Story za mkeo/mpenz wa ndoa

Story za mkeo/mpenz wa ndoa

Sijamaliza kusoma story nzima lakini hapo red pamenichekesha sanam, loh! ........ ila ngoja nimalizie utamu wote plus comments za wadau

we cheka tu na usiombe yakukute looh inachosha na kukera kwa kweli, usije ukamfanyia hivo mkeo kwakweli
 
Nimejifunza mengi baada ya kupitia uzi huu; Asante mleta mada. Sina uzoefu sana ktk hili coz mimi ni mvivu wa kusikiliza lkn pia si muongeaji saaana!

Nahisi, mko katika stage ya kuanza kuchokana at least mwenzio. Jaribu kupeana space, ikiwezekana kutoshare usafiri mnapoenda kazini; ili atleast mkumbukane walau kidogo. Usibadilike, alikupendea jinsi ulivyo na ndio maana ukistopisha story ananuna; ila punguza muda wa kuwa pamoja ili usijiboe na kumboa mwenzio!

Cha mwisho, ulivyouliza humu; muulize the same question mumeo lkn make sure anapata picha ambayo sisi tumeipata in a constructing way.

All the best!

thanx Kaunga, hata mi nimejifunza mengi sana, will do that.
 
....SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??

Ever remaining,
Sakapal
Si wanaume wote. Pamoja na jitihada zetu za kujaribu kupata mpenzi ambaye mtakuwa na compatibility ya kiwango cha kuridhisha, lakini bado kuna compromise nyingi tu inabidi tuzifanye ili kutengeneza, kuboresha na kudumisha mahusiano/mapenzi. Kila upande ni muhimu kufanya compromise na jambo hili linawezekana kama nyinyi wawili mmesomana na kuelewana tabia zenu vizuri.

Nikiangalia haya malalamiko yako, napata hisia kuwa nyinyi wawili bado hamjajuana vya kutosha na pengine hakuna uwazi wa kutosha kati yenu. Ni vema pia mkajifunza masuala kadhaa ya kibaolojia na hata kisaikolojia na hasa tofauti zilizopo kati ya jinsia ya kiume na ile ya kike. Elimu hiyo inaweza kuwasaidia kujua kiini cha tofauti zenu na hivyo kuweza kuelewana, kuvumiliana na kuchukuliana kwa urahisi zaidi.
 
Kwanza umenichosha na story yako ndeefu . . . Lol(kiding).Wanaume wengine sisi ni wavivu wa kuongea na kusikiliza pia.Mimi mfano huwa sipendi sana mizaha,ni mara mojamoja sana ndo maana hata comedy si mpenzi.Nikioa nitamwambia mke wangu tabiia yangu hii ili wakati mwingine asiwe anakwazika,lakini nitajitahidi kumsikiliza mara nyingi ili asiboreke.Ukitaka wanaume tufurahi leta story za mipango ya hela utaona kama tutaongeza sauti ya radio.Ila kwa kuwa umeshajua hebu ufuate ushauri wa Kaunga,japokuwa wanawake kimaumbile mnapenda kusikilizwa!
 
Last edited by a moderator:
nyumba kubwa well said..
Kweli bwana kuna watu kuongea wamejaaliwa yaani wanajua namna ya kupangilia maneno mpaka basi..
Ninaye shemeji yangu kwa kweli ukifika kwake unabaki kucheka tu..she is truly a charming lady..
Bahati mbaya mume wake hapendi vile anavoongea..so, unakuta akianza stori zake broo anaanza kumtuma ili mradi amkate flow ya maongezi..Kingine nilichogundua kupitia huu uzi..wanaume wengi hawapendi kustorishwa na wake zao..
Na wanapenda ile ya one way traffic conversation..yaan mke awage wa kuulizwa na kuitikia tu..lol!!

my dear SnowBall u deserve my gift.....
Asante sana huo mfano wa shemeji yako nyumba nyingi ziko hivo, na hao wanaume wanaofanya hivo hawajui ni kiasi gani wanawakwaza wake zao. Just emagine mtu yuko in between the story then unamwambia hebu nenda chumbani kaniletee mawani yangu au ile charge ya simu yangu ya zamani. Tena anaweza kukutuma kitu ambacho kiko mbali ili utumie muda mrefu ukirudi story ingine ishaanza. Sasa utakuta yeye hajui kuongea na wageni anawawekea video waangalie utasema wageni kwao hawana video, watu skuhizi wakikutana ni kustorisha sio kama zamani unawatolea albam za picha waangalie na kuwawekea mikanda ya video lol wanaume wa namna hii michosho kwa kweli sio siri wala nn. Kama mnaosoma hapa mko hivi jirekebisheni.
 
nakusapoti sana kwani mtu na mwenzie lazima msomane (understand each other). Ni lazima ujue mwenzako anapenda mazungumzo ya aina gani. Kuna ambayo ni ya kina mama kwa mama ambayo hatuhitaji kuyasikia wala kuyaelewa. Mumeo/mkeo pigeni stori za familia yenu na mipango ya maendeleo yenu! Uepuke kusifia wengine kwani hubomoa badala ya kujenga. stori zinazomfanya mwenzio aone au ajiskie kuwa anatakiwa kuwajibika ni nzuri pia. However mimi sio mtaalamu wa mahusiano just my own experience
 
ha ha haaaa... yaan uko kama mke wangu...lakini mimi huwa namsikiliza...kiukweli sio kwamba hapendi kukusikiliza lakini inategemeana na kazi anayofanya mumeo coz kama ni kazi inayomtaka aconcetrate then by the time akirud home anakuwa amechoka sana...hakika anakupenda tatizo ni hilo tu uchovu. Hata mie kama kuna siku nimechoka sana namuambia plz naomba tulale...!!!
pole sana Sakapal, bt trust me anakupenda wala hajakuchoka tatizo ni stress tu za mjini.

at least nimepata moyo asante sana kamanda moshi
 
Nadhani umefanya research yako wrongly..
Itakuwa kitu cha ajabu sana kama unadate mtu ambaye hamna 'compatibility'..
Miongoni mwa vitu vinavyowafanya watu wawe pamoja ni hili la kustorishana..
Sikatai inawezekana kuna 'extreme cases' ambapo me au ke ni mwongeaji kuliko mwenziwe kiasi cha kupigiwa mfano..
But my brain tells me kwamba pale ambapo kuna mwanamke muongeaji kuna mwanaume muongeaji pia..
Sema kwa muktadha wa mleta mada inaonekana 'wameanza kuchokana'..yaan mume hana furaha tena na stori za mkewe

mmmh inatisha... hadi naogopa, hivi inawezekana mkiwa mechokana na kuzoeana wote mkawa na hamu ya kuflash back first days mnaanzana kama chachu ya kuamsha mapenz?
 
For what I know, men are different from women. Women are upto details. They would want to give each and every detail of their day! For men its different. They concentrate more on general terms! If you ask a man how was your day, 'it was good/ I had a great day' is more than enough response while a woman would want the details of how good it was! What is important is for both of you to sit down and talk! Good communication is a cure to many problems in a marriage! Let him know that it means a lot when you listen to him! And if he is a man loving you for real, will change for good.
 
Si kweli kwamba ni kawaida ya wanaume waongeaji kutopenda wanawake waongeaji.

Kuna wanaume waongeaji waliojaa vacuous talk, wamejaa majisifu kumpita Kiranga na kila mara wanataka waonekane wao wako juu (kumpita Kiranga, can you believe that?)

Kuna wanaume wengine wengi wa maneno na wanapenda wanawake wenye wingi wa maneno.

Mie mamaa wangu tukikaa hatuishi kuongea istilahi za Kiswahili, siasa, quantum physics, tamaduni za Watanzania kulinganisha na watu wa nje, etc.

Na heshi kuniburudisha kwa kila asemalo, maana ni kichwa. Na mie siishi kumpa vi quiz vya kiajabu ajabu, mara nimuulize maana ya maneno magumu ya kiswahili kuona kama anakikumbuka bado, mara kuongelea habari za Vladimir Putin na mkono wake wa chuma, mara muungano, mara familia zetu.

Basi ilimuradi karibu kila nitakalosema ni muziki masikioni pake, na yeye kila mara heshi kunishangaza kwa kunipa namna mpya ya kuangalia mambo, iliyojaa manzili, ucheshi wa shajara, haiba ya madaha, utanashati na mlahaka, nazaa zote za kike na nakawa iliyo hidaya maridhawa ya kuupa moyo wangu fanaka kuliko johari na libasi, iso dhihaka, uzembe wa kufikiri wala inda na kisirani.

Kwa hiyo twapeana utumbuizo murua sote, bila kashfa.

Na kukanusha maoni yako.

:clap2::clap2::clap2:
 
For what I know, men are different from women. Women are upto details. They would want to give each and every detail of their day! For men its different. They concentrate more on general terms! If you ask a man how was your day, 'it was good/ I had a great day' is more than enough response while a woman would want the details of how good it was! What is important is for both of you to sit down and talk! Good communication is a cure to many problems in a marriage! Let him know that it means a lot when you listen to him! And if he is a man loving you for real, will change for good.
 
Mibazazi ishaanza.

Halafu inavunga kuvunga (i am kiddin)

Taratibu Kiranga, mimi na SnowBall tumetoka mbali na tunajuana vilivyooo, nimesikitika sana kumuita mpenz wangu bazazi, if u can say sorry pls...
 
Sio wanaume wote hawataki kusikiliza story za wake zao ila ni kwamba wanaume wengi hawapendi story za umbea au zisizo na tija. Binafsi napenda kuongea sana, nadhani ni kama wewe, tena siku nikinyamaza lzm ataniuliza mbona leo hivyo unaumwa? nikimwambia nipo normal atakataa ni kuniambia mbona leo huongei, huko ofisini kwema? So hapo kwako nilichokiona jaribu ku-edit story zako. labda vp jmosi tutaenda site, au kutafuta mashamba, au nafikiri tukifanya hivi tutapata pesa, au what ever tu ili mradi zinahusu familia yenu. Mimi ndio huwa story zangu, na haziishi for sure. sababu nisipozungumza kwenye gari nitazungumza wapi, home jiko linanihitaji, watoto na ukiingia chumbani inabidi uwajibike kile kilichokutoa kwenu na kukuleta hapo kwa mume. Na usitumie muda wa malovidave kuongelea viwanja hapo napo utachemka mamii.
 
Back
Top Bottom