Story za mtaani kuhusu umafia wa madalali

nae ni zofle anakaaje na hyo ela ndani kwanza anapokeaje malipo kwa cash....
 
Kuna mzee mmoja alikuwa dalali maarufu sana mkoani Morogoro, jina linahifadhiwa. Alimuuzia mmasai msikiti mkubwa pale Boma road watu wakiwa ndani wanaswali...nilijiuliza inawezekana vipi hii lakini ilikuwa too late, mtu kishauziwa msikiti na watu wake, huyu mzee sasa hivi eti ni mkandarasi huko Singida anapiga hela za barabara, anazeeka na uhuni wake
 
Katika principal ambayo huwa Nina iheshimu duniani ni Kuneshimu makubaliano.

Kinyume na hapo unajitafutia Matatizo
 
Acha kujidanganya wewe, kawaulize matajiri wakubwa mjini wanaotumia dark art Kama dalali anadhulumiwa

Ukileta dark art unapewa lead!
1. Kuna watu wanamuamini Mungu

2. Kuna watu wamechanjiwa hata iweje huwaingii

3. Kuna watu wana uchawi hata kuliko hao
 
mmmh
 
Mnawakuza sana hao madalali.

Mnawekeana makubaliano, akivunja mnaweka terms upya.

Nimetaka mteja wa 100m wewe umeleta wa 400m, mnaanza upya akubaliano.
Upya kivipi wewe?.
kisa umeona hela kubwa? umehusika kumshawishi mteja akafika dau lililozidi?
Kama kuleta mteja ni rahisi si muwe mnawatafuta wenyewe?
 
Kuna jamaa mmoja alikuwaga raisi nchi flani akaleta tamaa ya makinikia, akawadangaya watu wake kuwa wanatakiwa wapewe Noah mojamoja kila mtu 😂😂😂. Alikuaga na akili kama za kwako siui kapotelea wapi sikuizi.

Greed imeonywa hata kwenye maandiko matakatifu!
 
but all in all madalali sio watu wazuri. They know alot
Hapa nimekuelewa zaidi

BTW wenye mali wanapaswa kuheshimu na kuzingatia makubaliano waliyokubaliana na Madalari.
 
Makubaliano yawe percentage bei ya mauzo kuepusha mfarakano.
 
Mimi nishawahi kuwazingua madalali na hawajaniambia kitu.Nchi ina taratibu za kuendeshwa.
Pia tukiamua kuishi kihuni na mimi namtumia dalali watoto wa kihuni(commando Yosso)

Haikuwa ishu yenye pesa ya maana! Waliona unanuka shida tu, hela huna wakakupotezea tu!
 
Upya kivipi wewe?.
kisa umeona hela kubwa? umehusika kumshawishi mteja akafika dau lililozidi?
Kama kuleta mteja ni rahisi si muwe mnawatafuta wenyewe?
Kama dalali ukipata mteja wa pesa ndogo chini ya makubaliano unamheshimu mwenye mali unampigia simu unamfata mnazungumza upya kwann ukipata wa pesa kubwa usimheshimu pia mkaizungumzia hiyo pesa mpya ambayo ni kubwa kuliko makubaliano?
 
Yani unalinganisha mafia anayefanya biashara za mazao, ng'ombe, pombe na vitu haramu akapata mamilioni akajenga kisha baadae akauza VS jamaa anayetafuta wanunuzi akipata kazi.

Hii nchi mafia wako wengi na kati ya hao dalali hawapo hata hawatambuliki. Siku nyingine mtatutisha na wapiga debe
 
hapo naona mkubaliane kua cut yake ni 25% na min price ni 100.
Huu ndio utaratibu. Eti unakaa Kinondoni ulete umafia mbele ya wale Wahindi na Waarabu wenye godowns, wachimba migodi wastaafu, makanali wakiuza daladala zao au wafanyabishara sugu wa kwenda Sheli sheli na DRC. Sasa kipya kwao nini si ndio maisha yao, unawaza hiki wanawaza kile
 
Tatizo watanzania wengi hawazingatii makubaliano .Heshimu mlichokubaliana .Uswahili hautakiwi.mumekubaliana milioni 25 akiuza hata bilioni moja chukua chako zilizozidi mwachie

Kukosa uaminifu kwenye makubaliano kumesababisha madalali wengine kubuni mbinu mpya kukwepa Hilo akipata mnunuzi mfano wa nyumba ya milioni 25 anayetaka kununua kwa bilioni moja anachofanya anaenda kopa benki milioni 25 anampa ndugu yake anakuja nunua hiyo nyumba kwa milioni 25 halafu ukishampa hati zote wanaiuza kwa bilioni moja.Wanaenda kufuta mkopo wanaweka pesa iliyobaki kibindoni wanakuacha na ujinga wako

Njia nzuri kwenye mkataba andikianeni hivi kuwa nyumba hii usiuze chini ya milioni 25 chochote kitakachozidi juu dalali utachukua nusu na Mimi nusu na muandikishane kisheria kabisa .Akiuza usiwe na wivu Tena kuwa ohh anatajirikia kwangu . Biashara yeyote ni kutajirishana mfano wewe waweza kuwa unauza basi faida yako Hilo basi ukiuza Ni milioni kumi Sasa ukaona uliyemuuzia anafanya biashara ya basi anapata faida ya milioni 50 kwa mwezi usibweke kuwa unamtajirisha na wewe kakutajirisha kwa kununua chako
 
Umemaliza kila kitu Uzi ufutwe Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…