Striker kama huyu anaejituma na kutegemewa ktk club yake utamuachaje kwenda Russia?

Hamnaga mshabiki wa Argentina bongo wewe ni shabiki wa Andunje
 
Aise! kumbe aliwahi kuichezea Barca,, nilikuwa sijui...
Mauro Icardi ni product kutoka La Masia na alitabiriwa kuja kuwa striker mkali tatizo kubwa lilikuwa nidhamu ndio maana Barca walimuacha aondoke kiulaini
 
Mkuu belo...hii formation ingetufaa sana 4-2_3_1
Mpira wa siku hizi forward ndio wanaanza kukaba Messi/Dybala/Icardi wote ni free player kuwachezesha wote pamoja timu hai-balance bora kina Di Maria/Correa wanaweza kukaba unafikiri kwa nini Pep anampenda Jesus badala ya Aguero

Tatizo la Argentina wamekosa kocha anayeweza kujenga morali ili wachezaji waweze kupambana wana wachezaji wengi wazuri lakini hawana timu
 
Kweli kabisa mkuu Argentina ni mkusanyiko wa wachezaji tu Ila hawajitumi kabisa..World cup ya mwaka huu siwapi nafasi sana.

Hapa ndipo ninapowakubali Wajerumani,Wanajituma na morali Yao ipo juu sana.
 
Kweli kabisa mkuu Argentina ni mkusanyiko wa wachezaji tu Ila hawajitumi kabisa..World cup ya mwaka huu siwapi nafasi sana.

Hapa ndipo ninapowakubali Wajerumani,Wanajituma na morali Yao ipo juu sana.
Argentina,Brazil,France,Spain hizi timu zina wachezaji wazuri wengi sana huwa wanakosa makocha wa kujenga morali na kutengeneza timu Brazil wana kocha mzuri sana wanaweza kufika mbali sana

Germany,Italy,Egypt wanaweza kutengeneza timu
 
Bila kuwasahau Belgium..hawa nao ni Simba wa karatasi tu,majina makubwa Ila wanafungwa na Wales..

Majina hayachukui kombe bila morali na Chemistry kwenye Timu.Spain nafkiri kutokana na kupata wachezaji Wengi toka Barcelona na Madrid wanakuwa rahisi sana kutengeneza Chemistry kwenye Timu Yao ya Taifa..

Ila still nawavulia kofia sana Wajerumani kwa Uzalendo kwenye Timu Yao ya Taifa..huwezi kuwaona akina Ozil wakitegea kama wanavyofanya kwenye Club Yao..

NB; WAKUU HATUNA UZI KUELEKEA KOMBE LA DUNIA TUKABADILISHANE MAWAZO....Siasa zinachosha.
 
Kwa case ya Dybala, nadhani ni yeye mwenyewe (Dybala) alisema kuwa hawezi kucheza na Messi maana wana style inayofanana mno kiasi kwamba yeye mwenyewe haoni akiwa huru kufurukuta.

Kocha wao akamtetea kuwa alichokisema hakikuwa na nia ya kuwa anamchukia Messi bali hata yeye kocha ni ngumu kuwapanga pamoja kwani wana style inayofanana mno.

Kuhusu kwenda WC naamini Dybala ataitwa ila atakuwa benchi muda mrefu. Ila ni muhimu yeye kuwepo maana baada ya mashindano haya nina imani Messi atatundika daluga kuitumikia timu yake ya taifa. Nafasi hiyo itabaki kwa Dybala labda ndani ya miaka minne hii atokee mchezaji bora kuliko yeye tena.
 
Yani inakera sana kuona wachezaji wenye vipaji wakiachwa au kuwekwa benchi kwenye national teams

Mfano kama Brazil eti Gabriel Jesus anamweka bench Roberto Firmino!! Si ajabu sana hii?
 
Uko sahihi mkuu nankume! Lakini kumbuka huyo huyo Higuain si ndiye aliikosesha ubingwa wc 2014, coppa america na Chile pia,, tazama kwenye club zake alizocheza since REAL MADRID-NAPOLI and now JUVENTUS jamaa kaperform vizuri sana...ila kwenye tim yake ya taifa sioni akifanya maajabu hayo.
 
Yani inakera sana kuona wachezaji wenye vipaji wakiachwa au kuwekwa benchi kwenye national teams

Mfano kama Brazil eti Gabriel Jesus anamweka bench Roberto Firmino!! Si ajabu sana hii?

Hizo ndio tim za america ya kusini mkuu,na kombe watakuwa wanaliona kwenye tv...I'm Argentina fan,, but Mjerumani nampa nafasi kubwa ya kutwaa,, Spain kwa mbali...
 
Yani inakera sana kuona wachezaji wenye vipaji wakiachwa au kuwekwa benchi kwenye national teams

Mfano kama Brazil eti Gabriel Jesus anamweka bench Roberto Firmino!! Si ajabu sana hii?
Inategemea kocha anataka nini na mfumo upi anatumia kulingana na mchezaji...

Mimi namuona Jesus ni striker aliyekamilika kulinganisha na Firmino..Japo game moja wanaweza kucheza kwa kubadilishana
 
Mkuu! Kwa formation ya 4-2-3-1 mbona inawezekana kabisa...De Maria kushoto-Dybala kati-Messi kulia...mbele Lcardi,, Lanzini or Aguero...ila tusiwategemee wote kwenye ukabaji...Aguero mzito, Dybala nae sio mkabaji sana
 
yeah ni vgumu kucheza timu moja na messi ukafanya mambo makuubwa kuliko angalia hata benzema ni bonge la striker lkn anaonekana wa kawaida sababu ronaldo yupo, sema kila mtu na mtazamo wake ila striker km icardi,belloti,imobille hawa jamaa wanafit timu znazocheza mipira migumu km italy vile au km club basi juve,inter na man u, mi naona sampaoli yuko sahihi kumwacha ingawa anaweza kumwita yy au dybala coz ya hii uncertainty ya aguero, mi nmemwona icardi kwe baadhi ya mechi za kufuzu WC yaani unaona kabisa yuko isolated uwanjani ile mipira yake ya kusubir haipatikan kabisa
 
Mkuu! Kwa formation ya 4-2-3-1 mbona inawezekana kabisa...De Maria kushoto-Dybala kati-Messi kulia...mbele Lcardi,, Lanzini or Aguero...ila tusiwategemee wote kwenye ukabaji...Aguero mzito, Dybala nae sio mkabaji sana

Nadhani umejijibu kuwa inawezekana kuwapanga lakini italeta ugumu kwenye performance zao.
 
Anatembea na wake za wachezaji wenzake, hana adabu hata dyabala atajaza idadi hawezi kucheza ,hayo ndio maneno ya sampaoli pia ,sampaoli anasema waliangalie kombe la Dunia wakiwa holiday. Kuna Aguero na gonzelo Hakuna visingizio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…