HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
- Thread starter
- #41
*HISTORIA YA KIGOMA UJIJI NA ASILI YA KABILA LA WAHA.*
Wakati miji mingine ikipata majina kutokana na ujio wa wageni, kuna baadhi ya miji ilipata majina yake kutokana na Waafrika wenyewe. Na kutaja majina kutokana na wenyeji kulitegemea sana watu, hasa wale waliokuwa maarufu kwenye jamii. Na ile miji iliyopata majina kutokana na wageni, sababu ilikuwa ni kujiwekea sifa kwa mataifa hayo na wakati mwingine mitazamo tu ya wageni hao ilisababisha mji fulani kupata jina.
Kwa upande wa mji kama Ujiji na Kigoma, watu huamini kuwa miji hii ilipata kukua katika kipindi cha ukoloni. Ukweli ni kwamba Ujiji na Kigoma ilipata kukua kwa muda mrefu sana hata kabla ya ujio wa wageni kwenye maeneo hayo.
Kihistoria miji hii ilipata majina kutokana na watu maarufu waliopata kuishi na kujiwekea historia katikia miji hiyo.
Watu wengi hudhani kuwa mji wa Kigoma na Ujiji ilianzishwa na ndugu wawili waliofahamika kwa majina ya Kajiji na Kagoma *(Bugoye)*.
Ifahamike tu kwamba kabla ya mji wa Kigoma kuitwa Kigoma palikuwa panaitwa *Lusambo Gwa Nyange* na Ujiji palikuwa panaitwa *Ubujiji.*
Inaelezwa kuwa bwana *Kajiji* alikuwa mkarimu , mpole na mwenye upendo kwa watu wote. Na Kagoma alionekana kuwa tofauti kwa jamii. Kutoka na tabia hizo za ndugu hao wawili, wengi walimpenda sana Kajiji na kufanya maeneo aliyokuwa akiishi bwana Kajiji kupendwa na watu wengi. Na kwa kuwa idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka, basi walipokuwa wakienda kwa kajiji wakasema tunaenda *Ubujiji* kulingana na lugha ya kikabila.
Na wengi walikuwa wanapenda kwenda Ubujiji na kujikuta wakijazana kwenye mji huo. Na hata wageni walipoingi kwenye miaka ya 1800, walikuta mji huo una idadi kubwa sana ya watu. Na kwa kuwa wakati huo Waarabu hawakuwa na nguvu sana hawakukutana kubadilisha jina hilo na badala yake waliamua kuendeleza mji huo na jina hilo.
Na hata mpaka ukoloni ukianzishwa bado eneo hilo lilikuwa na jina hilo, isipokuwa kukawa na mabadiliko katika kiothografia na matamshi ya neno Ubujiji.
Na hapo ndipo tukapata jina *Ujiji.*
Na hata kwenye maandiko ya wakati huo ulitambulisha mji huo kama Ujiji.
Kwa upande wa Kagoma au Bugoye pia mambo yalikuwa hivyo, sema kwa upande wa Kagoma, mji ulipata kukua kutokana na ujio wa *Wagoma* katika mji wa bwana Kagoma.
Ikumbukwe kuwa Wagoma ni moja ya kabila la kimanyema waliokuja tanganyika kipindi cha ukoloni Karne ya 18. Lakini sultani wao wagoma alikuwa akiitwa *Sultan Simba.*
Na mara baada ya Wagoma hao kusikia mji huo unaitwa Kigoma, walijisikia raha sana kwani mji ulikuwa unafanana na jina la kabila lao. Na hivyo kujikuta wakiupenda na kuanza kuujenga mji. Na ile sehemu aliyokuwa akikaa bwana Kagoma au Bugoye palifahamika kwa jina la Ibugoye ambapo kwa sasa ndio pale *Mwanga.* Lakini Kiuhalisia Wagoma walifikia Maeneo ya Bangwe.
Na kwa kuwa ardhi ya Ujiji ilikuwa yenye rutuba, Wagoma walipenda kulima maeneo ya Ujiji. Kwa hiyo mji wa *Kigoma na Ujiji ni miji ambayo ilijipatia historia ya pekee barani Afrika, kwani miji hiyo imepata majina yenye asili yake hapa hapa Afrika.*
Ikumbukwe kwamba wagoma ni Kabila La wamanyema... Kwasababu Wamanyema ni Mkusanyiko wa makabila zaidi ya 18 yaliyoungana na kuwa kitu kimoja.
Pia wamanyema walipofika Kigoma Kuna ambao walipata majina katika miji kama Katonga, Kabwe, Mkabogo au Kabogo hao wote walikuwa ni wamanyema wenye Asili ya DRC.
Pia Waha waliokuwa Kigoma na ujiji waliwapokea watani wao wamanyema na kuanza kuishi pamoja mpaka sasa.
*Asili ya kabila la Waha.*
Historia ya waha ilianzia katika kijiji kiitwacho *Buha* kilichopo *Heru* hapo ndipo waha walipofikia baada ya kutoka maeneo ya *Burundi, Rwanda na Kongo.* Asili ya Waha ni watu kutoka Burundi, Rwanda na Kongo, kama ilivyo kwa wamanyema asili yao ni Kongo.
Inafahamika kuwa waha au kabila la *Ha* ni moja ya kabila kutoka Wabantu wa mashariki. Wabantu hawa walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600 yaani kabla ya wamanyema.
Na ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona.
Na kuna makabila yalipata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliopata majina namna wanavyopiga makelele na wangine walipewa majina kulingana na lugha yao au matamshi yao. Kwa upande wa kabila la Waha ambao wengi tunafahamu kuwa wanapatikana katika mkoa wa Kigoma.
Ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa kabila ambalo lina historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo na pia ni kablia lenye umaarufu mkubwa hapa nchini..
Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya Afrika mashariki hawakujulikana kama kabila la (Ha) na hawakuja wakiwa na kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa Koo au ukoo. Na kila ukoo ulikuwa na jina lake.
Ukoo au koo zilizokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. Na cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuitwa majina ya maeneo waliyokaa kutokana na mazingira yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye uongo (Bayungu) walijiita *Wayungu* na wale waliokaa sehemu za mwinuko(Heru) walijiita *Wanyaheru.* Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na chifu mmoja.
Na hapo ndipo watu hao walianza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni.
Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha?
Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno *Waha au Ha.*
*1.* Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale wageni walipofika katika ardhi ya Kigoma na kuwauliza watu hao kuwa “ ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha “ sisi ni wazaliwa wa hapa hapa. Na hapo wageni hao walikalili kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”,,,, Kiuhalisia waha na wamanyema ni Watu wamoja tangu enzi na enzi walipendana na kuthaminiana.
*2.* Wapo wanaodai kuwa wageni walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekuwa na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza mfalme wao kuwa “hawa ni wakina nani” na ndio mfalme wa Buha alipojibu kuwa “N’abhaha” akimaanisha kuwa “ hawa ni wenyeji wa hapa hapa” na hapo wageni hao walipata neno “Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.
Maelezo haya yalitolewa kwa mujibu wa watu walikuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa, Watusi walikuwa watawala wa kabila la Waha.
Na kuna mahususiano makubwa sana kati ya Watusi na Waha. Na hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.
*Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mtoke. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha.*
*Na waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha” na hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “ Waha” na ndio maana hata walivyotawala walijiita hivyo.*
Wamanyema na Waha Ndio wenyeji wa kigoma. Uwenyeji huu tunauzungumza ni miaka ya zamani sana hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja... na walikuwa wakipendana na kuthaminiana na kuna vitu Waha waliwafundisha wamanyema na pia kuna vitu wamanyema waliwafundisha waha na wote hawa waliipigania Tanganyika Kutoka mikononi mwa serekali ya kikoloni. Kwa mfano *Iddi_Faiz* ni mmanyema ambae hatuwezi kumsahau kwasababu yeye ndie aliyekuwa muweka hazina wa chama cha TANU
Hata kuligawa bara la Afrika Scramble For Africa ilikuwa bado kabisa wamanyema na waha walikuwa wakiishi pamoja .. na Ikumbukwe uhuru wa nchi hii hatuwezi kumsahau *Mwami Thereza Ntare* malkia wa Waha na chifu mwanamke wa kasulu ambae aliipigania nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni na likawa Taifa huru.
*Sisi Ndio Watanzania na sisi ndio mwisho wa Reli na Tunaposema Mwisho wa Reli tunamaanisha reli ndipo ilipoishia kutengenezwa huku. Heshima imfikie Mtu mwenye asili ya Kigoma.*