Wote mliochangia siwapingi. Ulikuwa tu ni ushauri. Inabidi juhudi za ziada zifanyike ili kuzigawa kura za Wasukuma.
Nimetoka kuangalia video hii hapa chini, nimeona amewasalimu kwa lugha yao, hapo safi. Kilichobaki, wale wanaobaki huko Sukumaland kuendelea na kampeni, wajaribu kuzingatia ushauri wangu.
Ushauri mzuri zaidi ni Lisu kumhakikishia mkubwa wa Polisi nafasi yake mpaka astaafu. Pia Mkubwa wa JWTZ asimame nyutro kwani General ni international rank asijihusishe na siasa.
Kwa sasa Lisu atafute namna ya kuungwa mkono na vyombo vya Dola kwa kuanza safu nzima na sio kuwatisha kuwa atavunja jeshi lile Mara nitalifumua n.k. Wengi wanahofia nafasi zao kwani CCM imekua ikiwatumia kama dili lao ndio maana baada ya uchaguzi hawana habari bao tena .
Mpaka sasa Lisu ameshinda kwenye suala la kura. Cha msingi ni kuanza sasa kuwatafuta watu wenye imani kubwa ili wawe wanaendelea kusoma dua njema kwa wasimamizi wema na mbaya kwa wasomamizi wabaya ili wasije wakafaidika kwa udhalimu wao.
Hata wabunge na madiwani watakaopitishwa kwa dhulma nao pia wasomewe dua mbaya wasije wakanufaika kwa dhulma yao.
Albadir zianze kusomwa sasa kwa Wakurugenzi na wasimamizi waliovuruga uteuzi wa wagombea na kuwaengua watu kwa dhulma bila kufuata sheria kwa haki.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Haki.
Lisu atawapiga CCM Nyanda za juu kusini, atawapiga Kaskazini, atawapiga Kigoma na Mpanda ,atawapiga ,Morogoro, DSM,atawapiga ,Lindi na mtwara, atawapiga ,Unguja na Pemba, atawapiga. Atawapiga. Mara, Atawapiga Mwanza, atawapiga. Geita Atawapiga Kagera,Atawapiga Singida .
Kifupi Lisu atashinda kwa kura za kimbunga maeneo hayo. Kwingine watatoka droo na CCM.