Strength Of A Woman: Kutana na mhudumu wa ndege ya Pan Am Flight 73 aliyepigwa risasi mgongoni akiwa amewakumbatia watoto 3 na passports 41 za U.S.A

Strength Of A Woman: Kutana na mhudumu wa ndege ya Pan Am Flight 73 aliyepigwa risasi mgongoni akiwa amewakumbatia watoto 3 na passports 41 za U.S.A

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Strength Of A Woman: Kutana na mhudumu wa ndege ya Pan Am Flight 73 aliyepigwa risasi mgongoni akiwa amewakumbatia watoto 3 na passports 41 za U.S.A

118211270_3225888980842000_3050236220584413685_o.jpg


Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

Mhudumu mmoja wa ndege dada mrembo sana aliyejulikana kwa jina la Neerja Bhanot, shabiki kindakindaki wa Rajesh Khanna, mara nyingi sana alijikuta akiota ndoto ambayo amejikuta akishiriki kikamilifu na kutimiza majukumu yake ipasavyo. Siku moja katika hali ya kufikirika, alimuomba mama yake mzazi ampe mpango madhubuti wa vitendo wa nini cha kufanya endapo litatokea tukio la utakaji wa ndege ya abiria.

Mama yake akamwambia, "Ikiwa kitu kama hicho kitatokea siku moja, basi wewe toroka tu" kauli ambayo Neerja akiwa mwenye ujasiri wa hali ya juu kabisa alijibu kwa kusema, "Ikiwa akina mama wote wanafikiria kama wewe, ni nini kitatokea katika nchi? Afadhali nife kuliko kukimbia kama muoga”

Maneno hayo yalitimia mnamo tarehe 5 Septemba, 1986 wakati Bhanot alipokufa wakati akiokoa abiria kwenye ndege aina ya Pan Am Flight 73, iliyokuwa imetekwa nyara na magaidi wakati iliposimama kwa muda huko jijini Karachi. Lakini, 'shujaa yule wa kike kiboko ya watekaji' alikuwa tayari ameshapitia shida kama sehemu maisha yake ya kila siku

Neerja-Bhanot-BW.jpg


Alizaliwa kwa Harishi na Rama Bhanot mnamo tarehe 7 mwezi Septemba mwaka 1963 huko Chandigarh, alikuwa dada kipenzi wa familia yake, ambayo ni pamoja na ndugu wawili, ambao wote kwa pamoja walimuita kuwa ndio NGUZO yao.

Alisoma Chandigarh na baadaye huko Mumbai, hapo ndipo alipokuwa anafanya kazi ya "modeling", akitangaza bidhaa kama vile dawa ya meno ya Binaca, Forhans na Godrej.Akiwa na umri wa miaka 19, alikuja kuolewa na mhandisi wa masuala ya baharini na kisha akahamia Sharjah, U.A.E

Baada ya miezi miwili ya unyanyasaji, pamoja na njaa, matusi na vitishi, Bhanot aliondoka kwa mumewe, akarudi Mumbai na aliamua kuwa mhudumu wa ndege. Bhanot aliteuliwa kuwa msaidizi muandamizi wa ndege ile aina ya Pan Am Flight 73 ikiruka kutoka Mumbai kwenda Marekani siku hiyo ya majanga ya Septemba

Wakati wa iliposimama huko Karachi, watu wanne raia wa Palestina wenye silaha kali za kivita kutoka katika kundi la magaidi la Abu Nidal waliteka nyara ndege hiyo, ambayo ilikuwa imebeba abiria karibu 380 pamoja na watumishi wa ndege hiyo wapatao 13

images (16).jpg


Bhanot alitoa taaifa ya onyo kwa wafanyakazi waliokuwa katika chumba cha marubani kwa kutumia ishara maalum ambazo wahudumu hufundishwa kuwasiliana na marubani, hali ambayo iliwaruhusu marubani wale wa kimarekani kufunga mlango wao na hivyo, kuwezesha kutua salama kwa ndege ile.

Wateka nyara wale waliokuwa wamekasirika alimuagiza kukusanya passports za abiria wote. Baada ya kugundua kuwa malengo makuu ya magaidi wale yalikuwa ni kuwatambua kisha kuwaua raia wa Marekani, Bhanot na wafanyakazi wake (yeye ndiye aliyekuwa boss) walificha passports hizo chini ya viti na kwenye kapu ya takataka.

Kuwepo kwake katika hali ya utulivu pia, inasemekana, kulizuia wasiwasi na kiwewe miongoni mwa abiria na wafanyakazi wa shirika hilo kwa muda wa masaa kama 17 hivi wakati huo huo alikuwa anahudumia vyakula kama sandwichi pamoja na vinywaji na kujaribu kuongeza morali zao ili awaondoe uoga, hata pale magaidi hao walivyoamua kumuua abiria mmoja na kumtupa nje ya ndege.

Wakati wateka nyara walipoona sasa wamevumilia vya kutosha na kuamua kuanza kutumia silaha zao, Bhanot alifanya kazi haraka na nguvu zote kuwaokoa abiria wengi kadri awezavyo kupitia dirisha la dharura. Aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akiwalinda watoto watatu wa Kimarekani dhidi ya ukatili wa magaidi wale.

images (17).jpg


Kati ya Wamarekani 44 waliokuwa ndani ya ile ndege, 42 waliokolewa kutokana na uwezo mkubwa sana wa kiakili wa Bhanot. Walionusurika katika shambulio hilo walimpa dada yule mhudumu jina la masihara la 'Heroine wa the Hijack' yaaani "shujaa wa kike kiboko ya watekanyara".

Ujasiri, utulivu wa Bhanot pamoja na uwezo wake wa kufanya maamuzi ya haraka ndani ya muda mchache vyote kwa pamoja vilisababisha yeye kupewa tuzo ya heshima sana baada ya kifo chake (posthumous Medals of Honor), ikiwa ni pamoja na tuzo za Ashoka Chakra - tuzo kubwa zaidi ya amani ya India.

Alikuwa mwanamke wa kwanza na mpokeaji mdogo zaidi wa tuzo hiyo. Hadithi yake inaendelea kuhamasisha na kuwapa changamoto wanawake wachanga, na ili kukumbuka uhodari wake, familia ya Bhanot ilitumia pesa kutoka shirika la ndege la Pan Am kuanzisha taasisi ya kutoa msaada katika jamii iliyojulikana kama Neerja Bhanot Pan Am Trust.

Taasisi ile huwa inatambua na kutoa tuzo kwa wanawake wa India wanaopambana na kushinda dhuluma za kijamii na wahudumu wa mashirika ya ndege ambao huenda zaidi ya wito wao wa kazi na kufanya mambo makuwba wakati wa huko angani.

Neerja_Bhanot_2004_stamp_of_India.jpg


Katika tuzo zingine za heshima, Bhanot alipewa tuzo ya Tamgha-e-Insaniyat na serikali ya Pakistan, na mnamo mwaka 2004, shirila la taifa la Posta huko nchini India likatoa stamps maalum kama sehemu ya kumbukumbu yake.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa idara ya ujasusi ya KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja maarufu sana katika hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus.

Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

Nipo ninaiandaa hiyo story alafu nitaiweka humu HARAKA SANA.
 
Hakika alikuwa jasiri.kanjibhai walishaigiza na filamu kuhusu hilo tukio
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja huko Belarus aliyepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979. Nipo ninaiandaa hiyo story alafu nitaiweka humu HARAKA SANA.
Naisubiri hiyo story
 
Poa..nipo rafiki
Nilikuwa ninakumulika katika THREAD yetu ile ya Kivule kwa maana ninaona siku hizi umepotea. Pole kwa majukumu pia ninajua ndio yamekubana mpaka umepotea kidogo.
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus.

Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

Nipo ninaiandaa hiyo story alafu nitaiweka humu HARAKA SANA.

Pamoja mkuu
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus.

Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

Nipo ninaiandaa hiyo story alafu nitaiweka humu HARAKA SANA.
kamanda umesahau tangazo lako au mzigo umeisha afande?
 
Back
Top Bottom