Kwani Tanzania ni mwiko kuwa na wasanii walio juu hata 100. Hivi hizi akili za kutaka msanii mmoja ndio awe juu mmesitoa wapi?
Kwani Zuchu akiwa juu, nandy akiwa juu na wakitokea wasanii wengine wakitokea hata 100 Nyie huwa mnaumia Nini.?
Acha watu wafanye kazi kijana. Fanya kazi. Nandy ana maisha anaweza kukuajiri ukawa houseboy wake. Zuchu ana maisha anaweza kukuajiri uwe mtu wa Garden kwake.
Huo muda wa kuchambua riziki za binadamu wenzio na kuzi underrate ni Bora ujikite mtaani kutafuta Mia za kula.
Najua una maisha magumu kijana, umri unakukimbia kazi kuja kudiscus watoto wa kike. Utakuja kushtuka muda umeenda huna lolote.