Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

*HISTORIA YA KIGOMA UJIJI NA ASILI YA KABILA LA WAHA.*

Wakati miji mingine ikipata majina kutokana na ujio wa wageni, kuna baadhi ya miji ilipata majina yake kutokana na Waafrika wenyewe. Na kutaja majina kutokana na wenyeji kulitegemea sana watu, hasa wale waliokuwa maarufu kwenye jamii. Na ile miji iliyopata majina kutokana na wageni, sababu ilikuwa ni kujiwekea sifa kwa mataifa hayo na wakati mwingine mitazamo tu ya wageni hao ilisababisha mji fulani kupata jina.

Kwa upande wa mji kama Ujiji na Kigoma, watu huamini kuwa miji hii ilipata kukua katika kipindi cha ukoloni. Ukweli ni kwamba Ujiji na Kigoma ilipata kukua kwa muda mrefu sana hata kabla ya ujio wa wageni kwenye maeneo hayo.

Kihistoria miji hii ilipata majina kutokana na watu maarufu waliopata kuishi na kujiwekea historia katikia miji hiyo.

Watu wengi hudhani kuwa mji wa Kigoma na Ujiji ilianzishwa na ndugu wawili waliofahamika kwa majina ya Kajiji na Kagoma *(Bugoye)*.

Ifahamike tu kwamba kabla ya mji wa Kigoma kuitwa Kigoma palikuwa panaitwa *Lusambo Gwa Nyange* na Ujiji palikuwa panaitwa *Ubujiji.*

Inaelezwa kuwa bwana *Kajiji* alikuwa mkarimu , mpole na mwenye upendo kwa watu wote. Na Kagoma alionekana kuwa tofauti kwa jamii. Kutoka na tabia hizo za ndugu hao wawili, wengi walimpenda sana Kajiji na kufanya maeneo aliyokuwa akiishi bwana Kajiji kupendwa na watu wengi. Na kwa kuwa idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka, basi walipokuwa wakienda kwa kajiji wakasema tunaenda *Ubujiji* kulingana na lugha ya kikabila.

Na wengi walikuwa wanapenda kwenda Ubujiji na kujikuta wakijazana kwenye mji huo. Na hata wageni walipoingi kwenye miaka ya 1800, walikuta mji huo una idadi kubwa sana ya watu. Na kwa kuwa wakati huo Waarabu hawakuwa na nguvu sana hawakukutana kubadilisha jina hilo na badala yake waliamua kuendeleza mji huo na jina hilo.

Na hata mpaka ukoloni ukianzishwa bado eneo hilo lilikuwa na jina hilo, isipokuwa kukawa na mabadiliko katika kiothografia na matamshi ya neno Ubujiji.

Na hapo ndipo tukapata jina *Ujiji.*
Na hata kwenye maandiko ya wakati huo ulitambulisha mji huo kama Ujiji.

Kwa upande wa Kagoma au Bugoye pia mambo yalikuwa hivyo, sema kwa upande wa Kagoma, mji ulipata kukua kutokana na ujio wa *Wagoma* katika mji wa bwana Kagoma.

Ikumbukwe kuwa Wagoma ni moja ya kabila la kimanyema waliokuja tanganyika kipindi cha ukoloni Karne ya 18. Lakini sultani wao wagoma alikuwa akiitwa *Sultan Simba.*

Na mara baada ya Wagoma hao kusikia mji huo unaitwa Kigoma, walijisikia raha sana kwani mji ulikuwa unafanana na jina la kabila lao. Na hivyo kujikuta wakiupenda na kuanza kuujenga mji. Na ile sehemu aliyokuwa akikaa bwana Kagoma au Bugoye palifahamika kwa jina la Ibugoye ambapo kwa sasa ndio pale *Mwanga.* Lakini Kiuhalisia Wagoma walifikia Maeneo ya Bangwe.

Na kwa kuwa ardhi ya Ujiji ilikuwa yenye rutuba, Wagoma walipenda kulima maeneo ya Ujiji. Kwa hiyo mji wa *Kigoma na Ujiji ni miji ambayo ilijipatia historia ya pekee barani Afrika, kwani miji hiyo imepata majina yenye asili yake hapa hapa Afrika.*

Ikumbukwe kwamba wagoma ni Kabila La wamanyema... Kwasababu Wamanyema ni Mkusanyiko wa makabila zaidi ya 18 yaliyoungana na kuwa kitu kimoja.

Pia wamanyema walipofika Kigoma Kuna ambao walipata majina katika miji kama Katonga, Kabwe, Mkabogo au Kabogo hao wote walikuwa ni wamanyema wenye Asili ya DRC.

Pia Waha waliokuwa Kigoma na ujiji waliwapokea watani wao wamanyema na kuanza kuishi pamoja mpaka sasa.

*Asili ya kabila la Waha.*

Historia ya waha ilianzia katika kijiji kiitwacho *Buha* kilichopo *Heru* hapo ndipo waha walipofikia baada ya kutoka maeneo ya *Burundi, Rwanda na Kongo.* Asili ya Waha ni watu kutoka Burundi, Rwanda na Kongo, kama ilivyo kwa wamanyema asili yao ni Kongo.

Inafahamika kuwa waha au kabila la *Ha* ni moja ya kabila kutoka Wabantu wa mashariki. Wabantu hawa walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600 yaani kabla ya wamanyema.

Na ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona.
Na kuna makabila yalipata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliopata majina namna wanavyopiga makelele na wangine walipewa majina kulingana na lugha yao au matamshi yao. Kwa upande wa kabila la Waha ambao wengi tunafahamu kuwa wanapatikana katika mkoa wa Kigoma.

Ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa kabila ambalo lina historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo na pia ni kablia lenye umaarufu mkubwa hapa nchini..

Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya Afrika mashariki hawakujulikana kama kabila la (Ha) na hawakuja wakiwa na kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa Koo au ukoo. Na kila ukoo ulikuwa na jina lake.

Ukoo au koo zilizokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. Na cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuitwa majina ya maeneo waliyokaa kutokana na mazingira yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye uongo (Bayungu) walijiita *Wayungu* na wale waliokaa sehemu za mwinuko(Heru) walijiita *Wanyaheru.* Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na chifu mmoja.

Na hapo ndipo watu hao walianza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni.

Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha?

Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno *Waha au Ha.*

*1.* Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale wageni walipofika katika ardhi ya Kigoma na kuwauliza watu hao kuwa “ ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha “ sisi ni wazaliwa wa hapa hapa. Na hapo wageni hao walikalili kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”,,,, Kiuhalisia waha na wamanyema ni Watu wamoja tangu enzi na enzi walipendana na kuthaminiana.

*2.* Wapo wanaodai kuwa wageni walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekuwa na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza mfalme wao kuwa “hawa ni wakina nani” na ndio mfalme wa Buha alipojibu kuwa “N’abhaha” akimaanisha kuwa “ hawa ni wenyeji wa hapa hapa” na hapo wageni hao walipata neno “Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.

Maelezo haya yalitolewa kwa mujibu wa watu walikuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa, Watusi walikuwa watawala wa kabila la Waha.

Na kuna mahususiano makubwa sana kati ya Watusi na Waha. Na hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.

*Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mtoke. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha.*

*Na waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha” na hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “ Waha” na ndio maana hata walivyotawala walijiita hivyo.*

Wamanyema na Waha Ndio wenyeji wa kigoma. Uwenyeji huu tunauzungumza ni miaka ya zamani sana hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja... na walikuwa wakipendana na kuthaminiana na kuna vitu Waha waliwafundisha wamanyema na pia kuna vitu wamanyema waliwafundisha waha na wote hawa waliipigania Tanganyika Kutoka mikononi mwa serekali ya kikoloni. Kwa mfano *Iddi_Faiz* ni mmanyema ambae hatuwezi kumsahau kwasababu yeye ndie aliyekuwa muweka hazina wa chama cha TANU

Hata kuligawa bara la Afrika Scramble For Africa ilikuwa bado kabisa wamanyema na waha walikuwa wakiishi pamoja .. na Ikumbukwe uhuru wa nchi hii hatuwezi kumsahau *Mwami Thereza Ntare* malkia wa Waha na chifu mwanamke wa kasulu ambae aliipigania nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni na likawa Taifa huru.

*Sisi Ndio Watanzania na sisi ndio mwisho wa Reli na Tunaposema Mwisho wa Reli tunamaanisha reli ndipo ilipoishia kutengenezwa huku. Heshima imfikie Mtu mwenye asili ya Kigoma.*
 
*HII NDIYO BIBLIA YA SHETANI (THE CODEX GIGAS).*



The Codex Gigas au kwa kiswahili maana yake ni *kitabu kikubwa*, ndiyo kitabu kikubwa Zaidi kuwahi kuandikwa duniani tangu medieval periods (karne za kumi kumi).




The codex Gigas kina ukubwa wa (urefu sm 92, upana sm 22) na uzito wa kilogramu 75. Kitabu hichi pia *kinaitwa “Devil’s bible” au biblia ya shetani* kutokana na historia yake.




Katikati ya kitabu hiki cha maajabu kuna picha kubwa ya malaika wa zamani aliyetupwa yaani *ibilisi* ambayo inaongeza utata juu ya kitabu hichi kikongwe.





Kitabu hiki kiliundwa mnamo karne ya 13 mwanzoni huko monastery of podlacize ndani ya mji ambao kwa sasa unaitwa *Czech Republic.*





Ndani ya kitabu hichi kuna biblia ya kiitaliano (latino) inayoitwa *Vulgate Bible* ikiwa ndiyo biblia ya kwanza kwa lugha ya kiitaliano mwishoni mwa karne ya 4 ambayo baadae ndiyo ilikuwa biblia halisi ya *kikatoliki.*





Vitabu vingine mashuhuri vilivyomo katika codex gigas ni pamoja na *baadhi ya maandishi ya agano jipya na agano la kale la biblia ya wakristo wengine pamoja na medica books au vitabu vya uganga.*





Baada ya miaka mingi kupita baada ya kuandikwa kitabu hiki, kilifika katika maktaba ya *Prague* ambao ndiyo mji mkuu wa Jamhuri ya Czech, ambapo baada ya vita iliyoitwa *“thirty years’ war”,* maktaba hiyo iliharibiwa vibaya na vitabu vingi kupotea, pia na codex gigas nayo ilipata madhara lakini ilisalimika haikuweza kuungua baada ya mtu mmoja asiyejulikana *kuibeba na kuitupia dirishani nje ya maktaba ambapo ilianguka juu ya mtu ambaye alikuwa amesimama chini ya maktaba hiyo na kumdhuru vibaya kwa sababu ya uzito wake.*





Baada ya hapo biblia hii kubwa ilichukuliwa mpaka maktaba kuu ya mji wa Sweden huko *Stockholm ambapo sio kila mtu anaruhusiwa kuiona.*





Codex Gigas kimefanyiwa binding kwa mbao, pia karatasi zake au velum ambapo maandishi yameandikwa zimetokana na ngozi za punda wapatao 160 ambacho kina jumla ya *kurasa 320.* Ila kwa sasa kitabu hiki kina *kurasa 310,* mpaka sasa kuna maswali mengi juu ya *karatasi 10 zilizopungua,* huku ikiwa *haijulikani ni nani au kwanini karatasi hizi hazipo* huku wengine wakisema labda ziliungua siku ile ya moto maktaba na kadhalika.






Maandishi ya kitabu hiki yameandikwa kwa mwandiko wa aina moja yakiwa na rangi za kijana, bluu, nyekundu na dhahabu.






Kitu kingine kinastaajabisha juu ya kitabu hiki ni picha mbili, moja ya *mbingu* na nyingine ya dunia wakati wa *uumbaji ambapo inadaiwa kuna siri kubwa iliyoandikwa juu ya fafanuzi ya hizo picha.*






*Historia yake (From Legends).*

Kutokana na kumbukumbu, codex gigas iliandikwa na *Herman the Recluse* mjini Czech ambaye alikuwa ni *Monk*.





Monk huyu inasemekana alikuwa amevunja (amefanya kosa) baadhi ya sheria zao za kimonk, hivyo alihukumiwa kifo kibaya cha adhabu kali kinachoitwa *“walled up alive” yaani unajengewa kijumba chako kidogo sana ambacho hakina upenyo, kisha unaingia kwa kusimama mpaka utakapokata roho.*

kuepuka adhabu hiyo, monk huyu aliamua kutoa ahadi kwa wakubwa zake na miungu yao kua *atatengeneza kitabu kimoja kikubwa kwa usiku mmoja ambacho kitakuwa na hekima yote ya dunia hii na kuwatukuza mamonks wote milele na milele.*






Alipoanza kufanya hiyo kazi, katikati ya usiku alianza kuona kuwa hawezi kuandika kitabu hicho akamaliza kwa usiku mmoja peke yake hivyo alihitaji msaada. Alifanya maombi maalumu *sio kwa Mungu bali kwa Lucifer ama shetani ili amsaidie hiyo kazi.* Legends zinasema Lucifer alikubali kumaliza hiyo kazi huku akitaka roho ya Herman kama shukrani kwake. Hivi ndivyo kitabu kilivyoandikwa na kuna sababu za msingi nyingi ambazo zinathibitisha kitabu hiki hakikuandikwa na mwandamu, moja wapo ni hii hapa, *Kwa mahesabu ya wanasayansi wanasema kama kitabu hiki kingeandikwa na mwanadamu basi kingechukua Zaidi ya miaka 30 kukiandaa kutokana na umakini ambacho kinacho hiki kitabu, ikiwemo marembo mengi tena yasiyopishana hata kidogo.*
 
Codex
IMG-20180628-WA0013.jpg
 
KUTANA NA MTABIRI WA ZAMA ZA KALE ALIYECHUKULIWA KAMA CHIZI ILA MWISHOWE AKAJAKUKUMBUKWA MANENO YAKE.

Katika wilaya ya Musoma kuna eneo mashuhuri kwa uvuvi na shughuli za kilimo linaitwa Majita,hili ni eneo linalokaliwa na Wajita kwa sehemu kubwa na Wakwaya ambao pia ni jamii ya wajita.

Nilipofika katika hili eneo ambalo kwa sasa limetengwa kuwa halmashauri ambayo makao makuu yako Mrangi,kabla ya kuhama kurudi Arusha niliifatilia historia ya hili eneo na kati ya mambo mengi ya kihistoria nilvutiwa na historia ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mjee.

Mjee alikuwa hajaoa na alikuwa hana makazi maalumu,alikuwa mtu wakutembea tembea leo yuko kijiji hiki na wiki kesho yuko vijiji vingine.Alikuwa hana urafiki wa karibu na watu wazima,maana huwezi mkuta akijadiliana jambo na watu wazima ama wazee bali ni watoto wadogo ndo walikuwa ni marafiki zake.

Akiingia kijijini unakuta anatembea na rundo la watoto wadogo maana watu wazima walimuona kama hazimtoshi yaani punguani,ila walikuja kujua kama hakuwa punguani pale mambo aliyokuwa anawaambia yalipoanza kutokea ikiwa ni baada ya miaka mingi kupita.

Ni mtu wa pekee ukiifatilia historia yake maana alitabiri mambo mengi na hata yeye kujitabiria angali akiwa hai kuwa baada ya kifo chake kila mwanamke katika Majita nzima atakaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima atamuita jina lake yaani Mjee iwe kwa kupenda ama kutopenda.Hili limethibitika ndani ya majita nzima,maana kwa kila mwanamke anaye jifungua mtoto wa kiume ni lazima amuite jina la Mjee ingawa atakuwa na jina lake lingine.Hivyo hata wazee wa miaka 90 kule majita waliitwa jina la Mjee na mama zao na hili halina ubishi,hii inaendelea hadi leo.

Nilipoongea na wazee wakaniambia alitabiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuja kwa wakoloni,watu kuishi pamoja yaani vijiji vya ujamaa,watu kuishi kwenye vichuguu,kiongozi wa kwanza wa hili taifa kutawala akiwa tumboni,atake fuata na utawala wake,wa pili na hata wa mwisho na pia jiwe litakalo tokea.Alipo kuwa anayaongea hayo alikuwa anatoa sauti kama ya mtu anaye lia kwa kupiga mayowe.

KUJA KWA WAKOLONI.

Ikiwa ni kabula ya kuja kwa wakoloni,mjee alipita kwenye vijiji na kupaza sauti ya mayowe huku akifuatwa na msururu wa watoto na kuwaambia watu kuwa anaona mitumbwi mikubwa inakuja akimaanisha(meli na majaazi) imebeba watu ambao ni kama watoto(yaani ni weupe).Wanakuja ili kututesa na kila tulicho nacho watatunyang’anya. Alipo kuwa anayaongea haya watu wazima walisikika wakisema haaaa ni Mjee omusasi (yaani ni Mjee punguani/kichaa) alikuwa akidharaulika sana maana alionekana hazimtoshi.

Baada ya kifo chake na miaka mingi kupita ndipo wakoloni waliivamia Tanzania na hata wengine kufika majita na watu wengi kuuwawa wale walokuonesha upinzani wa kutawaliwa na wale watu.Maeneo yaliyo tumika kwa wenyeji kujificha wakati wa mapambano ni maeneo ya Makojo hadi Chimati,ambapo maeneo ya Chimati kuna mto ambapo mafuvu na mifupa ya watu ilionekan hadi miaka ya 1985.Ndipo hapo walianza kumkumbuka Mjee kuwa yule mtu hakuwa punguwani bali mtabiri.

VIJIJI VYA UJAMAA

Mjee alitabiri pia kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa ambapo alisikika akisema,ameiona mitumbwi inakuja huku imejaza mashoka(yaani jimbasa),akaona watu wanachukua mashoka na kufyeka pori(yaani kandokando) na akaona watu wanaishi ndani ya hayo maeneo. Akasema anaona watu wamejaa na wengi wanauana maana wamekosa mahala pa kuishi alipo kuwa anayasema hayo watu wazima wa maeneo aliyokuwa anapita walikuwa wanamcheka,ila kwa sasa maono yake yamesha timia.

WATU KUISHI KWENYE VICHUGUU

Miaka hiyo kila nyumba iliyokuwa inajengwa lazima ujenzi wake ulikuwa ama ukitumia nyasi,juu hadi chini ama ukitumia miti. Mjee aliona watu wakiishi kwenye vichuguu nadhani alishindwa kujua ujenzi unao tumika kwa sasa kutokana na uhalisia wa mazingira ya wakati huo na tekinolojia ya wakati huu.Vichuguu ni nyumba ya mchwa ambayo hujengwa na mchwa wenyewe kwa tope,ila alivyokua anaangalia huko mbele aliona pia watu wakiishi kwenye vichuguu yaani nyumba iliyo jengwa kwa tope kama za wakati huu.Hili halina ubishi maana maono yake yalitimia na yametimia kwa watu kutumia tope( yaani tofali) kujenga nyum

MTAWALA WA KWANZA KUTAWALA AKIWA TUMBONI

Miaka ya Mjee kuzunguka hili eneo la Majita,pia aliweza kutabiri kuhusu kiongozi wa kwanza wa nchi hii,akiwa katika kutembea na marafiki zake ambao walikuwa ni vijana wadogo,alisikika akisema(kwa sauti ya juu) kuwa ameoneshwa kuwa kiongozi wa kwanza atazaliwa huku majita,pia anaona huyo mtoto akitawala nchi akiwa tumboni maana wabaya wake watamuua,akasema ameona mtoto mwingine amezaliwa mashariki huyo ndo atakuja kuitawala nchi hadi ataacha mwenyewe,na atakuwa na amri juu ya hao watu weupe maana atawaambia ondokeni nyumbani kwangu nao watamtii maana wa mwanzo hatakuwepo tena.Aliyetabiriwa hapa ni mwl J.K.Nyerere maana Zanaki (Butiama) ipo mashariki mwa Majita

Baada ya miaka mingi kupita kati ya kijiji cha Bugunda au Bulinga alitokea mama mmoja mjamzito,ilikuwa ni kama muujiza pale mtoto aliyekuwa tumboni mwa mama yake alipo mwambia mama yake kuwa amzae ili akatawale nchi.Habari hii ilienea majita nzima kwa wakati huo hadi kwa machifu wa wakati huo hii haikuwa habari njema kwa watawala wa wakati huo kwani walidhani huyo mtoto atakuja kuwanyang’anya uchifu wao.Mtoto alipoanza kukua watawala wa wakati huo wakafanya mbinu ya kumuangamiza na hilo lilifanikiwa na kutimiza usemi wa Mjee wa kusema kuwa atatawala akiwa tumboni.Lakini baada ya mwl Nyerere kuja na kuikomboa nchi ndipo walipo kumbuka maneno ya mjee. Hili lilitokea kama maono ya mjee alivyokuwa ameoneshwa.

KIONGOZI ALIYEFUATIA.

Katika kutembea kwake huku akipiga mayowe,Mjee aliendelea na utabiri ambapo aliongea bayana kuwa baada ya utawala wa huyo atakaye tokea mashariki atakuja kiongozi mwingine atakeye tokea (Kwisinga) akimaanisha kisiwani,mda ukayoyoma na Nyerere alipo staafu kiongozi aliyefuata alikuwa ni Mzee Ruksa(Mwinyi).Waalokuwa na kumbukumbu ya kile Mjee alichoongea walikumbuka maana Mzee Mwinyi alitokea Zanzibar.

ATAKEYE MFUATA HUYO

Mjee alioneshwa kuwa baada ya huyo wa kisiwani atafuatia mtawala mwingine atakaye tokea mwisho wa nchi,Mtu akiwa Musoma(Mara) mwisho wa nchi itakuwa ni mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi.Lakini huu utabiri wake ulikuja kuthibitika pale Rais aliyefuata baada ya Mwinyi alitokea mkoa ambao uko mwisho wanchi kwa mtu atakayetokea mkoa wa Mara ama Musoma mwisho wa nchi ni mikoa niloitaja hapo juu ambapo BWMkapa alitokea mkoa wa Mtwara.
 
*KUTANA NA VYOMBO VISIVYOJULIKANA VITEMBEAVYO ANGANI NA KUIACHA DUNIA NA BUMBUWAZI.*



Kwa miaka takriban 100 sasa dunia imeshindwa kutengua kile kinachoonekana kuwa kitendawili kigumu, kuhusu kuwepo Vyombo vya Anga maarufu kwa jina la UFO.

UFO ni 'Unidentified Flying Objects,' yaani Vyombo vya Anga Visivyofahamika.

Mpaka wakati huu, hudaiwa na Wanasayansi wa masuala ya anga kuwa vyombo hivyo haijulikani ni wapi vinatoka kuja duniani.

Hata hivyo, yapo madai kuwa mataifa makubwa, ikiwemo Marekani, Urusi, China, Uingereza na Japan, yanafahamu chanzo cha kuwepo vyombo hivyo.

Upo uwezekano kuwa mataifa hayo yamekubaliana kutunza siri kuhusiana na UFO.

Pia zimekuwepo dalili nyingi kuonesha kuwa upo uwezekano kwa Marekani kufahamu kile kinachoendelea kuhusiana na vyombo hivyo, hususan kutokana na madai ya Wamarekani wengi kuishutumu serikali yao kuficha ukweli juu ya vyombo hivyo.

Wamarekani huishutumu serikali yao kuwa inafahamu au inahusika na kuwepo UFO, na hivyo kusababisha hofu kwao.

Miongoni mwa watu maarufu waliowahi kutaka ufanyike uchunguzi kuhusiana na UFO ni milionea Laurance Rockeffer, ambaye sasa ni marehemu.

Mwaka 1993 hadi 1995, tajiri huyo alitoa kiasi cha fedha zake kuanzisha na kuendesha kampeni ya kutaka serikali ya Rais Bill Clinton nchini Marekani iueleze umma ukweli kuhusiana na UFO.

Ingawa kimsingi serikali hiyo ilikubaliana na matakwa hayo, lakini baadaye ilielezwa kuwa uchunguzi haukubaini chanzo cha UFO.

Kadhalika, wakati wa kampeni ya kuwania Urais wa Marekani ambapo Bi Hillary Clinton alichuana na Rais wa sasa, Donald Trump, mwanamama huyo aliahidi kwendeleza uchunguzi huo dhidi ya UFO.

Hata hivyo, Clinton alibwagwa na Trump na hivyo wazo la kutafiti UFO likafa.

Miongoni mwa taasisi ambazo zimekuwa zikibanwa na umma kueleza au kuthibitisha kama UFO ni vyombo vya anga kutoka anga za mbali, ni pamoja na NASA ambalo ni shirika la anga za juu la nchi hiyo.

Kwa upande wake, shirika hilo lenye wanasayansi wa anga waliotukuka, limekuwa linakanusha kufahamu chochote kuhusiana na uwepo wa UFO.

Nchi zingine zote hazisemi chochote kuhusiana na vyombo hivyo, ingawa watu wao wamekuwa wakiviona na kuhoji serikali zao.

Kadhalika, licha ya wanaanga wa vyombo vya Apollo vilivyosafirisha binadamu 12 kwa nyakati tofauti kwenda kutua mwezini mwaka 1969 hadi 1972 kudai kuwa waliona UFO, lakini NASA hukanusha vikali.

Miongoni mwa wanaanga hao ni wale wa Apollo 11 mwaka 1969, ambao walidai kuwa wakiwa katika siku ya 3 safarini tangu kuondoka duniani (siku 1 kabla ya kuwasili mwezini), ghafla walistukia UFO inajitokeza angani na kwenda sambamba na Apollo ambayo kasi yake ilikuwa kubwa ajabu.

Kwa mujibu wa kitabu cha David Knight: "UFOs" cha mwaka 1979, mwandishi hueleza kuwa Julai 19, 1969 saa 12 jioni katikati ya anga ya dunia na mwezi, UFO ilijitokeza na kumudu kwenda na kasi ya Apollo.

Licha ya wanaanga hao kuiarifu NASA duniani kuwa chombo cha kigeni kilikuwa kimejitokeza angani na kutishia usalama wa Apollo, walijibiwa kuwa "hiyo ni UFO, achana nayo, zingatieni safari yenu, chunga muda."

Aidha, huelezwa kuwa kwa nyakati tofauti UFO zilijitokeza mara 3 dhidi ya hiyo Apollo 11, mara ya mwisho ikiwa wakati imetua mwezini; ambapo UFO ilituwa kwa mbali.

Kwa vile wanaanga wote wa Apollo zote hueleza kutokewa na UFO huko anga za juu, ngoja tugeukie eneo lingine.

Yapo machapisho ya miaka mingi yanayosimulia kuonekana kwa UFO, ambapo mwaka 1930 nchini Marekani vyombo hivyo viliripotiwa kuonekana.

Kuna kumbukumbu inayoeleza kuwa hata katika karne ya 15, UFO zilikuwepo katika anga ya dunia.

Kumbukumbu hiyo inataja Aprili 14, 1561 ambapo chombo chenye umbo la pembetatu kilionekana kuruka katika anga ya Nuremberg, Ujerumani.

Kati ya mwaka 1916 na 1926 matukio 1,305 ya kuonekana UFO yalirekodiwa nchini Marekani, mwaka 1946 matukio 2,000 katika nchini za Scandinavia, yaani Sweden, Norway, Finland, Denmark na pia nchini Uholanzi.

Hali hiyo pia imekuwa ikiripotiwa katika nchi mbali mbali, ambapo nchini Afrika ya Kusini ambayo pia huandamwa na UFO iliripoti kuonekana chombo hicho Oktoba 30, 2011.

Nao marubani wa ndege za abiria wamekuwa wakiripoti kuona UFO wakiwa safarini angani.

Katika ripoti za watafiti wa UFO duniani kote, zaonyesha kuwa mpaka wakati huu jumla ya matukio 3,500 ya kuonekana vyombo hivyo yameripotiwa na marubani wa ndege za abiria.

Aidha, mwaka 1952 ndipo jina la UFO lilipoanza kutumika nchini Marekani, badala ya jina la awali la "flying saucers" (visahani virukavyo).

Lakini pia wakati utata ukiendelea hivyo, inadaiwa na mashuhuda kuwa katika Jimbo la Nevada nchini Marekani kuna eneo la siri liitwalo No. 51 ambalo ni hifadhi ya viumbe kutoka anga za mbali na baadhi ya UFO zao.

Hudaiwa kuwa eneo hilo lenye ulinzi mkali kutoka vyombo vya ulinzi vya Marekani, lina barabara ya urefu wa kilomita 158 iitwayo "Extraterrestrial Highway" (barabara kuu ya anga za mbali), ambayo wasafiri wa kitalii huripoti kuona viumbe wenye maumbo ya kibinadamu wakiranda jirani.

Barabara hiyo ilipewa jina hilo mwaka 1996, na inadaiwa kuwa tangu mwaka 1976 shughuli katika eneo hilo zimeongezeka maradufu.

Inadhaniwa kuwa yawezekana viumbe hao ni wale ambao huripotiwa kukamatwa mateka baada ya kuanguka UFO, au pengine huenda Marekani ina "ubia" wa kiteknolojia na viumbe wa UFO kutoka anga za mbali.

Hiyo inatokana na kuwepo usiri mkubwa katika eneo hilo No. 51, ambalo hata hivyo kuwepo kwake hukanushwa na serikali ya Marekani.
 
HIVI NDIVYO NA FBI MPELELEZI ALIVYOFANYAKAZI NA MAGAIDI ILI KUWAPELELEZA.

Tamer El-Noury ni jina lake kamili akiwa ni FBI muislamu ambaye alipewa jukumu la kuingia ndani ya makundi ya kigaidi yenye msimamo mkali na kushirikiana nao katika kupanga mashambulizi dhidi ya Marekani. Huyu alihusika kwa kiasi kikubwa kabisa katika kupanga mashambulizi huko new York ambako walitakiwa kuiondoa train kwenye reli ili isababishe uharibifu na vifo vingi miaka minne iliyopita.

Aliamua kuandika kitabu akitaka waamerika wafahamu kazi yake akiitumikia nchi yake kama Muislamu ndani ya FBI. Anaelezea magaidi ni watu wa namna gani katika mahojiano yake na BBC.

“Kiukweli magaidi ni watu ambao katika maisha wanakuwa wameshakata tamaa. Ni watuwasio jielewa wasioelewa wataishi vipi. Hawa huchukuliwa na kufundishwa chuki, hupandikizwa chuki ambao inahusishwa na dini , Imani. Hapa kwa kupandikiziwa haya huwafanya wajione sasa wamepata tumaini,wamepata uelekeo”

Anaendelea kusema “mimi ni Muislamu na pia ni Mwamerika na nina fadhaishwa na haya yanayofanywa na hawa wanyama kwa nchi yangu na kuidhalilisha pia dini yangu”

FBI waliona wana upungufu kiasi flan cha watu wanaoweza kuzungumza kiarabu. Kwa namna utendaji kazi wa FBI ulivyo una departments nyingi na kila aina ya watu. Kuna walimu,kuna madaktari,kuna wanasheria,kuna wanajeshi,kuna polisi,kuna kila kada ambayo inahitajika hapa duniani ambayo wanajua wanaweza hitaji mtu wa namna hiyo katika operations zao mbalimbali hapa duniani. Hivyo hata wale ambao kuna wakati inabidi wajifanye vichaa, ombaomba, wapiga debe n.k kila sehemu kila aina ya mtu. Huko kote watu huwa wamejifunza lugha husika kwa kiwango cha juu sana. Hulelewa katika kujifunza kazi za FBI wengine toka wakiwa wadogo. Hivyo kila mara hujiangalia wanahitaji kuboresha kada gani katika vitengo vyao mbalimbali. Kumbuka walipoenda kumpeleleza Osama kuna walioenda kipindi cha upelelezi huko Pakistani kama madaktari wa chanjo wakizungumza kiarabu kizuri kabisa.

Bwana EL- Noury ni motto wa Mhamiaji wa Kiarabu kutoka Misri. Ambaye alijiunga na jeshi la polisi huko New Jersey. Ambako alikuwa akifanya kazi kubwa ya kuyavunja makundi yanayojihusisha na madawa ya kulevya. Kipindi chote hicho FBI walikuwa wakimsoma,wakimfuatilia kwa ukaribu na mwishowe waliamua ku mchukua baada ya kugundua wamepungukiwa na wafanyakazi wanaozungumza kiarabu.

Katika shughuli zake hizo akiwa kama undercover alikuwa amepewa jukumu la kuua watu wengi kadri awezavyo katika jaribio flan la kigaidi ambalo lilihusisha kuiangusha train ya umeme kutoka New York kwenda Toronto. Na hii ni kwa vile magaidi wenyewe walikuwa wakiamini kuwa huyu jamaa ni mtu wao mmoja ya watu wenye chuki na USA. Alijiunga kupitia urafiki wake wa karibu na Raia wa Tunisia Chiheb Esseghaier ambaye alikuwa mmoja ya wahusika wakuu katika jaribio hilo la Kigaidi. unaweza soma zaidi habari zake na namna ambavyo alikamatwa kutokana na intelejensia iliyofanyika ikisaidiwa na El-Noury kwa kiwango kikubwa.

Kutokana na urafiki ambao alikuwa amejitengenezea na Esseghaier basi naye akawekwa kuwa mmoja ya wahusika wa jaribio hilo la hatari. Yeye alikuwa akionekana kama ni Ni Mmarekani mwenye asili ya kiarabu tajiri. Ambaye alikuwa na chuki kubwa sana kwa Wamarekani. Na hii ndiyo ilikuwa gear yake ya kuingilia katika hilo kundi la kigaidi. Anasema alikuwa na wakati mgumu . maana alitakiwa hasa ajengeke kuwa ni mtu wa namna hiyo kwa kipindi chote yupo na lile kundi. Alijitahidi sana kuendana na ukweli wa kile ambacho alikuwa amewaambia.

Hivyo hadith zake zote, kila ambacho alisema kilipaswa kiwe kina uhalisia kulingana na aliyokuwa kiwaambia. Anasema “unaposafiri dunia nzima na kundi la magaidi wenye msimamo mkali ukimaliza siku,wiki na miezi pamoja nao inabidi uwe kama wao. Ama sivyo uhalisia wako utaonekana maana upo chini ya ngozi yao.hivyo inabidi u copy na maisha yao na kile unachokisema”

Unapaswa kuwafanya wakuamini, waone wewe ni mwenzao maana kinyume na hapo ni kuhatarisha maisha yako .lilikuwa ni suala la kufumba na kufumbua wao wakijua kuwa si mwenzao unauawa kwa mateso makali sana. Hivyo ni kama umeiweka roho yako rehani.

"Kazi yangu ilikuwa ni kuwa karibu sana na wale watu wabaya.wale watu makatili wenye kupanga na kutenda mambo ya kinyama. Nilipaswa kuwasikiliza na pia kuwafuatilia kwa ukaribu sana jinsi wanavyozungumzia familia zao, mama zao, ndugu zao n.k"

Wakiwa katika safari ya kwenda New York Esseghaier alianza kupanga nao mipango ya shambulio lijalo eneo la Times Square huko New York wakati wa sherehe za Krismas na mwaka mpya. Wakiwa katika safari hiyo hiyo wakatembelea Twin Tower ilipotokea shambulio la 9/11. Anasema wakiwa katika eneo hilo Esseghaier alisema” Marekani inahitaji September 11 nyingine tena” kauli hii ilimshtua sana El- Noury na anasema ilikuwa kidogo ajiumbue kutokana na ule mshtuko na mchango wake katika matamshi hayo.

Anasema bahati nzuri mipangao hiyo haikufanikiwa sababu Esseghaier na Raed Jaser na mpalestina mmoja aliyekuwa akiishi Canada walikamatwa mwaka 2013 na kuhukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2015 kupitia upelelezi uliofanywa na El-Noury.

Mahojiano yaliyofanyika kuhusiana na story hii ya El-Noury yalitoa mwangaza mkubwa sana kuhusiana na nini kina fanyika katika ulimwengu wa giza wa kikaidi akiwa kama undercover.FBI walisisitiza kuwa mahojiano hayo yafanyike kwa njia ya simu huku wakifuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kumlinda mtu wao.

Kwa mengi ambayo aliyaelezea ni bora ukisoma kitabu cha Ameican Radical Inside the world of an Undecover Muslim FBI Agent.
 
UTATA WA HALI YA JUU KUHUSU KIFO CHA ADOLF HITLER.

Kwenye misitu mizito ya Eurasia na kusini mwa marekani hasa Argentina ndipo asili ya mbwa mwitu wa kijivu (The grey wolf). Ni jamii ya wanyama wenye meno makali sana (canine) na ni adui mkubwa sana wa binadamu, alipo mnyama huyu mwanadamu hasogei kabisa. Lakini katika misitu hii mwanaume mmoja mjerumani alitia miguu yake akapaza sauti na kusema "sioni sababu yoyote kwanini mwanaume kama mimi nisiwe katili kama mbwa mwitu wa kijivu"

Uwezo wake wa kuzungumza kimkakati na ushawishi wa hoja ulikua ngome yake kuu ya kujizolea umaarufu na kumpandisha cheo katika chama kipya kilichoibuka kwa nguvu sana katika jiji la Berlin. Akiwa kijana mbichi kabisa, mwaka 1932 alikiongoza chama chake chaa Unazi (Nazi party) kushika madaraka naye kuwa kansela wa Ujerumani na Führer (kiongozi mwenye madaraka ya juu zaidi).

Kipindi cha utawala wake wa kibabe na mabavu, Hitler alitengeneza maadui wengi sana, hakuwahi kuwa mtu wa amani sana kwa yeyote aliyempinga. Pamoja na kusaini mikataba ya kirafiki na mataifa ya Urusi (Soviet), Hitler alipinga vikali ukomunisti (communism). Lengo lake kubwa lilikuwa kuteka, kuongeza ushawishi na kutawala mashariki mwa Lebensraum (ukanda wa nchi za mashariki mwa Ulaya). Sept 1, 1939 Hitler alipenya na kuvamia taifa la Poland. Miezi minne baadae Urusi muungano (Soviet union) ikiongozwa na Joseph Stalin walivamia na kumiliki nchi za Baltic (Estonia, Lithuania na Latvia).

Hitler hakufurahia kitendo cha mrusi kumzidi kete katika kumiliki mataifa haya ya Lebensraum. Aliamini angelisambaratisha vibaya Jeshi la damu (The red army), ndipo June 1 1941 ndipo Hitler aliamuru uvamizi wa nchi ya Urusi. Uingereza na Ufaransa wakatoa tamko la kupambana kumuangusha Hitler.

Aliingia kwenye handaki lake takatifu (FuhrerBunker) akapaza sauti kwa maofisa wote wa kijeshi na kusema "surrender is forbidden"_ "kujisalimisha ni mwiko". Mapambano ya WW2 yalianza, Majira ya michipuko (spring) ya 1942 Hitler alisuka mkakati wa kuteketeza wapinzani wake na aliamini ushindi utarudi kwake. Falsafa yake kuu ilikua "mwanaume hodari hapimwi kwa uwezo wake wa kujihami, bali makali yake katika kushambulia na kuteketeza". Hali ilikuwa tofauti sana baada ya mapigano kufikia Stalingrad (ngome kuu ya kivita ya Urusi), Marekani iliingia kwenye vita na ngome ya Urusi ikaimarika zaidi, Hitler alishindwa kushambulia na jeshi lake likaanza kujihami.

Kwa mara ya kwanza chozi lilimtoka Hitler baada ya kuona dalili za kupoteza ushindi. Wanamgambo wake na maafisa wa juu walimkosoa vikali hukusu kusalimu amri, upinzani dhidi ya Hitler ndani ya jeshi la Ujerumani ulizidi, hali ilikua tete Kipindi ambacho makamanda watiifu walianza kuweka silaha mezani na baadhi ya maafisa waandamizi wa jeshi la Ujerumani walitamani Hitler afariki/auwawe.

Mnamo tarehe 20 Nov 1942 Hitler akiwa katika kikao na viongozi wa juu wa kivita katika makao makuu yao ya Wofl's liar, afisa daraja la kwanza, Luten Kanali Stauffenberg aliandaa shambulizi la kumuangamiza Hitler. Alitega bomu ndani ya mkoba na kuuacha mkoba juu ya meza, saa 6:42 mchana bomu lililipuka. Maafisa wa4 wa Ujerumani walifariki, lakini Hilter aliponea chupuchupu na kutoka akiwa na majeraha madogo.

Alisikika akisema kwa dharau "nani tena haamini kuwa kuna nguvu maalumu ya Mungu inayonilinda". Baada ya shambulio hilo jeshi la Hitler liliendelea kudhoofika kwa kasi na Hitler kujiridhisha kua kamwe hakuna muujiza utakaomfanya ashinde vita.

Jeshi la Urusi lilipenya zaidi kufikia ngome ya Ujerumani. Katika siku za mwisho kabisa za vita Hitler aliamua kumuoa mpenzi wake wa muda mrefu Eve Braun. Siku chache baadae Hitler akiwa kwenye handaki maalumu aliagiza apunguziwe ulinzi, aliomba aletewe vidonge vya cyanide. Alivijaribu vidonge hivyo kupitia mbwa wake wa2, ambao wote walikufa.

Saa 3 asubuhi tarehe 2 May 1945, inasemekana Hitler alichukua vidonge 6 vya cyanide akavichanganya kwenye glass yake ya wine, yeye pamoja na mkewe wakanywa, kisha Hitler akafungua bastola yake ndogo, akapenyeza risasi kichwani kwake. Damu iliyomwagika kwenye sofa ilitunzwa kama ukumbusho. Mwili wa Hitler na mkewe ulichukuliwa hadi nje ya handaki na kuchomwa moto.

Keshowe, tarehe 3 May 1945, kiongozi wa ngazi ya kuu kabisa wa jeshi la wanamaji (navy) Generali Karl Domtz alivuta simu ya mezani na kupigia kituo cha redio cha Ujerumani na kutangaza rasmi kifo cha Hutler na mkewe Eva.

UKWELI KUHUSU KIFO CHA HITLER

Kiongozi mkuu wa Urusi Josef Stalin aliomba ushahidi juu ya kifo cha Hitler, alisikika akisema "Isingekuwa rahisi kumuuwa Hitler wala Hitler kujiuwa_huyu yu'hai".

Taarifa za ushahidi wa Hitler na mkewe Eve kuwa hai zilianza kupenya. Habari za kushtusha zilisambaa kwamba dakika za mwisho wa mapigano Hitler na mkewe walitoroshwa kwenda kwenye pori zito huko Argentina. Mnamo tarehe 29 April 1945 kupitia tundu refu la siri lililokuwemo ndani ya handaki tukufu lilitumika kumpenyeza Hitler hadi baharini, ambapo U-boat [HASHTAG]#502[/HASHTAG] (underground boat nambari 501) lilikua likiwasubiri kuwasafirisha chini ya bahari hadi Argentina ambako walipokelewa na wageni wa Juan Peron (Raisi wa Argentina) pamoja na mkewe Evita. Ikumbukwe serikali ya Hitler ilidhamini uchaguzi uliomuweka madarakani Juan kuwa kiongozi wa mabavu wa Argentina.

Hitler, mkewe na binti yao waliishi maisha ya kifahari sana kwenye miji mbalimbali nchini Argentina hadi mwaka 1955, ambapo Eva na bintiye Ursula walimwacha Hitler na kuelekea Neuquen. Hitler alifariki kifo cha kawaida sana mfamo mwaka 1962.

USHAHIDI JUU YA KIFO CHA HITLER

●Mwaka 2010 kikosi cha Marekani cha kiinteligensia cha CIA kilitoa taarifa za siri ya juu (declassified information), andiko lenye kurasa 792 zikieleza uhalisia juu ya nadharia ya kifo cha Hitler na kubainisha kua kikosi maalumu cha Marekani kilisaini kumtorosha kwa siri Fuhrer Hitler mafichoni.

●Hakuna uthibitisho wowote wa mwili wa Hitler sehemu yoyote duniani baada ya WW2. Marshall Zhukov, kiongozi wa jeshi la Urusi alizungumza na waandishi wa habari na alinukuliwa akisema "We never identified the body of Hitler, I can say nothing about about his fate. He could have flown away from Germany at the last moment"__ "Hatukufanikiwa kuutambua mwili wa Hitler, siwezi kuzungumza chochote kuhusu mauti yake. Yawezekana alitoroka dakika za mwisho kabisa".

●Simulizi ilibadilika mwaka 1968, Warusi walipoamua kufukua kilichoaminika kuwa ni mabaki ya mwili wa Hitler yaliyochomwa moto. Walifanikiwa kupata fuvu lenye tundu la risasi, taya na meno ya Hitler. kwa muda mrefu serikali ya Urusi haikutaka kupeleleza mabaki hayo, hadi ilipofika 2009 ambapo serikali iliridhia uchunguzi ufanyike. Jopo la wataalamu wa mifupa, vinasaba na akiolojia likiongozwa na Bellanton walifanya uchunguzi wa mabaki hayo. Matokeo yaliuduwaza na kuustaajabisha ulimwengu. Hapakuwa na sampuli yoyote iliyoendana na DNA ya Hitler, fuvu lile liligundulika kua lilikua la mwanamke mrembo sana mwenye umri wa miaka 39-40. (Wala hakuwa Eva, mke wa Hitler).

Fuvu lilitokea wapi? Lilikuwa na nani? Kwanini Warusi walilihusisha na Hitler? Vyovyote vile, vipomo na majibu ya uchunguzi viliuwa porojo zote kuhusu kujiuwa kwa Hitler.

●Njia ya Panya ya Wanazi.
Viongozi wengi wa juu Nazi walioshiriki katika utawala wa damu wa Ujerumani walitoroka mafichoni baada ya WW2, kwa msaada wa mitandao ya siri ikiwemo Odessa (wa Ukraine), kanisa katoliki pamoja na Taasisi ya siri ya Marekani. Wamwaga damy mashuhuri kama Josef Mongele na Adolf Eichman walikimbilia katika nchi za kidikteka kama Chile na Argentina.

●Mnamo mwaka 2014 Simon Dunstan na Gerrard Williams waliandika kitabu kiitwacho Grey wolf: The escape of Adolf Hitler (Mbwa mwitu wa kijivu: Kutoroka kwa Adolf Hitler). Kitabu hiki kilibainisha kwa undani kuhusu kutoroka kwa Adolf Hitler na nadharia ya uwongo juu ya kifo cha Hitler. Kitabu hiki kilijumuisha wakazi wa Argentina waliotoa ushahidi wa kumuona Hitler akikatiza mitaa ya Argentina.

Maneno ya mwisho yaliyosikika kutoka kwa Hitler akiwa ndani ya Handaki, alisema " Naamini leo kwamba mwenendo wangu ni kwa mujibu wa mapenzi ya Muumba Mwenyezi Mungu"
 
KWA NINI WATU MASKINI WENGI WANAMPENDA CHE GUEVARA?.

Alizaliwa mnamo 14 Mei 1928 Rosario nchini Argentina. Alikuwa mtabibu aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.

Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumng'oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba katika umoja wa Mataifa UN, aliweza kupata sifa ya mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

"Wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?"

Mwaka 1965 ikiwa ni Miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida public life na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha.

Baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari, aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry forest.

Mnamo mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake.

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema

"Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa".

Alifungwa kamba na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu René Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili asiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale.

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho,

"Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili"

Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda kuivaa vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.

Aliacha wake wawili na watoto watano
 
NGOJA NA MIMI NIONGEZEE KANGU

Ukifika mpwapwa mjini ni story maarufu sana ,kuna mlima uko jirani mji kuna uvumi kuwa kuna nyoka anajiwe la kati ya kilo 2-5 lipo kichwani mwake na linag'ara sana ,jiwe hili huonekana mara kwa mara (haizidi wiki) nyakati za usiku na huwa lina hama hama.kuna waarabu walifika hapo baada ya kuambiwa tetesi wakaenda mlimani usiku wakarudi na taarifa ni kweli ,aidha kabla sijaendelea joka hili huonwa na watu wengi na halina madhara kabisa kwa binaadamu ,basi jamaa wakaondoka wakarudi na mfao wa jiwe lenye taa ndani wakamvizia nyoka yule alipoliacha kwenda kujipatia ridhiki kama ilivyo ada wakamuachia lile litaaa wakiwa wameshalipata jiwe lile wamelifungia kwenye mfuko joka lile kila likichungulia linaona mwanga mwekundu haliji ghafla wakiwa wanakimbia nalo jiwe lile joka likagundua unaambiwa jamaa wanasema kulikuwa na bonge la mvua halafu kiangazi jumlisha na tetemeko la ardhi wanadai walilitupa jiwe na kikubwa hata gari walilolipaki karibu na mlima walitelekeza na hawakurudi tena ,alitumwa mwarabu mwenzao kulifata baada ya nwezi,asubuhi wazee walipiga tambiko na kukagua mlima walikuta miti imekatwa kwa mstali kama msumeno ,taa hiyo hadi leo ipo ila ujanja na ujasiri hakuna.
 
The only Wakati Nakua Miaka Ya Hivi Karibuni Lilikuwepo Joka Katika Mlima Wa Mlali-Iyegu(ambayo Ni Safu Moja Na Milima Ya Mpwapwa),Kiukweli Joka Hilo Sikuwahi Kuliona Ila Mwanga Wake Niliuona Kila Ilipofikia Majira Ya Usiku Likizunguka-zunguka Mlimani!

Hadithi Za Wakubwa Zilisema Kuwa Ni Joka Mkubwa Mwenye Almasi Na Baadhi Yao Walisema Walimuona Nyoka Huyo Walipopanda Mlima Kwa Nyakati Za Mchana, Ila Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Joka Hilo Na ' Almasi ' Yake Ni Adimu Kuonekana!

Nakala Kwa devor
 
The only Wakati Nakua Miaka Ya Hivi Karibuni Lilikuwepo Joka Katika Mlima Wa Mlali-Iyegu(ambayo Ni Safu Moja Na Milima Ya Mpwapwa),Kiukweli Joka Hilo Sikuwahi Kuliona Ila Mwanga Wake Niliuona Kila Ilipofikia Majira Ya Usiku Likizunguka-zunguka Mlimani!

Hadithi Za Wakubwa Zilisema Kuwa Ni Joka Mkubwa Mwenye Almasi Na Baadhi Yao Walisema Walimuona Nyoka Huyo Walipopanda Mlima Kwa Nyakati Za Mchana, Ila Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Joka Hilo Na ' Almasi ' Yake Ni Adimu Kuonekana!

Nakala Kwa devor
mkuu ukifia mpwapwa tafuta mzee wa jadi mtoe hata efu 50 mwambie akuoneshe within 3 days wanadawa mnapatrol mnaliona ila usilogwe kupiga picha wala kurusha jiwe kuna maji huwa linaacha likitembea wazee huyatumia kuwafanya wanawake wapende na wanaume watulie
 
KUTANA NA JEAN BEDEL BOKASSA, RAIS ALIYEPENDA STAREHE KULIKO WOTE AFRIKA KATIKA UTAWALA WAKE.

Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa.

Jean Bedel Bokassa akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi bilioni 32 za Kitanzania za wakati huu. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!.

Jean Bedel Bokassa alikuwa dikteta wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Alikuwa na wake kumi na saba (17) na watoto hamsini (50).

Alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akiwa na miaka sita (6) baada ya baba yake kufa mama yake naye alijiua.

Alipata kupigana vita ya pili ya dunia chini ya Wafaransa. Baadaye alikuja kumpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965. Alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. Akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

Alikuwa ana majumba zaidi ya sita Ufaransa. Pia alikuwa na majumba mengine nchi mwake, katika majumba yake mengine yaliyokuwa nchini mwake, Jumba lake mojawapo lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa, alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake.

Wake zake walikuwa Mchina, Mjerumani, Msweden, Mtunisia na Mromania. Aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea kila siku na kusababisha foleni kubwa barabarani kutoka na wingi wa safari hizo huku akiambatana na misafara.

Alipinduliwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. Alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.

Walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

Mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na huku akiwa anajiita mtume wa yesu. Hatimae alifariki mnamo mwaka 1996 kutokana na ugonjwa wa moyo.

View attachment 802286

kulubule Asante sana umenipa hamasa zaidi ya kusoma kuhusu huyu Bukasa na nilichokutana nacho kipo hapo chini kwa lugha yetu pendwa. Big up brother


Jean-Bedel Bokassa, Self-Crowned Emperor Of the Central African Republic, Dies at 75


By HOWARD W. FRENCHNOV. 5, 1996
  • As commander of the army and Defense Minister, Mr. Bokassa, then a colonel, was plucked by France to overthrow the Central African Republic's first President, his cousin David Dacko, when Mr. Dacko began establishing close ties with China. Mr. Bokassa's legendary devotion to France and fierce anti-Communism made him the perfect candidate in Paris's view to replace Mr. Dacko.

    Within days of taking power, Mr. Bokassa broke off relations with Beijing, expelling a large delegation of Chinese advisers. At the same time, showing the lust for titles and power that would lead him 12 years later to proclaim himself Emperor, Mr. Bokassa took on the titles of President, Prime Minister, Commander in Chief of the army and leader of the sole political party.

    Even as his behavior grew increasingly erratic, Mr. Bokassa maintained warm relations with France for several years. Valery Giscard d'Estaing, then the French President, was a frequent visitor to the Central African Republic, where he and Mr. Bokassa enjoyed big-game hunting together.

    Paris congratulated Mr. Bokassa when he decided that his republic should be known as an empire, and the French Government helped finance some of the estimated $30 million cost of Mr. Bokassa's lavish coronation in 1977, which was consciously patterned after Napoleon's coronation.

    But eventually, a combination of increasingly frequent bids for independence in foreign affairs by Mr. Bokassa and a growing opposition to the Emperor's extravagance at home led France to conclude that he must go.

    In September 1979, in one of the first actions of its type in Africa in which foreign troops were used to overthrow a leader in power, 700 French paratroopers took control of Bangui while Mr. Bokassa was in Libya.

    Citing the growing repressiveness of his rule, and the reports of cannibalism, France installed Mr. Dacko, whom it had prompted Mr. Bokassa to overthrow 14 years earlier, as President.

    The charges of cannibalism got their start in an article published in Paris-Match magazine that included photographs purporting to show a refrigerator in which the Central African leader kept the bodies of schoolchildren who had been arrested and beaten to death. They had protested having to wear uniforms made from a cloth sold by a business run by the Emperor's wife.

    The Government's violent crackdown on student demonstrations shocked public opinion at home and in France, and ultimately led to Mr. Bokassa's overthrow by French troops. But when he was tried years later on treason and murder counts, Mr. Bokassa was acquitted of all charges related to the killing.

    Mr. Bokassa remained serene throughout a long interview at his home this year, except when asked about the cannibalism story, which he angrily insisted had been planted in the French press by a photographer who was close to President Giscard d'Estaing.


    ''That was not my refrigerator,'' he said of the appliance that appeared in the Paris-Match photos. ''What they showed was the freezer from the morgue, which you can see for yourself. It is still there.''

    Though Paris had successfully removed a leader who had proven himself a nuisance with minimal opposition from other African countries, Mr. Giscard d'Estaing's closeness with Mr. Bokassa would come back to haunt him.

    From exile in the Ivory Coast, where he settled after France refused to allow him entry, an embittered Mr. Bokassa began writing about his long and deep ties with the French. The autobiographical writings, published under the title ''My Truth,'' included details of gifts of diamonds that Mr. Bokassa is said to have frequently made to Mr. Giscard d'Estaing.

    Although the book was banned in France, the disclosures are widely believed to have helped doom Mr. Giscard d'Estaing's 1981 re-election bid against his Socialist rival, Francois Mitterrand.

    After returning home to face the charges against him, and serving time in prison, Mr. Bokassa continued to harbor bitter feelings against France, which he said he had served for more than 20 years but which still refused to open its doors to him.

    Mr. Bokassa was applauded by many Central Africans for condemning France when it intervened yet again in the Central African Republic this May to put down an army mutiny .

    ''Every time we have a problem, the French have to come and meddle,'' he said at the time. ''Finally, you have to ask yourself, are we independent, or are we not?''

    Jean-Bedel Bokassa was born on Feb. 22, 1921, at Boubangui, Central African Republic. One of 12 children, he was born to a family of local chiefs that was prominent in Lobaye Province.

    When he was 6, his father, Mindogon Mgboundoulou, was slain at the local prefect's office in a dispute that the future leader later insisted centered on an argument with French administrators in favor of greater rights for native Central Africans. His mother, Marie Yokowo, committed suicide soon afterward.

    Mr. Bokassa was educated in Roman Catholic missionary schools in Bangui and Brazzaville and initially planned to study for the priesthood. But when World War II began in 1939, he joined the French Army as a private.

    In 1940, the young soldier took part in the campaign at Brazzaville that led to the capture of the Vichy governor for the region and the establishment of the Free French Government there.

    Ten years later, Mr. Bokassa, by then a company sergeant, fought with valor in Indochina, where he survived the French defeat at Dien Bien Phu. His dozen decorations, which he proudly showed to visitors almost until his death, included the Croix de Guerre and membership in the Legion of Honor. At his death, Mr. Bokassa's only income was his French captain's pension, paid quarterly at the French Embassy in Bangui.

    Toward the end of his life, Mr. Bokassa returned to the intense religion of his youth, praying several times a day with a well-thumbed Bible. The former Emperor, long known for his high living, told a recent visitor that he had renounced alcohol and sexual relations for several years.

    Mr. Bokassa, who married several times, is survived by as many as 60 children.

    The Government announced today that Mr. Bokassa, who had enjoyed something of a return to popularity as a nationalist icon in recent years, would be given a state funeral.
 
mkuu ukifia mpwapwa tafuta mzee wa jadi mtoe hata efu 50 mwambie akuoneshe within 3 days wanadawa mnapatrol mnaliona ila usilogwe kupiga picha wala kurusha jiwe kuna maji huwa linaacha likitembea wazee huyatumia kuwafanya wanawake wapende na wanaume watulie
Duh... Dunia Ina Mengi Sana Tusiyoyajua!
 
Back
Top Bottom