Nakumbuka kipindi niko primary std 5 au 6, kuna ndugu yetu alikuja home.... alikua mtu wa vyombo sana so ikanunuliwa konyagi kwa ajili yake maana hakuna mwingine alikua anatumia hyo kitu pale nyumbani.
Hyo siku baada ya kunywa kiasi nikatumwa kwenda kuitunza, sasa nmefika nlipotakiwa kuiweka nikaiangalia then nikawa natamani kujua ina ladha gani, akili ya utoto ikaniambia onja[emoji23] basi nikamimina kwenye kifuniko chake then nikabugia daah sitasahau hyo siku niliunguaaaa kuanzia kwenye koo had ilipofikia tumboni nikawa naiskilizia.
Nlitamani kulia kuomba msaada ila nlijua kitu ambacho kingenipata so nikajikaza nkaenda kujipooza na maji kuzima moto tumboni.
Since then nkawa muoga kudokoa vitu nisivyovijua.