Story za udokozi

Story za udokozi

Hahah mmenikumbusha mbali sana,pindi nipo primary school nilikuwa natembea na kijiko kidogo/tea spoon kwa ajili ya kulambia sukari kabatini yaani nikitoka shuleni au mpirani nalamba sukari.

Sasa kuna siku nililamba sukari jioni nilivyomaliza sikuifunika asubuhi nikaamka nilambe kidogo kushtuka nimekula mavi mende vyeusi vidogo vidogo nikaacha kulamba sukari
 
Nakumbuka kipindi niko primary std 5 au 6, kuna ndugu yetu alikuja home.... alikua mtu wa vyombo sana so ikanunuliwa konyagi kwa ajili yake maana hakuna mwingine alikua anatumia hyo kitu pale nyumbani.
Hyo siku baada ya kunywa kiasi nikatumwa kwenda kuitunza, sasa nmefika nlipotakiwa kuiweka nikaiangalia then nikawa natamani kujua ina ladha gani, akili ya utoto ikaniambia onja😂 basi nikamimina kwenye kifuniko chake then nikabugia daah sitasahau hyo siku niliunguaaaa kuanzia kwenye koo had ilipofikia tumboni nikawa naiskilizia.
Nlitamani kulia kuomba msaada ila nlijua kitu ambacho kingenipata so nikajikaza nkaenda kujipooza na maji kuzima moto tumboni.
Since then nkawa muoga kudokoa vitu nisivyovijua.
🤣🤣😁 Ulikuwa unahisi kama unataka kufa kufa vile
 
Mnauliza kudokoa! Nakumbuka nilikuwa nachukua nyama kwenye sufuria naweka kwenye mfuko wa suruali basi huyoo naenda zangu nje?
 
Kwa wahaya tumefanya sana haka kamchezo kakudokoa senene
 
Watoto wa kike ni wahanga sana. Dada yangu alikuwa na hii tabia sana.😀😀

Me nilikuwa mrambaji mzuri sana wa sukari. Hii tabia mpaka dogo kaja kuwa nayo. Sema tu vile nakuwa si mfatiliaji maana anaramba halafu anaacha ushahidi.
 
Kuna siku nilikua kwa mamdogo kama darasa la5 au 6 akachinja Bata kuna wageni walikua wanakuja na nilikuwa sijawahi kula hivyo niliipania balaa,basi akanyonyoa alivomaliza akasema ibabue ye akaenda kununua chumvi,hapo ndo balaa lilipoanza,..ikawa badala ya kubabua naivisha upande afu nakata nakula kuja kushtuka naona kifuani na mapajan mifupa inaonekana,kuua Soo ikabidi nimkate Kate nitenge vipande hata havikueleweka,aliporudi akachungulia sufuria na kuguna mmh! nlimuona kama mkubwa kumbe mdogo ,nilipumzika kwa muda harakati zangu za udokozi
[emoji23][emoji23][emoji23]lamba lamba humaliza buyu la asali[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dadeq mara paaap unashtuka umebakisha shingo tu
 
Back
Top Bottom