za nazi kwa mwaka
Kuna utititiri wa Wafilipino kwa idadi ya watu, mnamo mwaka 2014 walifikisha mtoto wa milioni 100 duniani na ni nchi ya 12 kwa idadi ya watu dunianiBendera ya Ufilipino inatakiwa kuwekwa kwa umakini mkubwa sana, kwa sheria za Philipine ni kosa kubwa kuigeuza bila muktadhawa wakati husika kwani Bendera ya nchi hiyo inaweka tofauti wakati wa amani na wakati wa vita Kusanyiko kubwa zaidi la kidini lilifanyika mnamo mwaka 1995 ambapo Papa John Paul II alikutanisha wakristo zaidi ya milioni 5.....kutokana na asili ya Uspain zaidi ya 90% YA Wafilipino NI WAKATOLIKI.

Ni nchi tata sana kwa viongozi kupinduliwa kutokana na kujisahau waingiapo madarakani. Kama unamkumbuka Ferdinand Marcosi aliyeingia madaakani akiwa Mlokole na kula bata Ikulu kama atakavyo, Mkewe Imelda anasaidkiwa kuwa na pea 3000 za viatu yaani akivaa kila siku anaweza kumaliza mwaka HAJAVIMALIZA, As first lady of the Philippines for more than 20 years, Imelda Marcos was known for her extravagant and opulent lifestyle, including her special love for shoes.... When protestors stormed Malacanang Palace, it was famously discovered that more than 2,700 pairs of shoes had been left behind in Imelda's ... Imelda Marcos' legendary 3,000 plus shoe collection destroyed by termites, floods and neglect | Daily Mail OnlineNi nchi yenye malaya wengi duniani walio ughaibuni wakikadiriwa kuwa zaidi ya LAKI NNE wanaifanya biashara ya ngono wengi wao wakwa kati ya miaka 15 hadi 20 ingawa wapo walio chini ya miaka 11 pia -It has the fourth largest number of children who are prostituted in the world
Social media is important to Filipinos.

The Philippines is now considered the text capital of the world. With more than 450 million SMS messages sent by the residents daily, they surpass the daily texts sent in Europe and the U.S. combined.
 
HIVI NDIVYO SHUJAA SAMORA MACHEL ALIVYOUAWA, HAKIKA WEMA HAWADUMU.

Samora Moisés Machel alizaliwa tarehe 29 Septemba,1933 katika kijiji cha Madragoa (kwa sasa Chilembene), mkoa wa Gaza nchini Msumbiji au Mozambique. Alikuwa Kamanda wa Jeshi la Msumbiji, Mwanamapinduzi, Mjamaa na mwenye msimamo mkali wa Kimarx na Kilenin aliyeiongoza nchi ya Msumbiji tangu uhuru wake mwaka 1975 hadi kifo chake kilichotokea usiku wa tarehe 19 Oktoba 1986 katika eneo la milima la Mbuzini, mpakani mwa Msumbiji, Swaziland na Afrika Kusini.

Katika harakati za kupigania uhuru wa Msumbiji kutoka kwa wakoloni wa Kireno, Samora Machel alihudhuria mafunzo ya kijeshi ya kujitolea mjini Dar es Salaam na baadaye alikuwa ni miongoni mwa wapiganaji wa chama cha FRELIMO waliopelekwa nchini Algeria kwa ajili ya mafunzo zaidi. Aliporejea Tanzania kutoka Algeria, Samora Machel aliteuliwa kuongoza kambi ya mafunzo ya wapigania uhuru wa FRELIMO iliyokuwa KONGWA mkoani Dodoma.

Baada ya FRELIMO kuanzisha vita vya kudai uhuru wa Msumbiji tarehe 25 Septemba, 1964, Samora Machel alitokea kuwa Kamanda mahiri na muhimu sana katika mapambano hayo ambaye jina lake lilivuma kwa kasi mno miongoni mwa Makamanda na wapigania uhuru wa FRELIMO kutokana na umahiri wake katika medani. Na kutokana na umahiri huo, alipanda vyeo kwa haraka ndani ya jeshi la wapigania uhuru wa msituni lililokuwa likijulikana kama FPLM hadi kufikia cheo cha Kamanda wa Jeshi baada ya Kamanda wa Kwanza wa Jeshi hilo, Filipe Samuel Magaia, kufariki mwaka 1966. Na katika uchaguzi wa mwaka 1970, Samora Machel alichaguliwa kuwa Rais wa FRELIMO.

Kamanda mpya wa Jeshi la Kireno la Msumbiji, Jenerali Kaúlza de Arriaga, alitamba kuwa angewasambaratisha na kuwaangamiza kabisa wapiganaji wa FRELIMO kwa muda wa miezi michache tu lakini hakufua dafu licha ya kuanzisha mashambulizi makali mno katika mpango wake wa Operation Gordian Knot mwaka 1970 akielekeza mashambulizi zaidi katika ngome za FRELIMO zilizokuwa Cabo Delgado kaskazini ya mbali ya Msumbiji. FRELIMO chini ya Samora Machel ilijibu mapigo na kuhimili vishindo hivyo ambapo ilianza mashambulizi kutoka kila upande na kuelekeza nguvu upande wa magharibi mwa nchi katika mkoa wa Tete. Mpaka kufikia mwaka 1974, Wareno walikuwa hoi bin taaban katika uwanja wa mapambano.
Baada ya kupigwa vya kutosha, Wareno walikubali kutia saini makubaliano tarehe 7 Septemba, 1974 mjini LUSAKA kwa ajili ya kukipa mamlaka kamili chama cha FRELIMO na tarehe rasmi ya Uhuru wa Msumbiji ikapangwa iwe 25 Juni, 1975. Serikali ya mpito iliundwa ikiwa na Baraza la Mawaziri lililojumuisha FRELIMO na Wareno ikiongozwa na Waziri Mkuu JOACHIM CHISSANO. Samora Machel aliendelea kuongoza akiwa Tanzania hadi aliporejea nyumbani Msumbiji kishujaa katika safari iliyoitwa “KUTOKA RUVUMA MPAKA MAPUTO”.

Siku ya tarehe 19 Oktoba, 1986, Rais SAMORA MACHEL alikwenda kuhudhuria mkutano mjini Mbala, Zambia, ulioitishwa kumshinikisha Dikteta MOBUTU SESE SEKO wa Zaire juu ya uungaji wake mkono kwa chama cha upinzani cha Angola cha UNITA. Mkakati wa nchi zilizokuwa Mstari wa Mbele ulikuwa ni kupingana na Mobutu Sese Seko na Hastings Kamuzu Banda katika nia ya kumaliza kabisa uungaji wao mkono kwa UNITA na RENAMO, vyama au makundi ambayo nchi hizo ziliyaona kama wasaidizi au vibaraka wa Afrika Kusini.

Japokuwa mamlaka za Zambia zilikuwa zimemwalika Samora Machel kukaa mjini Mbala usiku mzima, yeye alisisitiza kurejea Maputo usiku uleule kwa kuwa asubuhi yake, alikuwa amepanga kuwa na kikao chenye lengo la kufanya mabadiliko katika uongozi jeshini. Kutokana na umuhimu wa kikao hicho kilichokuwa kimepangwa kifanyike asubuhi yake, Samora Machel alikiuka hata maelekezo ya Wizara ya Usalama kwamba Rais hakupaswa kusafiri usiku.

Na kweli Samora Machel aliondoka usiku wa tarehe 19 Oktoba, 1986 kwa ndege kurejea Maputo, lakini kwa bahati mbaya hakuweza kuiona tena Maputo kama alivyokuwa amepanga. Ndege yake ilianguka eneo la milima la Mbuzini mpakani mwa Msumbiji, Swaziland na Afrika Kusini, tena upande wa ndani ya Afrika Kusini; yeye Kamanda Samora Machel na watu wengine 33 walipoteza maisha huku watu 9 waliokuwa wamekaa viti vya nyuma ya ndege wakinusurika. Inaaminiwa kwamba ndege yake ilidunguliwa na utawala wa Kibaguzi wa Afrika Kusini wa wakati huo. Safari ya mwisho ya maisha ya Samora Moisés Machel wa Msumbiji ikawa imeishia hapo.

#FOLLOW UKURASA HUU KWA HABARI MAKINI ZAIDI
 
HII NDIYO SIRI YA KWA NINI MWALIMU NYERERE HAKUWA AKITHUBUTU KUVIACHA VIFIMBO VYAKE.

Unapofika katika nyumba yake iliyopo jijini Dar es Salaam maeneo ya Msasani maarufu kwa Mwalimu Nyerere, kinachoyatofautisha maisha ndani ya nyumba hiyo na zile za Magomeni na Ilala ni mazingira nadhifu.

Si urithi wa mali, isipokuwa ni mapenzi kwa binadamu wenzake na hekima ambavyo, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameviacha katika vitabu, maandiko mbalimbali na kwa familia Yake.

Wenyeji ndani ya nyumba hii kwa mwonekano na mazungumzo hawana tofauti na Watanzania wa kawaida, hawana majivuno na wanamkaribisha mgeni kama ndugu au jamaa waliyemfahamu miaka mingi.

Pamoja na kuwa nyumba ni kubwa na wenyeji ni wengi, lakini kwenye maegesho ya magari lipo gari moja tu. Mwonekano wa nje wa nyumba hii unaweza kukufanya ufikiri ndani kuna magari zaidi ya matatu tena ya kifahari.

Wanafamilia ni wakarimu sana, kwa kawaida ungetarajia kusikia wenyeji wakitumia maneno kama "Yes, No" na maneno mengine ya Kiingereza kwa kuwa hiki ni kitambulisho cha vijana waliopata elimu angalau ya sekondari, lakini hapa ni tofauti, wote wanazungumza Kiswahili na bahati mbaya wakichanganya huwa ni lugha ya Kizanaki.

Wajukuu wa Baba wa Taifa, Moringe Magige na Julius Makongoro wanasema huu ndiyo urithi ambao Baba wa Taifa aliwaachia ndugu zake wakisema kuwa walilelewa kuamini kuwa mali siyo kitu kuliko utu na ndivyo walivyo.

MAISHA YA MWALIMU NYERERE KAMA BABU.

Wengi tunafahamu historia ya Baba wa Taifa hasa katika majukumu yake ya uongozi wa Tanzania na ukombozi wa bara la Afrika, lakini Moringe na Julius wanaturudisha nyumbani wakisimulia walivyomfahamu babu yao.

Moringe anasimulia akisema; "Kwanza mimi sikufahamu kwa jinsi gani babu alikuwa mtu muhimu katika nchi hii na bara la Afrika kwa ujumla, nilijua baada ya kufariki dunia na kuanza kusoma historia yake na kugundua vitu vingi alivyofanya,"

"Sikuiona tofauti yake na mababu wengine kwani shuleni nilisikia watu wakisimulia jinsi walivyoishi na babu zao na sikuona tofauti na babu yangu," anasema Moringe.

Anasema Mwalimu Nyerere aliwapenda wajukuu zake, alipenda kufanya shughuli za shamba akiwa na wajukuu zake, hakutaka hata mmoja azembee kwenda shambani.

"Babu aliipenda familia yake, tumeishi na ndugu wengi kwa sababu hakutaka kukaa mbali na ndugu zake na kila mmoja alihakikisha anapata wasaa wa kukaa naye na kuzungumza naye, mfano alikuwa na utaratibu wa kula chakula cha jioni na sisi wajukuu zake," anasema Moringe. Aidha anasema kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa akiwahimiza kuongeza juhudi shuleni hasa katika masomo ya Kiingereza na Hisabati.
"Babu alikuwa akifuatilia maendeleo yetu shuleni, kila mwisho wa muhula alikagua matokeo ya kila mmoja wetu na alikuwa akisisitiza zaidi masomo ya Kiingereza na Hesabu akisema hayo ndiyo ya msingi," anasema Moringe.

Alikuwa anapenda kupiga makonzi

Kila mtu anakumbuka adhabu gani alikuwa anapewa na bibi au babu yake pale anapokosea, lakini Julius anatuambia kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa akiwapiga makonzi wajukuu zake pale wanapokosea.

Julius anasema adhabu kubwa waliyokuwa wakipewa na babu yao ni kupigwa makonzi hata hivyo utaokoka tu kwa juhudi zako za kutoka mbio kwani ukisimama anaendelea kukupiga. "Babu alikuwa na tabia ya kutupiga makonzi hasa ukiwa mtundu au ukimpitia karibu wakati anacheza bao lazima atakupiga japo konzi moja," anasema.

Pia anasema kamwe hatasahau siku moja alipomuomba babu yake akaangalie mkanda wa video mchana;" Nilimwambia babu tunaomba kuangalia mkanda kwa sababu Tv ilikuwa inakaa Maktaba, alinikubalia na kuniambia nenda ukawaite na wenzako unaotaka kuangalia nao. Basi nikaenda kuwaita tulivyofika alitufungia na kuanza kutupiga makonzi ," anasema Julius.

Aidha anasema babu yao aliwapangia muda maalumu wa kuangalia televisheni pia aliwachagulia mikanda ya kutazama kwa kuwa alipenda wawe na maadili mema.

Vituko,utani wa babu na wajukuu zake

Pamoja na kuwapiga makonzi wajukuu zake lakini kuna wakati alikuwa akiketi chini na kufanya utani na kushuhudia vituko vya wajukuu zake.

Moringe anasema moja kati ya maswali ya utani waliokuwa wakimuuliza babu yao ni iwapo enzi za ujana wake alikuwa akifanya starehe za aina mbalimbali.

"Tulikuwa tunamuuliza babu hivi unajua kuogelea au kucheza muziki kwa sababu hatujawahi kukuona hata siku moja ukicheza, alijibu 'siwezi', tukawa tunamuuliza sasa wewe ujana wako ulikuwa unafanya nini, alisema 'kusoma tu', anasema Moringe.

Aidha wanasema utani mwingine kwa babu yao ilikuwa ni kuwa hajui kuendesha gari. Julius anasema "Tangu nimepata akili sijawahi kumuona akiendesha gari, nina wasiwasi alikuwa hajui kuendesha". Julius pia anasema babu yake hakuwa na mazoea sana ya kuvaa suti au kuchomekea huku akisema inawezekana zamani alikuwa analazimishwa kuvaa hivyo. "Sijawahi kumuona babu amevaa suti au amechomekea shati, hata hakupenda ndugu wavae suti hasa tukiwa Butiama, alipenda kuvaa 'simple'.
Alisisitiza maadili.

Moringe na Julius wanasema wanaamini babu yao alikuwa akilinda maadili kwa kutowaachia watazame televisheni ovyo na kuwahimiza kushiriki kanisani.

"Babu hakuwa na mchezo linapokuja suala la kanisani, yaani usipoenda kanisani ni ugomvi mkubwa anaweza hata kukufukuza usile naye chakula cha jioni," anasema Moringe.

Wakizungumzia iwapo Baba wa Taifa angekuwa hai leo angebariki matumizi ya mitandao ya kijamii kama 'facebook' na 'twitter' kwa pamoja walisema asingepinga kwani alikuwa mpenda maendeleo.

"Watu wengi huwa wanazungumza wakisema kuwa babu alikuwa hataki watu waendelee kwa kutumia teknolojia, sio kweli, babu alikuwa anapenda maendeleo lakini aliheshimu utamaduni," anasema Julius.

Akitolea mfano wa dada yao mmoja aliyekuwa akiishi Ulaya walisema, babu yao hakuwa na tatizo na mavazi yake lakini alimwonya kuwa ni lazima aangalie anavaa wapi.

"Mfano tukiwa hapa Msasani babu hakumkataza kuvaa nguo zake anazopenda, lakini tulipoenda Butiama alikuwa akimrudisha pale anapovaa nguo anazoona haziendani na utamaduni wa watu wa kule," anasema Julius.

Anaongeza kuwa Mwalimu asingekuwa na tabu na mitandao hiyo au teknolojia yoyote isipokuwa pale itakapotumikwa visivyo kama wafanyavyo wengi.

"Ukiukwaji wa maadili unaotokana na teknolojia unawakwaza watu wengi, watu wanatumia ndivyo sivyo na hiki pengine kingemkera babu," anasema Julius.

Siri ya kifimbo cha babu yao

Moringe na Julius wanasema wamesikia hadithi nyingi kuhusu kifimbo cha Mwalimu Nyerere alichokuwa akipenda kukibeba, wengine wamediriki kusema alizikwa nacho. Julius anasema kwanza wanavyofahamu wao babu yao alikuwa nazo zaidi ya nne, nyingine alinunua mwenyewe na nyingine alipewa zawadi.
"Babu alikuwa na fimbo nyingi, alibeba yoyote anapotoka nyumbani, wakati mwingine aliweza kuisahau na kutuagiza tumpelekee nje kama ameshatoka," anasema Julius.

Aidha Moringe anasema amewahi kusikia kuwa asili ya babu yao kutembea na fimbo hiyo ilitokana na nia yake ya kuacha kuvuta sigara. "Niliwahi kusikia babu alikuwa akivuta sigara, sasa alipotaka kuacha alipewa fimbo kama njia mbadala ya kushika kitu mkononi ili aweze kuacha," anasema Moringe.

#Credits kwa Mwananchi.

#FOLLOW UKURASA HUU KWA HABARI MAKINI ZAIDI
 
Back
Top Bottom