asanteee, utawezaa au nawe utachoka njiani kama hubby wangu?
Sijamaliza kusoma story nzima lakini hapo red pamenichekesha sanam, loh! ........ ila ngoja nimalizie utamu wote plus comments za wadau
Nimejifunza mengi baada ya kupitia uzi huu; Asante mleta mada. Sina uzoefu sana ktk hili coz mimi ni mvivu wa kusikiliza lkn pia si muongeaji saaana!
Nahisi, mko katika stage ya kuanza kuchokana at least mwenzio. Jaribu kupeana space, ikiwezekana kutoshare usafiri mnapoenda kazini; ili atleast mkumbukane walau kidogo. Usibadilike, alikupendea jinsi ulivyo na ndio maana ukistopisha story ananuna; ila punguza muda wa kuwa pamoja ili usijiboe na kumboa mwenzio!
Cha mwisho, ulivyouliza humu; muulize the same question mumeo lkn make sure anapata picha ambayo sisi tumeipata in a constructing way.
All the best!
Si wanaume wote. Pamoja na jitihada zetu za kujaribu kupata mpenzi ambaye mtakuwa na compatibility ya kiwango cha kuridhisha, lakini bado kuna compromise nyingi tu inabidi tuzifanye ili kutengeneza, kuboresha na kudumisha mahusiano/mapenzi. Kila upande ni muhimu kufanya compromise na jambo hili linawezekana kama nyinyi wawili mmesomana na kuelewana tabia zenu vizuri.....SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??
Ever remaining,
Sakapal
heheheheeee sasa mbona huniambii au unanionea aibuuuu....? heheheheeee1 lol
nyumba kubwa well said..
Kweli bwana kuna watu kuongea wamejaaliwa yaani wanajua namna ya kupangilia maneno mpaka basi..
Ninaye shemeji yangu kwa kweli ukifika kwake unabaki kucheka tu..she is truly a charming lady..
Bahati mbaya mume wake hapendi vile anavoongea..so, unakuta akianza stori zake broo anaanza kumtuma ili mradi amkate flow ya maongezi..Kingine nilichogundua kupitia huu uzi..wanaume wengi hawapendi kustorishwa na wake zao..
Na wanapenda ile ya one way traffic conversation..yaan mke awage wa kuulizwa na kuitikia tu..lol!!
ha ha haaaa... yaan uko kama mke wangu...lakini mimi huwa namsikiliza...kiukweli sio kwamba hapendi kukusikiliza lakini inategemeana na kazi anayofanya mumeo coz kama ni kazi inayomtaka aconcetrate then by the time akirud home anakuwa amechoka sana...hakika anakupenda tatizo ni hilo tu uchovu. Hata mie kama kuna siku nimechoka sana namuambia plz naomba tulale...!!!
pole sana Sakapal, bt trust me anakupenda wala hajakuchoka tatizo ni stress tu za mjini.
Nadhani umefanya research yako wrongly..
Itakuwa kitu cha ajabu sana kama unadate mtu ambaye hamna 'compatibility'..
Miongoni mwa vitu vinavyowafanya watu wawe pamoja ni hili la kustorishana..
Sikatai inawezekana kuna 'extreme cases' ambapo me au ke ni mwongeaji kuliko mwenziwe kiasi cha kupigiwa mfano..
But my brain tells me kwamba pale ambapo kuna mwanamke muongeaji kuna mwanaume muongeaji pia..
Sema kwa muktadha wa mleta mada inaonekana 'wameanza kuchokana'..yaan mume hana furaha tena na stori za mkewe
Si kweli kwamba ni kawaida ya wanaume waongeaji kutopenda wanawake waongeaji.
Kuna wanaume waongeaji waliojaa vacuous talk, wamejaa majisifu kumpita Kiranga na kila mara wanataka waonekane wao wako juu (kumpita Kiranga, can you believe that?)
Kuna wanaume wengine wengi wa maneno na wanapenda wanawake wenye wingi wa maneno.
Mie mamaa wangu tukikaa hatuishi kuongea istilahi za Kiswahili, siasa, quantum physics, tamaduni za Watanzania kulinganisha na watu wa nje, etc.
Na heshi kuniburudisha kwa kila asemalo, maana ni kichwa. Na mie siishi kumpa vi quiz vya kiajabu ajabu, mara nimuulize maana ya maneno magumu ya kiswahili kuona kama anakikumbuka bado, mara kuongelea habari za Vladimir Putin na mkono wake wa chuma, mara muungano, mara familia zetu.
Basi ilimuradi karibu kila nitakalosema ni muziki masikioni pake, na yeye kila mara heshi kunishangaza kwa kunipa namna mpya ya kuangalia mambo, iliyojaa manzili, ucheshi wa shajara, haiba ya madaha, utanashati na mlahaka, nazaa zote za kike na nakawa iliyo hidaya maridhawa ya kuupa moyo wangu fanaka kuliko johari na libasi, iso dhihaka, uzembe wa kufikiri wala inda na kisirani.
Kwa hiyo twapeana utumbuizo murua sote, bila kashfa.
Na kukanusha maoni yako.